Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2015

DC LUTAVI AONGOZA UZINDUZI WA TANGA KWANZA ENTERTAINMENT MWISHONI MWA WIKI NYUMBANI HOTEL

WA PILI KUTOKA KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA TANGA,ABDULLA LUTAVI,WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU ZA WILAYA YA TANGA,KASSI KISAUJI NA WA MKINGA OMARI MWASINGO NA MOHAMED CHAMAEMBE "BONGE WA KWANZA KUSHOTO MWENYEKITI WA TAASISI YA TANGA KWANZA ENTERTAINMENT MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM WILAYA YA TANGA(MNEC) KASSIM KISAUJI AKISALIMIANA NA VIONGOZI MBALIMBALI WALIOHUDHURIA UZINDUZI HUO WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WILAYA YA MKINGA,OMARI MWASINGO AKIMUONYESHA KITU MNEC MWENZIE WA WILAYA YA TANGA,ALHAJI KASSIM KISAUJI PICHA ZOTE NA PASKAL MBUNGA

Rais Kikwete Akiri Mazingira Mabovu Magereza

RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwapo mazingira mabovu ya Jeshi la Magereza nchini na kulitaka jeshi hilo kubuni njia za uzalishaji wa bidhaa zao zitakazoweza kuwaletea faida na taifa kwa ujumla.   Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana kwenye sherehe za kumaliza kozi kwa maofisa 104 wa ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza yaliyofanyika katika Chuo cha Taaluma na Urekebishaji Ukonga.   Alisema mazingira mabovu yanachangiwa na wingi, msongamano wa wafungwa na watuhumiwa katika magereza hali inayofanya jamii kuwa na malalamiko ya mara kwa mara.   “Kila mwaka wanaotetea haki za binadamu wanapopita kwenye magereza zetu, tunakuwa tunashindwa kwenye suala la msongamano ndani ya gereza na hii inaonyesha magereza tulizonazo 126 hazitoshelezi kulingana na kasi ya ongezeko la uhalifu.   “Hii inajidhihirisha wazi kwani kila inapofika sikukuu za Muungano Aprili 26, tunasamehe wafungwa, lakini ikifika Desemba 9 Sikukuu ya Uhuru unakuta wameongezeka mara mbili,”  alisema Rais Kikw

Magaidi Yaitikisa Tena Morogoro

POLISI mkoani Morogoro kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama imekamata washukiwa wa ugaidi waliokuwa na mifuko mikubwa iliyokuwa na majambia na bunduki kadhaa aina ya Shot gun.   Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Mussa Marambo, alisema hayo jana mjini hapa na kufafanua kwamba ni washukiwa sita kati ya 50 waliotiwa mbaroni, huku msako ukiendelea kuwatafuta wengine.   Kwa mujibu wa Kamanda Marambo, Jumatano iliyopita Polisi iliarifiwa na raia wema kuhusu uwepo wa watu hao katika Msitu wa Njeula katika kijiji cha Njeula tarafa ya Turiani, wilayani Mvomero.   Kukamatwa Baada ya taarifa hiyo, Kamanda Marambo alisema Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama, walifika eneo la msitu huo kufuatilia nyendo zao ili kuwakamata.   Hata hivyo, katika harakati za kuwakamata Kamanda Marambo alisema washukiwa hao walifanikiwa kutoroka, isipokuwa mmoja ambaye alitiwa mbaroni.   Katika purukushani hiyo msituni, Kamanda Marambo alisema

Matonya Feat. Rich Mavoko | Mule Mule | Official Music Video

11 wauawa kwenye mapigano Mali

Mshirikishe mwenzako 11 wauawa kwenye mapigano chini Mali Takriban watu 11 wameuawa Magharibi mwa Mali wakati wa mapigano kati ya wapiganaji wa kiislamu na jeshi. Mkaazi moja kwenye mji wa Nara, alisema kuwa watu hao waliwasili kwa magari na pikipiki mapema asubuhi ambapo walipandisha bendera yenye maandishi ya kiarabu. Walioshuhudia walisema kuwa wanajeshi walijibu ambapo kulitokea ufyatulianaji wa risasi karibu na msikiti na kituo kimoja cha afya. Shambulizi hilo linafanyika baada ya waasi wa kiarabu na wale wa Tuareg kutia sahihi makubaliano ya amani na serikali ya Mali.

