Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2012

XLBONGO NIGHT SHOW!

Bila ya kusahau yale mashindano ya kudansi ktk Mji wa maraha Tanga Raha yanendelea tena siku ya J,2 hii ktk Club karee tulivu na ya ukweli Le Grande Lacasa Chika, Kamasutra Dancers watasindikiza usiku huo kwa zile show zao kareeeeeeeeeeeee.....hii si ya kukosa kwa mpenda burudani Tanga,ukiiona hii mmegee na mwenzako usim'bani Rahaaaaaaaa....za kijanjaaa..Weweeeeeeeeeee

TANESCO YATANGAZA NEEMA KWA WATEJA WAO

SHIRIKA la Umeme Tanzania(Tanesco), limesema ifikapo kesho litakuwa limeshawaunganishia umeme wateja wake wote walioomba kupata huduma hiyo kwa muda mrefu. Hayo yalisemewa jana na meneja uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud (pichani) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Alisema kwa sasa shirika hilo lina vifaa vya kutosha na kwamba ndicho kitu ambacho kilikuwa kikiwakwamisha kutekeleza majukumu yao. “Mteja wetu yeyote ambaye ameomba anapaswa kuwa ameunganishiwa umeme ifikapo Juni 30, mwaka huu,”alisema Badra. Alisema wateja ambao walikuwa wameomba wafike katika ofisi za Tanesco katika maeneo yote zilizopo ofisi zao ili waweze kupatiwa huduma hiyo. “Tutatoa namba maalum ili wateja ambao watakuwa wanasumbuliwa na wafanyakazi wetu waweze kutupigia moja kwa moja na sisi tutashughulika nao,”alisema. Alisema hakuna mfanyakazi wa Tanesco anayepaswa kumzungusha mteja wa shirika hilo hivyo mteja yeyote atakayezungushwa awasilia

PICHA ..Hatimaye Dr. Ulimboka apelekwa Afrika ya Kusini kutibiwa mapema leo.

 Gari la wangonjwa la AAR ambalo lilimbeba Dk. Ulimboka likiwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere. Baadhi ya wanaharakati na wauguzi wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kulaani kitendo cha kikatili alichofanyiwa daktari huyo. Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka leo mchana alifikishwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya madaktari kubaini kuwa ana mtatizo ya kitabibu yanayomkabili likiwemo la mtikisiko wa ubongo. Mwenyekiti huyo alifikishwa uwanjani hapo majira ya saa 8.30 na ndege aliyosafiri nayo iliondoka saa 10.15. Uwanjani hapo kulikuwa na wanaharakati ambao walikuwa na mabango, kinyume cha matarajio ya wengi walizani kuwa angeteremshwa na kuingizwa na machela Uwanjani hapo lakini gari lililombeba lilipita moja kwa moja hadi ndani ya uwanja huo.  CHANZO -GLOBALPUBLISHERS

DAWA MPYA KWA WAGONJWA WA UKIMWI YATOLEWA!!

Huenda wagonjwa wa Ukimwi wakanufaika na dawa mpya ambayo itawawezesha kutumia tembe moja kwa siku. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya nchini Marekani.Jarida la Afya Lancet limesema tembe hiyo inajumlisha dawa zote nne zinazokabiliana na makali ya ukimwi na kwamba ni salama.Utafiti unasema hii itawarahisishia wagonjwa katika kuhakikisha wanafuata maagizo ya madaktari wao. Ukimwi hauna tiba lakini watafiti wameweza kutoa dawa za kukabiliana na maradhi nyemela. Watafiti pamoja na kampuni za dawa wamechanganya dawa nne na kutengeneza tembe moja ili kurahisisha utumizi wa dawa hiyo miongoni mwa wagonjwa. Tembe inayofanyiwa majaribio na ambayo imechanganywa dawa nne inauwezo wa kudhibiti virusi vya HIV kuongezeka mwilini. Paul Sax mtafiti mkuum katika Hospitali ya Wanawake ya Brigham huko Boston,Massachussetts ambaye pia ni mwanazuo wa ziada wa taasisi ya afya ya Harvard ameelezea umuhimu wa tembe hii kwa kuimarisha afya ya wagonjwa. Dk. Sax ameongoza utafiti huu ambapo pi

