Skip to main content

Mtuhumiwa SUGU akamatwa SIMIYU, akutwa na silaha 45 za vita, 17 za kienyeji na idadi kubwa ya risasi










OPERESHENI Maalumu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu kukabiliana na vitendo vya Ujambazi, Ujangiri wa uwindaji haramu pamoja na wahamiaji haramu umefanikisha kukamatwa kwa silaha 45, zikiwemo za Kivita na 17 za kienyeji na risasi 892 na magazine 24 huku watuhumiwa sugu wa ujambazi na ujangiri wakitiwa mbaroni.

Akizungumza jana na mbele ya waandishi wa Habari ofisini kwake, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Salum Msangi (pichani) alisema kuwa opresheni hiyo ilitokana na kuwepo vitendo vya uhalifu katika Wilaya tano za Mkoa huo na kwenye maeneo ya mbalimbai ya Mapori Tengefu ya Uwindaji kwa kipindi cha mwaka moja tangu kuanzishwa kwake Desemba 2012.
Kamanda Msangi alieleza kuwa miongoni mwa silaha hizo 45 na magazine 28 zilikamatwa ni pamoja na SMG 7 risasi 763 na G3 moja ikiwa na risasi zake 35 iliyokuwa ikitumiwa na mwanamke mmoja aliyekamatwa Hollo Mabuga (28) mkazi wa Wilayani Bariadi, silaha nyingine 13 zilisalimishwa kwa hihali na baadhi ya watu waliokuwa wakizimiliki kinyume na sharia,Short-Gun saba, Gobole 17 na SAR moja.
“Tumeweza pia kumkamata mtuhumiwa hatari wa matukio ya uhalifu ambaye hivi karibuni aliachiwa kutoka Gerezani lakini tukapata taarifa za raia wema kuwa amekuwa akijihusisha na ujangiri na ujambazi ambaye ni Masanja Sumuni, tukaweka mtego na kufanikiwa kumkamata akiwa na SMG moja na risasi 96 huku mke wake Hollo Mabuga akikutwa pia na silaha” alisema.
Kufatia operesheni hiyo Jeshi hilo pia limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu wane katika maeneo ya Wilaya ya meatu huku zaidi ya watu kumi waliokuwa wakijihusisha na ujangiri wakikutwa na nyara za serikali ikiwa niza wanyama waliopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Mapori ya Akiba katika Wilaya za Meatu, Maswa na Itilima.
“Tumeunda kikosi kazi ambacho pia kinaendelea na operesheni ya kuwakamata wafugaji na mifugo yao ambao wamekuwa wakichungia mifugo ndani ya eneo la Hifadhi ya Serengeti ambapo zaidi ya ng’ombe wengi walikamatwa na kutozwa faini ambapo zaidi ya shilingi milioni 180 zilipatikana huku watu wanaoendesha vitendo vya ujangiri wakiuwa tembo na wamyama na kuuza kwa wananchi wa maeneo ya jirani” alisema Kamanda.
Kamanda Msangi amewataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za siri zitakazowawezesha kuwakamata wahalifu na wahamiaji haramu katika maeneo yote ya Wilaya za Meatu, Maswa, Bariadi, Itilima na Busega huku makakati wa kuanzisha vikosi kazi kila tarafa ukiwa mbioni kukamilika ili kuimalisha ulinzi kwa wananchi na mali zao.

Popular posts from this blog

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2013 wilaya ya tanga mjini pekee!!!

ARAFAH ENG-MED PRIMARY SCHOOL - P2007029 AVICENNA ENG -MD PRIMARY SCHOOL - P2007051 AZIMIO PRIMARY SCHOOL - P2007032 BOMBO PRIMARY SCHOOL - P2007001 BURHANI ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007055 CHANGA ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007033 CHANGA PRIMARY SCHOOL - P2007002 CHUDA PRIMARY SCHOOL - P2007034 CHUMA PRIMARY SCHOOL - P2007003 CHUMBAGENI PRIMARY SCHOOL - P2007004 DARAJANI PRIMARY SCHOOL - P2007005 DAYSTAR ENG - MD PRIMARY SCHOOL - P2007053 DONGE PRIMARY SCHOOL - P2007035 EBEN EZER ENG- MD PR SCHOOL - P2007048 ECKERNFORDE ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007044 GOFU-JUU PRIMARY SCHOOL - P2007006 INDIAN OCEAN ENG-MED PR SCHOOL - P2007049 JABIR BIN ZAID ENG- MED PRIMARY SCHOOL - P2007052 JUHUDI PRIMARY SCHOOL - P2007036 KANA CENTRAL ENGMED PRIMARY SCHOOL - P2007054 KANA PRIMARY SCHOOL - P2007007 KISOSORA PRIMARY SCHOOL - P2007008 KOMBEZI PRIMARY SCHOOL - P2007009 KWAKAEZA PRIMARY SCHOOL - P2007026 KWANJEKA PRIMARY SCHOOL - P2007010 MABAW...

MAJINA YA WASHIRIKI NA WA WEZESHAJI WA FILM YA HOUSE GIRL!

CAST SELEMANI MOHAMED / BUNTO ANDREW / C-O YORAM MWETA / MGANGA MWANTUMU / MKE WA C-O JOHN / MCHUNGAJI BI FURURATU / JINI WAOMBOLEZAJI SAUMU HUSENI HASHIMU BABA RASTA MAN YOHANNA TAMILWAI SAIDI MWALUBADU SEMY STIR SELEMANI MOHAMEDI  AND ANDREW C-O LOCATION ATHUMANI HAMADI MAKE UP MWASHAMBA RAMADHANI BEDUI DEREVA DAUDI SPOONSER SAIDI SHABANI AND THE FRESH2012 GLOB SOUND PRODUCER J-B LIGHT YOHANNA TAMILWAI THENK YOU THE FRESH ENERTAINMENT AND THE FRESH2012 BLOG CONTACTS 0653785027 +255714091786 ZAIDI TEMBELEA www.the-fresh.blogspot.com ADRESS Thefresh@ymail.com AU Saidshabani60@gmai.com

Video: Blackchild – Put Inside

David Abdulichel, also known as BlackChild is a Ghanaian from Asanti origin, born and raised in Lagos Nigeria. BlackChild, who is a recording artist, song writer and performer started his music career back in 2000 and since then has released four singles. He has also worked with top producers in Nigeria such as Fliptyce, Spanky, Meca E & BrainMix to mention but few. BlackChild Abdul rose to prominence with his hit songs “Treasure”, “Ele” featuring Rock Steady, “Could It Be Love” featuring Cartiar, “All I Need” featuring Solid Star. This time around he comes out with “Put Inside” which sees him delivering lines in french and his native language and is steadily generating buzz and enjoying airplay on radio stations within and outside Lagos. Listen up!