Skip to main content

Serikali bado inayo fursa kurekebisha kasoro za Sensa

KATIKA hali isiyotegemewa, zoezi la Sensa ya watu na Makazi iliyoanza juzi nchini kote, imekumbana na kasoro na vikwazo mbalimbali, huku tatizo kubwa likiwa ni uhaba wa vifaa na wenyeviti wa mitaa kugoma kuwaongoza makarani kuendesha zoezi hilo kwa madai ya kutolipwa posho.
 
Mbali na tatizo la baadhi ya wananchi kugoma kuhesabiwa ambalo tayari linafahamika kwa mamlaka za kiserikali, uchunguzi wa gazeti hili uliofanyika katika mikoa mbalimbali pia umegundua kwamba kasoro nyingine zinazolikabili zoezi hilo hazikutegemewa na  zilijitokeza tu mara baada ya zoezi hilo kuanza juzi. 
 
Tunaweza kusema kwamba kasoro zilizojitokeza ni za aina mbili. Moja ni kasoro zinazoweza kuwekwa katika kundi la kasoro zilizosababishwa na mamlaka za kiserikali. Pili, ni kasoro zilizosababishwa na wananchi wenyewe, wakiwamo viongozi wa mitaa ambao walishindwa kuwahamasisha wananchi katika ngazi hizo kuhusu zoezi hilo la Sensa ya Watu na Makazi.
   Pamoja na kusema kwamba mamlaka za kiserikali hazipaswi pekee kubeba lawama hizo, bado tuna kila sababu ya kusema kwamba mamlaka hizo lazima zibebe nyingi ya lawama hizo, hasa baada ya kufanya uchambuzi wa kina wa kila kasoro iliyojitokeza. Kwa maneno mengine, hata pale panapoonekana kwamba kasoro zilizojitokeza zilitokana na wananchi wenyewe, bado kuna dalili zinazoonyesha kwamba mamlaka za kiserikali zilichangia kasoro hizo kwa namna moja ama nyingine.
 
Tutatoa baadhi ya mifano. Katika baadhi ya mikoa, wenyeviti wa vitongoji na vijiji waligoma kushiriki katika  zoezi hilo baada ya Serikali kushindwa kuwatengea posho kama ilivyofanya kwa makarani na wasimamizi wa Sensa. Pamoja na kupiga filimbi ya kuanza kwa zoezi hilo, kwa maana ya kuashiria kwamba matayarisho ya zoezi hilo yamekamilika, Serikali ghafla ilijikuta ikiwa na masuala kadhaa muhimu ambayo awali ilikuwa haikuyatilia maanani.
   Baada ya Serikali kushtuka saa za ‘lala salama’ na kusema ingewalipa posho kwa ushiriki wao, ilibidi iongeze kiwango cha posho baada ya wenyeviti hao kuzikataa kwa madai kwamba zilikuwa hazitoshi. Hapa tunadhani Serikali ilifanya makosa kwa kutotambua mapema ukweli kwamba makarani wa Sensa wasingeweza kufanya kazi hiyo bila kuandamana na viongozi hao kutoka kaya moja hadi nyingine na pia kwamba viongozi hao wasingefanya kazi hiyo bila malipo.
 
Hivyo, kitendo cha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa mkoani Katavi juzi,  kuwatangazia  wenyeviti hao wa vijiji na vitongoji kushiriki kwenye zoezi hilo na kuwaahidi kwamba wangelipwa fedha zao, kilionyesha pasipo shaka kwamba Serikali ilikuwa imejisahau kuhusu ushiriki wa viongozi hao katika zoezi hilo muhimu.  Kutokana na hali hiyo, inaonekana kwamba pengine Serikali haikuwa imetenga katika bajeti yake fedha za kuwalipa viongozi hao.
 
Tumeshangazwa pia na taarifa kwamba katika baadhi ya mikoa, makarani wa Sensa walitishia kugoma siyo tu kutokana na kutolipwa posho zao, bali pia walizilalamikia kamati za Sensa kwa kuchelewesha vifaa vya zoezi hilo katika vituo vyao, kwa maana ya vitambulisho, sare na dodoso na kusema wasingeruhusiwa kuingia katika kaya yoyote pasipo kuwa na vifaa hivyo. Katika baadhi ya mikoa, zoezi hilo lilikwamishwa na mwamko mdogo wa wananchi ambao walionekana kuendelea na shughuli zao za kilimo na ufugaji kama kawaida wakidai walikuwa hawajui kinachoendelea.
 