COASTAL UNION

Timu ya Coastal Union ya vijana chini ya miaka 20,Leo itacheza mchezo wa Kirafiki na Timu ya vijana ya Hapa hapa mkoani Tanga(MKWAKWANI)kwaajili kujiandaa na mechi za kimataifa za Rolling Stone zitakazofanyika nchini Burundi kuanzia tarehe. 10/07/2012. Chini ya Kocha Juma Mgunda

ULIMBOKA ANA SIRI NZITO, ASEMA ATAANIKA KILA KITU BAADAYE, ASEMA ACHWE APUMZIKE, MKUU WA JOPO LA MADAKTARI WANAOMTIBU ASEMA ALING'OLEWA KUCHA, MENO MAWILI NA KUPATA MTIKISIKO WA UBONGO

[Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk Steven Ulimboka, akiwa amelazwa katika Chumba maalum cha wagonjwa mahututi (ICU)akiendelea na matibabu katika Taasisi ya mifupa (MOI)jijini Dar es Salaam jana.] Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk Steven Ulimboka, akiwa amelazwa katika Chumba maalum cha wagonjwa mahututi (ICU)akiendelea na matibabu katika Taasisi ya mifupa (MOI)jijini Dar es Salaam jana. ASEMA ATAANIKA KILA KITU BAADAYE, ASEMA ACHWE APUMZIKE, MKUU WA JOPO LA MADAKTARI WANAOMTIBU ASEMA ALING'OLEWA KUCHA, MENO MAWILI NA KUPATA MTIKISIKO WA UBONGO Geofrey Nyang'oro MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari aliyetekwa nyara na kuumizwa vibaya usiku wa kumkia juzi, kisha kutupwa Msitu wa Pande, Dk Steven Ulimboka amesema atazungumza kwa kina yote yaliyomsibu baadaye na kuomba sasa aachwe auguze maumivu makali yanayomkabili. Dk Ulimboka aliokotwa na wasamaria wema juzi asubuhi katika Msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, baada ya kutekwa nyara na watu waliokuwa na

IMETOKA KWENYE PAGE YA COASTAL UNION FACEBOOK,

Jembe jipya la upande wa kushoto katika ulinzi, Athuman Omari maarufu kama Mani ambaye pia ni mlinzi wa timu ya taifa ya Zanzibar akikaribishwa Coastal Union na Makamu mwenyekiti, Steven Mnguto........karibu jembe...piga kazi

RAY AZINDUA MOVIE MPYA - SOBING SOUND ONA UJIO WAKE!

MSANII wa filamu nchini Visent Kigos 'Ray' amezindua filam yake mpya inayojulikana kama 'SOBING SOUND'. Filam hiyo ameizindua kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua Ukumbini kama ilivyozoeleka na wengi, msanii huyo amezindua filam hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 1.5 kwa niaba ya Kempuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam Akizungumza mara baada ya kuzindua filamu hiyo akiwa pamoja na watoto yatima wa kituo hicho, Ray alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba watu wengi wamekuwa wakifurahia maisha uku wengine wakiendelea kutahabika kitendo ambacho si kizuri. Alisema ujio wa filamu hiyo ni kama azma yake aliyoipanga tangu awali kuhakikisha filamu zake zote zinafanya vizuri na atakuwa kila filamu anayotoa atakikisha japo kidogo kwa namna yoyote anawakumbuka watoto yatima kwana awajapenda. Alisema msaada uliotolewa kwa watoto yati

SERIKALI YASITISHA KUTOA TAMKO JUU YA MADAKTARI LEO

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza kusitisha Serikali kutoa tamko lake kuhusu mgomo wa madaktari, ambao ulitakiwa kutolewa leo kama alivyoahidi jana Bungeni. Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Waziri Mkuu, Pinda, alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua Serikali ina mipango gani ya dharula ya kuumaliza mgomo huo. Alisema kwa hivi sasa, Serikali imechukua dharura, kwa kuwaita madaktari wastaafu kwenda kwenye baadhi ya Hospitali za Serikali kushika nafasi maeneo ambayo madaktari waliogoma. Vilevile Serikali imewataka wananchi waende kuhudumiwa kwenye hospitali za Jeshi, ikiwemo Lugalo. Kuhusu Dkt Stephen Ulimboka, Mhe. Pinda ameseama kuwa hata yeye alipopokea taarifa kuwa Dkt. Ulimboka ametekwa na kupigwa na kwamba alisikitika sana, na anamuombea apone haraka ili waendelee na suluhisho la mgomo huo wa madakatari. Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya ndani kuunda jopo la

BREAKING NEWS: MADAKTARI 72 WASIMAMISHWA KAZI KWA MGOMO

Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara Aikzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kusimamishwa kazi kwa madaktari hao. Mkurugenzi wa wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr E. Sankey akimsikiliza kwa makini kaimu mkuu wa mkoa Mbeya.*********** BODI ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari 72 kwa kosa la kutoingia kazini...

