Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2013

HAPPY BIRTHDAY SAIDI NURU a.k.a Manywele Classic

Ongera kaka kwakutimiza miaka yako kazaa  M/mungu akupe maisha marefu na mafanikio katika miangaiko yako ya kilasiku kaka Endelea kutembelea blog hii uwe mjanja Mwaka huu mpya wa 2014 !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

BLOG HII INAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2014

Serikali ya Tanganyika yaibuliwa katika Rasimu ya pili

Jambo jingine jipya ni kupunguzwa kwa madaraka ya uteuzi ya Rais kwa kuweka vyombo vya kupendekeza majina ya watu wa kuteuliwa na baadhi ya vyeo kuhitaji kuthibitishwa na Bunge.PICHA|MAKTABA  Dar es Salaam. Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetoa Rasimu ya Pili ya Katiba ikiwa na mambo sita mpya, huku ikiendelea kupendekeza Muungano wa Serikali tatu na kurejea kwa nchi ya Tanganyika. Rasimu hiyo ya Pili ambayo imetolewa miezi saba baada ya Rasimu ya Kwanza, ilikabidhiwa jana kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam. Akizungumza kabla ya kukabidhi rasimu hiyo, Jaji Warioba alisema ina Ibara 271, tofauti na ile ya kwanza iliyokuwa na Ibara 240. Alisema ripoti ya rasimu hiyo pia ina maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya Katiba, sera, sheria na utekelezaji maoni ya Mabaraza ya Katiba, takwimu za ukusanyaji wa maoni ya w

HUYU NDIO ALIYE CHAGULIWA NA RAISI KUWA MKUU WA JESHI LA POLISI BAADA YA IGP MWEMA KUSTAAFU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema. Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence) katika Jeshi hilo la Polisi. Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi. Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations). Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne,  Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam

MATUKIO YA PICHA LEO WAKATI WA MAZISHI YA KOCHA WA MAKIPA SIMBA JAMES KISAKA

NDUGU WA MAREHEMU JAMES KISAKA WAKILIA KWA UCHUNGU LEO WAKATI MWILI WA NDUGU YAO UKISHUSHWA NYUMBANI KWAO LUSANGA LEO TAYARI KWA MAZIKO AMBAYO YALIFANYIKA KATIKA MAKABURI YA FAMILI KIJIJI HUMO. MMOJA WA NDUGU WA JAMES KISAKA AKILIA KWA UCHUNGU WAKATI MWILI WA NDUGU YAO ULIPOWASILI LEO MDOGO WAKE JAMES KISAKA,BENNY KISAKA AKIUAGA MWILI WA MAREHEMU KAKA YAKE,KABLA YA KUPUMZISHWA KATIKA MAKABURI YA FAMILI WILAYANI MUHEZA MKOANI TANGA LEO

Sikiliza na download ngoma mpya ya H Mbizo ft Joslin _Kosa langu

SIKILIZA NA DOWNLOOAD NGOMA MPYA YA MAN SASHA FT BAGUJE...BORA NISEME

PICHA ZA VIONGOZI WALIOUZURIA KATIKA BONANZA LA FULSA YA VIJANA MKOANI TANGA

Askari wa Marekani wajeruhiwa Bor!

Facebook Twitter Google+ Tuma kwa rafiki yako Chapisha Jeshi la Marekani linasema kuwa wanajeshi wake wane wamejeruhiwa Sudan Kusini pale ndege yao ilipopigwa risasi karibu na mji wa Bor, wakijaribu kuwahamisha raia wao. Ndege kadha zililazimika kurudi Uganda. Siku hiyo pia Marekani ilipeleka wanajeshi 45 kuwalinda raia na mali ya Marekani Sudan Kusini.Jeshi la serikali ya Sudan Kusini linajaribu kuukomboa mji wa Bor, kaskazini ya mji mkuu, Juba, kutoka wanajeshi walioasi na kujiunga na makamo wa rais wa zamani, Riek Machar ambaye aliuteka mji huo Jumatano. Kwa mujibu wa gazeti la taifa la Uganda, New Vision,ndege mbili za jeshi la Uganda pia yalinasa katika tukio hilo. Pamekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari kutoka Sudan Kusini kwamba ndege za Uganda piya zimekuwa zikiisaidia serikali kuukomboa mji wa Bor kutoka kwa wanajeshi walioasi - taarifa ambazo zinakanushwa na nchi zote mbili.