Tumeambiwa kwamba katika baadhi ya sehemu, kukosekana kwa wakalimani kulisababisha matatizo makubwa, hasa katika jamii za wafugaji wa jamii ya Kitaturu na Wahdzabe kutokana na kushindwa kutafsiri dodoso. Kasoro hiyo pia ilijitokeza katika mikoa ya Arusha na Mwanza ambako wananchi wengi, hasa jamii za wafugaji zinazoishi katika maeneo ya pembezoni walionyesha kutokuwa na uwezo wa kuelewa dodoso zilizokuwa katika lugha ya Kiswahili.
 
Hata hivyo, sisi tunasema Serikali bado inao uwezo na muda wa kutosha kumaliza kasoro hizo zilizojitokeza, ikiwa ni pamoja na kushawishi, badala ya kutumia nguvu, wananchi waliosusia Sensa ili washiriki katika zoezi hilo muhimu kwa taifa.

Popular posts from this blog

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2013 wilaya ya tanga mjini pekee!!!

ARAFAH ENG-MED PRIMARY SCHOOL - P2007029 AVICENNA ENG -MD PRIMARY SCHOOL - P2007051 AZIMIO PRIMARY SCHOOL - P2007032 BOMBO PRIMARY SCHOOL - P2007001 BURHANI ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007055 CHANGA ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007033 CHANGA PRIMARY SCHOOL - P2007002 CHUDA PRIMARY SCHOOL - P2007034 CHUMA PRIMARY SCHOOL - P2007003 CHUMBAGENI PRIMARY SCHOOL - P2007004 DARAJANI PRIMARY SCHOOL - P2007005 DAYSTAR ENG - MD PRIMARY SCHOOL - P2007053 DONGE PRIMARY SCHOOL - P2007035 EBEN EZER ENG- MD PR SCHOOL - P2007048 ECKERNFORDE ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007044 GOFU-JUU PRIMARY SCHOOL - P2007006 INDIAN OCEAN ENG-MED PR SCHOOL - P2007049 JABIR BIN ZAID ENG- MED PRIMARY SCHOOL - P2007052 JUHUDI PRIMARY SCHOOL - P2007036 KANA CENTRAL ENGMED PRIMARY SCHOOL - P2007054 KANA PRIMARY SCHOOL - P2007007 KISOSORA PRIMARY SCHOOL - P2007008 KOMBEZI PRIMARY SCHOOL - P2007009 KWAKAEZA PRIMARY SCHOOL - P2007026 KWANJEKA PRIMARY SCHOOL - P2007010 MABAW...

MAJINA YA WASHIRIKI NA WA WEZESHAJI WA FILM YA HOUSE GIRL!

CAST SELEMANI MOHAMED / BUNTO ANDREW / C-O YORAM MWETA / MGANGA MWANTUMU / MKE WA C-O JOHN / MCHUNGAJI BI FURURATU / JINI WAOMBOLEZAJI SAUMU HUSENI HASHIMU BABA RASTA MAN YOHANNA TAMILWAI SAIDI MWALUBADU SEMY STIR SELEMANI MOHAMEDI  AND ANDREW C-O LOCATION ATHUMANI HAMADI MAKE UP MWASHAMBA RAMADHANI BEDUI DEREVA DAUDI SPOONSER SAIDI SHABANI AND THE FRESH2012 GLOB SOUND PRODUCER J-B LIGHT YOHANNA TAMILWAI THENK YOU THE FRESH ENERTAINMENT AND THE FRESH2012 BLOG CONTACTS 0653785027 +255714091786 ZAIDI TEMBELEA www.the-fresh.blogspot.com ADRESS Thefresh@ymail.com AU Saidshabani60@gmai.com

Video: Blackchild – Put Inside

David Abdulichel, also known as BlackChild is a Ghanaian from Asanti origin, born and raised in Lagos Nigeria. BlackChild, who is a recording artist, song writer and performer started his music career back in 2000 and since then has released four singles. He has also worked with top producers in Nigeria such as Fliptyce, Spanky, Meca E & BrainMix to mention but few. BlackChild Abdul rose to prominence with his hit songs “Treasure”, “Ele” featuring Rock Steady, “Could It Be Love” featuring Cartiar, “All I Need” featuring Solid Star. This time around he comes out with “Put Inside” which sees him delivering lines in french and his native language and is steadily generating buzz and enjoying airplay on radio stations within and outside Lagos. Listen up!