MKALI ROMA MKATOLIKI ZAHABU YETU TANGA

PICHA ZA KIONGOZI WA JUMUIYA MADAKTARI TANZANIA ,DKT. STEVEN ULIMBOKA STEVEN BAADA YA KUOKOTWA MAENENO YA MABWEPANDE

Juu ni taswira mbalimbali za Dr. Steven Ulimboka baada ya kuokotwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwakaribisha ikulu jijini Dar es salaam viongozi wa Chama cha madaktari nchini. Wa pili kushoto ni Mratibu wa mgomo wa madaktari, Stephen Ulimboka na Kulia ni Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi Dr. Steven Ulimboka  alipokua akieleza jambo kwenye mkutano wao(madaktari na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Hivi Karibuni Picha na habari kwa hisani ya  http://www.patahabari.blogspot.com   soma habarihii kwa undani zaidi hapa  http://www.patahabari.blogspot.com/2012/06/picha-za-kiongozi-wa-jumuiya-ya.html  

JUMUIYA YA KIISLAMU KUPINGA SENSA MAHAKAMANI

Jumuiya na Taasisi za Kiislamu imepanga kwenda mahakamani kuzuia zoezi la sensa na kupinga kauli iliyotolewa na Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislamu (Bakwata), Mufti Issa Shaban Simba, kwamba Waislamu wamekubali kuhesabiwa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa jumuiya hizo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema kauli ya Mufti Simba, inaashiria kwamba Bakwata limekiuka makubaliano yaliyofikiwa mjini Dodoma na jumuiya zote za waumini wa dini hiyo. Alisema kauli hiyo haitakuwa na athari kubwa kwa msimamo wa Waislamu wemgi ambao hawatashiriki zoezi la sensa. "Waislamu tumepanga tarehe hiyo ya sensa kufanya maandamano ya amani nchi nzima kwani sensa inayokusudiwa haitakuwa na matokeo sahihi kwakuwa asilimia 80 ya Waislamu ambao ni zaidi ya nusu ya Watanzania hawatahesabiwa," alisema Shekh Ponda. Hivi karibuni Mufti Simba, alitoa msimamo wa Bakwata, akiwataka Waislamu wote nchini kushiriki Sensa ya Watu na Makazi

COASTAL UNION!

Pius Kisambale akimwaga wino wa kuichezea Coastal Union kwa mkataba wa miaka miwili mbele ya makamu mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto...bado wachezaji wawili wa kigeno tufunge usajili huu.... Pius Kisambale akikaribishwa Coastal Union na Makamu Mwenyekiti wa Coasta Union, Steven Mguto.....welcome home new boy....

KIONGOZI WA MGOMO WA MADAKTARI APIGWA VIBAYA ONA PICHA

Dkt. Ulimboka:Dkt. Helen Kijo-Bisimba wa LHRC akinukuliwa katika EA Redio amekariri maelezo ya Dkt. Ulimboka ambayo pia yamesikika yakitamkwa na mwenyewe (Dkt. Ulimboka Steven), kupitia kituo cha redio cha CloudsFM, kwamba walikuja watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Watu hao walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na namba na kuanza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa usoni, kamba mikononi na miguuni kisha wakampiga huku wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu na kama wangekuwa na sindano ya sumu wangemmaliza kabisa. --- UPDATE: Dkt. Ulimboka amefikishwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma. Hali yake ni mbaya ila "stable". ------ Baadhi ya watu wa shirika la Tanzania Legal Human Rights Center (LHRC) walifanya juhudi za kumtafuta kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Ulimboka Steven aliyekamatawa (? tekwa) jana usiku. Taarifa iliyotoka kwa mmoja wa wanaharakati ha

Happy Birthday Rama

Happy bday bro allah akuzidishie umri zaidi ya huu uliokua nao!