SIMBA FC YAITANIA YANGA YAWAPIGA 3-1 NA OKWI WAO

Nahodha wa Simba SC, Haruna Shamte akiwa ameinua Kombe baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe mwenye suti nyeusi kulia baada ya kuifunga Yanga SC mabao 3-1    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam SIMBA SC ndiye Mtani Jembe 2013. Hiyo inafuatia Wekundu hao wa Msimbazi kuwafunga watani wao wa jadi, Yanga mabao 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mabao ya Simba yamefungwa na Amisi Tambwe mawili na Awadh Juma moja, wakati la Yanga lilifungwa na Emmanuel Okwi.  Katika mchezo huo, Yanga ilimaliza pungufu baada ya beki wake, Kevin Yondan kutolewa nje kwa kadi ya pili ya njano, baada ya kumchezea rafu Ramadhani Singano ‘Messi’.  Mfungaji wa mabao mawili ya Simba SC leo, Amisi Tambwe akipongezwa na Issa Rashid 'Baba Ubaya' Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0 ambayo yote yalifugwa na Amisi Tambwe dakika ya 14 na 44. Tambwe alifunga bao la kwanza baada ya kupokea pasi ya kiufundi ya Said Hamisi Ndemla na kumt

MASHINDANO YA VYUO VIKUU YAENDELEA MKOANI TANGA.

Picha by Tanga raha blog!!!!!!!!!!!!!!

Waasi waua watu 1000 Afrika ya Kati

Askari wa Ufaransa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Wanamgambo wa kundi la anti-balaka, Jamhuri ya Afrika ya Kati Takriban watu elfu moja wameuawa na waasi wa zamani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mapambano yaliyodumu kwa siku mbili yaliyojitokeza mwezi huu, makadirio haya yanazidi yale ya Umoja wa Mataifa. Shirika la Amnesty International limesema. Shirika hilo limesema kuwa uhalifu wa kivita bado unaendelea kufanyika nchini humo. Taarifa zinazohusiana Mauaji ,  Afrika Wapiganaji hao ambao wengi wao ni Waislamu walimuondoa madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo, Francois Bozize mwezi March, hali iliyosababisha mgogoro ndani ya jamii nchini humo. Kiongozi wa waasi Michel Djotodia hivi sasa ni kiongozi wa kwanza kutoka jamii ya Waislamu anayeongoza taifa lenye Wakristo wengi na ndiye kiongozi wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya kati. Katika ripoti hiyo, Amnesty International imesema waasi wa zamani wa Seleka waliwaua takriban watu 1000 mjini Ban

Macho yote Qunu: Buriani Tata Madiba

Qunu.  Huzuni na simanzi viliyateka maeneo ya Mthatha na Qunu katika Jimbo la Eastern Cape, Afrika Kusini baada ya kuwasili kwa mwili wa rais wa kwanza mzalendo wa nchi, Nelson Mandela. Mwili wa Mandela uliwasili jana katika Uwanja wa Ndege wa Mthatha saa 7:40 mchana (kwa saa za huku) dakika 20 kabla ya muda uliotarajiwa, ukiwa umesafirishwa kutoka Uwanja wa Ndege wa Jeshi wa Waterkloof, Pretoria. Ulisindikizwa na maofisa waandamizi wa Jeshi la Afrika Kusini (SANDF), maofisa kutoka Serikali, wawakilishi wa familia yake na viongozi wa mila kutoka kabila la abaThembu. Mandela anazikwa leo katika makaburi ya familia yaliyopo katika Kijiji cha Qunu ambako alikulia, katika mazishi ambayo yatakuwa mchanganyiko wa mila na desturi, dini yake ya Kikristo ikifuata taratibu za kimethodisti na kijeshi kwa maana ya Serikali,  Alizaliwa katika Kijiji cha Mvezo, Julai 18, 1918 na alifariki dunia Desemba 5, mwaka huu nyumbani kwake, Houghton, Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 ba

Msanii Dr Leader afiwa na mke,

Pole sana Dr Leader Kwa msiba mzito wa kuondokewa na mke, mzazi mwenzio na mpendwa  wako. mungu akupe roho ya uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. kila nafsi itaonja mauti.  mwenyezi mungu aiweke roho ya marahemu mahali pema peponi, You,  Selle Wamichanno  and  16 others  like this. Ally Mohamed   R.I.P SHEM.WE SASHA ALIKUWA AUMWA KWN AU? 9 hours ago  via  mobile  ·  Like Young Dutch Mahesabu   dah r.i.p shemeji yetu mpendwa ... natanguliza pole hiz kwa ndugu yetu dr.leader msambaa mungu akupe roho ya uvimilivu kwakipndi chote hki cha mpito 9 hours ago  via  mobile  ·  Like Baba Dailysuperstar   R.!.P 8 hours ago  via  mobile  ·  Like Rajab Kidagaa   R.I.P Xhem 8 hours ago  via  mobile  ·  Like Nick Regy   mung amlaze pem pepn 2ngulia n xx 2taft mpndw rip!!!!!!!! 8 hours ago  via  mobile  ·  Like Lilla Mntambo Ramsey   R.I.P SHEM WETU mbwana ametoa na bwana ametwaaa