Skip to main content

Posts

WEMA AONYESHA NYUMBA YAKE ILIVYO HADI NDANI.

WEMA AONYESHA NYUMBA YAKE ILIVYO HADI NDANI. Wema akiwa na Zamaradi kutoka Clouds TV  Wema akiwa na James mtu ambaye ametengeneza style yote ya nyuma ya Wema.   Gari yake ya kwanza ilikuwa hii Gari ya pili ya wema Wema Sepetu anaishi  maeneo ya Kijitonyama\ picha kwa hisani ya dj choka blog

BIFU LA 50 CENT NA OPRA WINFREY LAFIKIA HAPA!!

Baada ya kuwa na bifu lililodumu toka mwaka 2006 hadi kufikia mwaka huu wa 2012 mastaa wawili kutoka pande za Obama wamekaa chini na kuamua kulifutilia mbali bifu hilo na kuganga ya mbele. Bifu hilo lililoanza mwaka 2006 baada ya 50 cent kumtukana Opra kwa kile alichodai kuwa Mwanamama huyo ni mbaguzi kwani kwenye show yake inayorushwa na kituo chake cha Luninga cha OWN amekuwa akiwabagua wasanii weusi wa HipHop na kuwapendelea vibibi vizee vya kizunguu ambapo kutokana na upendeleo huo 50 Cent aliamua kumwita mbwa wake jina la Oprah kutokana na kumchukia mwanamama huyo, Lakini jana kupitia new Episode ya kipindi cha Oprah show wawili hao waliweza kukaa na kumaliza tofauti zao hizo.

ALICHOKISEMA DIAMOND JUU YA KUHUSISHWA NA FREEMASON!!

Ili kumaliza utata wa je, Diamond ni Freemason au la, Ijumaa Wikienda lilibeba jukumu la kumtafuta ili aanike ukweli wake ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Unajua mwanzoni nilikuwa sikumbuki ni lini na wapi nilipiga picha ya dizaini hiyo. ‘Anyway’, isiwe kesi, nakumbuka ilikuwa Uingereza kipindi kile nilikuwa na shoo nchini humo. “Nakumbuka walinifuata watasha wengi tofauti lakini huyo mmoja alining’ang’ania sana nipige naye picha. “Kwa kweli alinilazimisha sana kwa sababu mwanzo nilikataa lakini baadaye nikaona isiwe ishu nikampa ushirikiano alioutaka. “Mimi sikuona matatizo alivyotaka tusalimiane kwa kugusisha vidole kwa sababu nilikuwa sijui chochote kuhusu Freemason. Nimeijua baada ya mambo haya kuyasikia kwa sana hivi karibuni. “Kwa hiyo inawezekana siku hiyo waliniunganisha bila mimi kujua (kicheko).” Habari kutoka Ijumaa Wikenda.

TISA WATEMWA COASTAL UNION

1.Ben Mwalala 2.Ally Ahmed (Shiboli) 3.Samweli Temi 4.Ramadhani Wasso 5.Enock John 6.Laurence Mugia 7.Bakari Mohamed 8.Daudi Chengula na 9.Francis Busungu 'Uongozi umeamua kuchana na wachezaji hao kutokana na viwango vyao kushuka' Alisema Katibu mkuu Coastal Union Kassim El Siagi.

COASTAL UNION YAPATA KOCHA MPYA!

"Habari Njema kwa Wapenzi watimu ya Coastal Union Hatimaye Tumepata Coach mpya kutoka bandari ya Mombasa-Kenya anaitwa Sheduu"NASSOR BINSLUM

MKALI MAN, SASHA NAUJIO MPYA SOON!

MAN SASHA akiwa studio za URUMA REC, akimalizia mzigo wake mpya mashabiki wake kaeni mkao wakula!!!!!

KOCHA AFARIKI SAA 24 BAADA YA MKATABA

Kocha mpya aliyeteuliwa juzi Manuel Preciado amefariki saa 24 baada ya kutangazwa kama Kocha wa klabu ya Uhispania, Villarreal. Kocha huyo ambaye hapo zamani alikua kocha wa Sporting Gijon alifariki kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 54. Kifo chake kimetokea saa 24 baada ya kukubali mkataba wa kuiongoza klabu ya Villareal iliyoshuka daraja, ambapo mkataba wake ulikua wa kuanza msimu wa mwaka 2012 hadi 2013. Preciado alifutwa kazi na Sporting Gijon mnamo mwezi Januari licha ya kuiwezesha klabu hio kupanda daraja mara mbili kuingia Ligi kuu ya Uhispania, La Liga. Mnamo mwezi Aprili mwaka 2011, klabu yake ya Sporting Gijon iliikwamisha klabu maarufu ya Real Madrid kwa kuvunja rekodi yake ya miaka tisa bila kupoteza kwenye uwanja wa nyumbani safari hii ikiwa chini ya Jose Mourinho. Wakati wake wa uchezaji soka Preciado alicheza kama beki aliyeanzia uchezaji wake katika klabu ya Racing Santander na pia kushiriki mechi za vilabu kama Linares, Mallorca, Alaves, Ourens...