BREEZ FM RADIO

 Kuanzia Tareh 02.07.2012.. Cheza na Breez ya Breez Fm {Tanga} inakuja kivingine.. So stay tune kwa wale washabiki wa BREEZ FM.!! Host wa show atakuwa Ameir Salim a.k.a Raydo.! Kuanzia time ya saa 4 asubuhi hadi 7 mchana.!! Usikose kuskiliza 100.6

MAAJABU: WANAIJERIA HUUZA FIGO KWA SH MILION 51($30,000)

Baadhi ya wanaijeria waishio nje ya nchi wamejikuta wakiwa na maisha magumu kiasi cha kuamua kuuza figo zao ili waweze kuishi. Biashara hiyo iliyoshamiri kwenye mtandao imewafanya baadhi yao kutafuta soko la viungo hivyo muhimu kwenye mwili wa binadamu na wengine wakisafiri hadi Malaysia na India kuuza figo zao zote mbili kwa $30,000. Kwa mujibu wa mtandao wa nigeriafilms.com, watafiti wake wamebaini kuwa kuna mtandao mkubwa sana wa wafanyabiashara, mawakala, wauzaji wa watafutaji wa bidhaa hiyo ambao hutafuta watu watakaouza figo zao. Wengine hufikia hatua za kuteka watu na kuwanyofoa figo zao ili kujipatia maisha mazuri na ya haraka. Kuna taarifa kuwa watu wengine hupoteza maisha wakati wa oparesheni ya kunyofoa figo hizo. Mpaka sasa karibu wanaijeria 1000 wana matumaini ya kupata connection hizo ili nao waweze kuuza figo zao na kujipatia maisha wanayoyataka. Mtandao huo umemaliza kwa kusema, “Hivi ndivyo umaskini unaosababishwa na uongozi mbovu umeifikisha Nigeria.”

KAZI YAKE KUTAFUTA VYANZO VIPYA VYA MAPATO, KUONGEZA BAJETI YA MAENDELEO

 Neville Meena na Mussa Juma, Dodoma  WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameunda Kamati Maalum ya mawaziri sita kusaidia mchakato wa marekebisho ya Bajeti ya Serikali ambayo mjadala wake utahitimishwa kesho.Kuundwa kwa kamati hiyo kunazifanya kamati zinazoifanyia kazi Bajeti ya 2012/2013 kufikia tatu. Ijumaa iliyopita wabunge wa CCM waliunda kamati ndogo kwa ajili ya kusaidi pamoja na mambo mengine kuangalia vyanzo vingine vya mapato na kuona iwapo bajeti ya maendeleo inaweza kuongezwa, kukidhi kiu ya wabunge. Kamati nyingine ni ile ya Fedha na Uchumi ya Bunge ambayo tayari imetoa maoni yake bungeni kuhusu Bajeti, lakini ikabainisha kuwapo kwa kasoro kadhaa ambazo zinapaswa kurekebishwa. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alikiri kuundwa kwa kamati hiyo, lakini akakataa kutoa taarifa za kina kuhusu suala hilo kwa maelezo kwamba huo ni utendaji wa kawaida wa shughuli za Serikali. “Sidhani kama hiyo ni habari kubwa ya kwenda kwenye pu

MTU ALIYEMWIBIA GARI KHADIJA KOPA AKAMATWA,!!

May  ya mwaka huu kulisikika habari za kuibiwa kwa gari la mwimbaji wa Taarabu Malkia Khadija Kopa ambalo lilikuwa aina ya Noah lililokuwa limelazwa sehemu ya kupaki magari kwa kulipia. Gari hilo lililoibiwa maeneo ya Mwananyamala pamoja na magari mengine liliweza kukamatwa mjini Moshi likiwa limepakiwa nyumbani kwa mtu huku likiwa limeng'olewa rim zote huku likiwa limewekwa rehani na mtu ambaye alilinunua gari hilo, taarifa zaidi zinadai kuwa jambazi aliekamatwa na kuhusika na wizi huo anafahamika kwa jina la Ringo na anashikiliwa na polisi pia akiwa amekamatwa na magari mengine matatu.

WARIOBA: NI RUKSA KUJADILI MUUNGANO ASEMA HATA WANAOTAKA KUUVUNJA WALETE MAONI YAO YATASIKILIZWA

Elias Msuya MWENYEKITI wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao hata kama ni ya kutaka kuvunja Muungano katika mchakato wa kuundwa kwa Katiba mpya.  Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja kipindi ambacho kuna vuguvugu la kutaka Zanzibar ijitenge, linalofanywa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIK), na kusababisha machafuko visiwano humo. Jana, Jaji Warioba akizungumza na waandishi wa habari kutangaza kuanza rasmi kazi kwa tume hiyo tangu ilipozinduliwa rasmi April 13, mwaka huu, aliweka wazi msimamo huo unaoondoa mkanganyiko katika suala hilo.  Kumekuwapo sintofahamu kuhusu msimamo wa Serikali juu ya Muungano, hasa baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza suala hilo kama moja ya tunu za Taifa, ambayo haitakiwi kujadiliwa kwa lengo la kuuvunja. Jaji Warioba alifafanua kwamba, tume hiyo inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kwamba itakusanya maoni yote na kuyaratibu, ili kupata Katiba wanayoitaka wananchi wenyewe. 

