Skip to main content

WAFANYAKAZI WA SUPERMARKET HUKO MOSHI WAANDAMANA KUPINGA RUSHWA YA NGONO WANAYOOMBWA NA BOSS WAO



Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama 

WAFANYAKAZI wa Supermarket ya Nakumatt, iliyopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wameulalamikia uongozi wa duka hilo kwa madai ya kuwanyanyasa na kuwaomba rushwa ya ngono.

Wafanyakazi hao ambao tayari walishafikisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama walidai wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya unyanyasaji ikiwemo kuombwa rushwa ya ngono na Meneja Mkuu na na msaidizi wake.

Walisema imekuwa kawaida kwa kila msichana anayefika kuomba nafasi kazi, lazima aombwe rushwa ya ngono huku wanaume wakitakiwa kinyume na maumbile: “Kila msichana anaefika hapa kuomba nafasi ya kazi, anaombwa rushwa ya ngono ndipo apatiwe kazi huku wanaume wakiingiliwa kinyume na maumbile,” walisema.

Aidha walisema sababu iliyowafanya wafikie maamuzi ya kuandamana hadi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa 

kutaka msaada ni kukithiri kwa vitendo hivyo.

Akizungumzia tuhuma hizo, Meneja wa Nakumatt Moshi, Alfrick Milimo alikanusha tuhuma hizo na kudai kwamba zote hizo ni njama za kupakana matope za watu wasiolitakia mema duka hilo.

Alisema kumekuwa na watu wanaozunguka kuwashawishi wafanyakazi huku akikumbushia matatizo yalitokea kipindi cha nyuma kati ya uongozi na wafanyakazi wake na kuwa tayari wameshabaini njama hizo.

Alisema katika duka lake kuna wafanyikazi wa Kenya na Tanzania lakini mara nyingi tatizo linatokea pale wanapowalazimisha Watanzania kufanya kazi maana wengi hawapendi kufanya kazi bila kushurutishwa:
 “Niko hapa kwa ajili ya kuwafundisha, kuwaonya na kuwaelekeza lakini inaonekana kuwa unapofanya hivyo unaonekana kuwa wewe ni mbaya na wanafika kazini na mavazi yasizoendana na maadili ya kazi pia wanasinzia kazini,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amekiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa wafanyakazi hao na kuahidi kuyashughulikia. 
Alisema tayari ameshaagiza Idara ya kazi kulifuatilia suala hilo kwa karibu na kutoa taarifa mapema ikiwa ni pamoja na idadi kamili ya Watanzania na Wakenya wanaofanya kazi katika duka hilo.

Popular posts from this blog

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2013 wilaya ya tanga mjini pekee!!!

ARAFAH ENG-MED PRIMARY SCHOOL - P2007029 AVICENNA ENG -MD PRIMARY SCHOOL - P2007051 AZIMIO PRIMARY SCHOOL - P2007032 BOMBO PRIMARY SCHOOL - P2007001 BURHANI ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007055 CHANGA ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007033 CHANGA PRIMARY SCHOOL - P2007002 CHUDA PRIMARY SCHOOL - P2007034 CHUMA PRIMARY SCHOOL - P2007003 CHUMBAGENI PRIMARY SCHOOL - P2007004 DARAJANI PRIMARY SCHOOL - P2007005 DAYSTAR ENG - MD PRIMARY SCHOOL - P2007053 DONGE PRIMARY SCHOOL - P2007035 EBEN EZER ENG- MD PR SCHOOL - P2007048 ECKERNFORDE ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007044 GOFU-JUU PRIMARY SCHOOL - P2007006 INDIAN OCEAN ENG-MED PR SCHOOL - P2007049 JABIR BIN ZAID ENG- MED PRIMARY SCHOOL - P2007052 JUHUDI PRIMARY SCHOOL - P2007036 KANA CENTRAL ENGMED PRIMARY SCHOOL - P2007054 KANA PRIMARY SCHOOL - P2007007 KISOSORA PRIMARY SCHOOL - P2007008 KOMBEZI PRIMARY SCHOOL - P2007009 KWAKAEZA PRIMARY SCHOOL - P2007026 KWANJEKA PRIMARY SCHOOL - P2007010 MABAW...

MAJINA YA WASHIRIKI NA WA WEZESHAJI WA FILM YA HOUSE GIRL!

CAST SELEMANI MOHAMED / BUNTO ANDREW / C-O YORAM MWETA / MGANGA MWANTUMU / MKE WA C-O JOHN / MCHUNGAJI BI FURURATU / JINI WAOMBOLEZAJI SAUMU HUSENI HASHIMU BABA RASTA MAN YOHANNA TAMILWAI SAIDI MWALUBADU SEMY STIR SELEMANI MOHAMEDI  AND ANDREW C-O LOCATION ATHUMANI HAMADI MAKE UP MWASHAMBA RAMADHANI BEDUI DEREVA DAUDI SPOONSER SAIDI SHABANI AND THE FRESH2012 GLOB SOUND PRODUCER J-B LIGHT YOHANNA TAMILWAI THENK YOU THE FRESH ENERTAINMENT AND THE FRESH2012 BLOG CONTACTS 0653785027 +255714091786 ZAIDI TEMBELEA www.the-fresh.blogspot.com ADRESS Thefresh@ymail.com AU Saidshabani60@gmai.com

Video: Blackchild – Put Inside

David Abdulichel, also known as BlackChild is a Ghanaian from Asanti origin, born and raised in Lagos Nigeria. BlackChild, who is a recording artist, song writer and performer started his music career back in 2000 and since then has released four singles. He has also worked with top producers in Nigeria such as Fliptyce, Spanky, Meca E & BrainMix to mention but few. BlackChild Abdul rose to prominence with his hit songs “Treasure”, “Ele” featuring Rock Steady, “Could It Be Love” featuring Cartiar, “All I Need” featuring Solid Star. This time around he comes out with “Put Inside” which sees him delivering lines in french and his native language and is steadily generating buzz and enjoying airplay on radio stations within and outside Lagos. Listen up!