Skip to main content

Posts

Showing posts from September, 2012

Watakao uongozi wa ANC wajitaje

Chama tawala cha Afrika Kusini, ANC, kimefungua daftari la watu wanaotaka kuania uongozi wa chama, ambao utaaniwa tena mwezi Disemba. Taarifa zinazohusiana Afrika Kusini , Siasa Rais Jacob Zuma anatarajiwa kupingwa na naibu wake, Kgalema Motlanthe kuania urais. Wanachama milioni 1.2 wa ANC watachagua nani wa kumuunga mkono. Katika miaka ya karibuni watu wa kabila la Zulu, kabila la Rais Zuma, wameingia kwa wingi zaidi kwenye chama; lakini wadadisi wanasema rais Zuma atapata shida kushikilia wadhifa wake. Uchumi wa Afrika Kusini umezorota, na mauaji ya wachimba migodi yaliyofanywa na polisi yamepunguza hadhi ya Rais

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA UDAKU NA MICHEZO

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

PICHA MKALI WA HIPHOP TANGA DULA WAMICHANO AKIFANYIWA INTERVIEW!

-nikiwa nafanya mahojiano na mwandish flan flan hapa town Imetoka kwenye page yake ya facebook!

TOP 12 WA EPIQ BONGO STAR SEARCH HAWA HAPA

HAWA NDO WASHIRIKI WALIOBAKI KWENYE JUMBA LA BONGO STAR SEARCH

COASTAL UNION WAGOSI WAKAYA SASA NAFASI YA PILI KATIKA MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM BARA!

Coastal Union 2012 Tunatisha......Ndio Inavyosomeka.Mmoja wa Shabiki wa Coastal Union Akitoa ujumbe wake Kwa njia ya Bango. Mechi 4 points 8=Nafasi ya 2 Ni Balaaaaaaaaaaaaaa!!! Na sasa tunakamata nafasi ya pili.........,Hii ndio raha ya ushindi......!!!!!!        Imetoka kwenye page yao ya facebook,

Serikali ikiheshimu bajeti, bei za bidhaa zitashuka

Mtaalamu wa masuala ya Uchumi,Profesa Ibrahim lipumba UKIPITA madukani, sokoni utawaona watu wakiomba wapunguziwe bei ya bidhaa na nyingine zimekuwa zikikaa muda mrefu licha kupungua kwa mfumuko wa bei. Achilia mbali sokoni na dukani, lakini pia katika ‘supermarket’ ukisimama kwa mbali utaona wateja wakiingia na kutoka bila kununua bidhaa yeyote kutokana na kushindwa kumudu bei ya bidhaa. Pia ukipita katika mitaa mbalimbali ya watu, utakuta watu wakilalamikia ukosefu wa ajira na ugumu wa maisha. Wakati wakazi wakilalamikia ugumu wa maisha unavyowaumiza, baadhi yao wamekuwa wakipunguza idadi ya milo kwa siku. Kwa kawaida ratiba ya milo ni mara tatu kwa siku: asubuhi, mchana, na jioni, lakini kutokana na ugumu wa maisha baadhi wamekuwa wakila mlo mmoja kwa siku. Wakati wananchi wakilalamika kuhusu ugumu wa maisha, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), imetoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei na kubainisha kwamba umepungua kutoka asilima 15.7 Julai hadi kufikia asilimia 14.9, Agos

WANAWAKE WA BONGO MOVIE WANAPENDA KUMEGWA NA WANAUME WANAOUZA MADAWA YA KULEVYA WAKIDHANI WATATAJIRIKA ” – SHILOLE…!!

WAKATI wasanii wengi wakishindana kwa kubadilisha magari ya kifahari hapa mjini, msanii wa filamu na muziki Shilole , amefunguka na kudai kuwa kuna kasoro kubwa hasa ya kiumaskini kwani wanawake wengi wa bongo movie wanapenda kumegwa na wanaume wanaofanya biashara haramu ya madawa ya kulevya kwa kudhani kuwa watapewa dili la kulala maskini na kuamka tajiri. Wapo wasanii wengi ambao wanajisifu kwa kuwa na magari ya kifahari lakini ukitazama kwa hali ya kawaida gari analiotembelea na thamani ya hela anayolipwa katika kila filamu wala haviendani. Shilole alidai kuwa kasoro hiyo inasababishwa na tamaa za baadhi ya wasanii kwani wanaamini wakitembea na wanaume wanaofanya biashara hizo nao wanaweza kufanikiwa mapema huku wakisahau kuwa riziki hutoa Mungu na si binadamu yeyote yule. Msanii huyo alidai kuwa wapo baadhi ya wasanii ambao wamefanikiwa si kwa kuwatengemea wanaume, lakini asilimia kubwa wanakaa na kujipendezesha wakisubiri mwanaume ndiye wawafanyie kila k

JE FIESTA YA DAR ITAMLETA NANI KATI YA RICK ROSS, DRAKE, T.I NA SNOOP DOGGY?.......UNGANA NASI

Rick Ross Drake T.I Snoop Rick Ross, Drake, T.I na Snoop ndio majina yaliyotajwa leo hii kama fumbo la msanii mkubwa wa kimataifa atakaekuja Tanzania kwa ajili ya Fiesta 2012 ya Dar es salaam inayotegemewa kuchukua nafasi yake siku chache zijazo. Hayo yamesikika kupitia campaign inayoendelea muda huu kuanzia asubuhi ya leo kupitia Clouds fm, inayohamasisha watu washiriki kubashiri ni msanii gani kati ya hawa atakae kuja kuperform katika Fiesta ya Dar. Jibu la swali hili litatolewa kupitia XXL ya leo Sept 27, 2012 mishale ya saa tisa za alasiri. Fuatilia Clouds fm ili kama umeshiriki uweze kujua kama utakua umetoa jibu sahihi basi utakua kati ya washindi watakaojishindia tiketi ya kwenda kushuhudia show hiyo.

DULLY SYKES AJIPANGA KUJA NA KAMPUNI YAKE YA VIDEO PRODUCTION

Mr Misifa Dully Sykes amesema kuwa anampango wa kufungua kampuni yake mwenyewe ya kutengeneza Video baada ya kumiliki audio studio ya Dhahabu records kwa miaka kadhaa sasa. Dully kupitia website yake ameandika:  "Mashabiki wangu nawapa nafasi ya pekee ya kuchagua jina la kampuni yangu mpya ya Video Production inayotarajiwa kuanza kazi hivi karibuni. Tupia jina kwenye comments."   Hapo kabla Tumeshuhudia wasanii wengi wa hapa bongo wakifungua music production studios zao wenyewe na kufanya idadi ya audio studios zinazo exist izidi kwenda juu.  Mpaka sasa wasanii wanaomiliki studio zao wenyewe za audio ni pamoja na Dully Sykes, Juma nature, Said Fella, Mike Tee, Benja wa Mambo Jambo na wengine. Sasa naona kete inahamia kwenye video production, msanii ambae ameshaanza kufanya kazi kama producer kupitia kampuni yake mwenyewe ya kutengeneza videos ni Benjamin wa Mambo Jambo.