MAONI NA USHAURI KUTOKA KWA MASHABIKI WA CLUB YA COASTAL UNION

Ibrah Ibrahm Jamani ningependa sana kutoa mchango wa mawazo ktk kutaka timu yetu ifanikiwe na ifike mbali. Hatuna budi kuhakikisha tuna kuwa na timu nzuri kuanzia ngazi ya chini mpaka juu, kweli niwajibu wa viongozi wetu kuhakikisha tunakuwa na timu bora ya u20 ambayo itakuwa ni tawi lakupata vijana ambao watakuwa tegemeo hapo baadae na mfano mzuri nipale tulipo fanikiwa kwa DANI amekuwawa mchezaji mzuri na tegemeo leo hii kwa coastal union Amakweli M/MUNGU ameibariki TANGA kwa watoto wenye vipaji vya kucheza mpira, viongozi hivi ss mpira huchezwa lakini pesa hutumika lazima mtumie fedha katika kupatikana kwa vijana na fedha ya kuwatunza yaani kuwaonyesha kuwajali nakuwa mahitaji muhimu niwazi kuwa zipo timu zinajipatia wachezaji kupitia timu B ( u20) . Leo hii tanga inatawaliwa na vijana wengi wenye vipaji lakini hupotea pasi nakuto fahamu wapi wamepotelea. Sio kwel kwamba coastal union inashindwa kuwa na academic au timu nzuri ambayo tuta pata wachezaji kam

ATUPELE GREEN Next samatta' ATUA COASTAL UNION

Afisa habari wa Coastal Union, Edo kumwembe (kushoto) akimkabidhi jezi mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Atupele Green 'Next samatta' mara baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo. Atupele ndiye mshambuliaji namba moja wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21.

DULLA WA MICHANO AFUNGUKA NA THE FRESH-2012

Akipiga stor na the fresh-2012 kwanjia ya mtandao jamaa alifunguka kama ifuatavyo Nipo dar but tanga nilikuja kwa matembez dat rigth nikwamba i have ar new song bt i need time coz am so so busy now kwa mambo ya kusoma ila naamin baada ya miez 2 itakuwa on air kwa tanga nilipokuja kuna ngoma nimefanya inaitwa supa ft kosh ila nikama mzuk Katka hiyo ngoma kuna kosh kesh,fat zinga, my young broo young dutch, and me so so watanzania mm nawambia sty tuney for me coz nipo kwajili yao maana najuwa wananipenda thas way kama blog ipo verry bhaaas inaweza kuwa pamoja na mimi

ATAJA KASORO ZAKE, ASEMA HAINA UNAFUU KWA WANANCHI WA KAWAIDA

Neville Meena, Dodoma  WAZIRI Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe jana aliwasilisha bungeni bajeti mbadala ya Kambi ya Upinzani kwa mwaka wa fedha 2012/2013, huku akibainisha kasoro lukuki katika bajeti ya Serikali ilioyowasilishwa Alhamisi iliyopita.Bajeti ya Zitto ilitanguliwa na hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Ofisi ya Rais – Mipango, Christina Mughwai ambaye pia aliweka wazi kile alichokiita udhaifu wa Serikali katika kuitekeleza mipango yake ya kiuchumi, hali ambayo inasababisha umaskini kwa wananchi. Hotuba zote mbili, ya Zitto na Lissu, zilisema licha ya Serikali kutangaza kwamba bajeti ya 2011/12 ilikuwa ya kupunguza makali ya maisha, hakukuwa na nafuu yoyote kwa wananchi kwani maisha yameendelea kupanda. Pamoja na kupendekeza njia kadhaa za kupanua wigo wa mapato ya Serikali, wapinzani wametaka kufanywa kwa ukaguzi wa deni la taifa, ili kubaini chanzo cha Serikali kukopa na kuweka wazi jinsi fedha hizo zilivyotumika hadi kufikia Sh22 trilio