NEC yaahirisha uandikishaji kwa BVR Dar es salaam

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji jijini Dar es salaa pamoja na mkoa wa Pwani kwa kutumia mashine za BVR lililokuwa linategemewa kuanza rasmi tarehe 4.7.2015 jijini Dar es salaam na  25.06.205 kwa mkoa wa Pwani.   Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo Habari, NEC imesema imeahirisha zoezi hilo kutokana na kuchelewa vifa vya uboreshaji kutoka mikoani ambako zoezi  hilo linaendelea pamoja na vifaa  vilivyokuwa vinakusudiwa kuanza kutumia Dar es salaam kupelekwa katika mikoa ambayo wananchi wamejitokeza kwa idadi kubwa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.   Hata hivyo tume hiyo imewataka wananchi kuwa watulivu wakati vifaa vikisubiriwa kutoka mikoani.   Kwa habari zaidi soma hapa taarifa kutoka Tume ya Taifa ya uchaguzi

Simba warejea Rwanda baada ya miaka 20

Mshirikishe mwenzako Simba warejea Rwanda baada ya miaka 20 Mfalme wa mwituni Simba ,atarejea Rwanda kwa mara ya kwanza tangu aangamie wakati wa mauaji ya kimbari mwaka wa 1994 Maafisa wanaowalinda wanyama pori wa Rwanda, wanasema kuwa simba watarudi nchini humo siku ya jumatatu kwa mara ya kwanza, tangu walipoangamizwa baada ya mauaji ya kimbari,ya mwaka wa 1994. Simba wawili dume, na majike watano, wanasafirishwa kutoka mbuga ya wanyama ya Kwazulu Natal, Afrika Kusini, na Jumatatu watawasili Rwanda kwa ndege. Simba hao 7 wanasafirishwa kutoka mbuga ya wanyama ya Kwazulu Natal, Afrika Kusini. Simba hao saba watawekwa kwenye karantini kisha waruhisiwe kutembea huru katika mbuga ya wanyama. Wanyama hao watapelekwa katika mbuga ya taifa ya Akagera. Maafisa wakuu huko Rwanda walisema, kurejeshwa tena kwa simba nchini Rwanda ,ni Kilele cha juhudi kubwa ya kuhifadhi mazingira katika mbuga hiyo na kwa taifa zima kwa jumla. Simba hao ni sehemu moja ya kampeini ya kuhifadhi Maz

Ija Music ft Issam_Kale Kabinti_@_Prdcer Issam touches.

JUMA BEE ,JIJI LA BONGO. prod by JB

Burundi upinzani kususia uchaguzi mkuu

Ban Ki-Moon ametoa wito kwa utawala wa nchi hiyo kuhairisha uchaguzi mkuu Nchini Burundi hali ya kisiasa inaendelea kutokota, huku vyama vya upinzani vikitangaza kususia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuanza wiki ijayo. Makundi ya asasi za kiraia yamewaomba raia wa nchi hio kususia kura hio, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akitaka uchaguzi mkuu wa Burundi kuahirishwa. Makundi ya kutetea haki za kibinadamu nchini Burundi yametoa wito kwa wapiga kura nchini humo kususia uchaguzi wa ubunge unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu. Mashirika hayo yamesema kuwa kwa sasa mazingira ya kisiasa nchini humo hayawezi kuruhusu uchaguzi huru na wa haki, kufuatia miezi kadhaa ya ghasia. Makundi hayo ya kijamii yametoa taarifa ya pamoja yakitoa wito kwa jamii ya Kimataifa kutotambua uhalali wa uchaguzi huo. Wakati huo huo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa utawala wa nchi hiyo kuhairisha uchaguzi mkuu baada ya vyama vya upinzani kutangaza kuwa ha

Tukielekea Uchaguzi : Wagombea urais CCM wagonga 40

Kada wa CCM, Helena Elinawinga akionyesha begi lenye fomu za kuomba kugombea kiti cha Urais kupitia chama cha CCM, baada ya kukabidhiwa jana katika makao makuu ya chama hicho, mjini Dodoma.  Dodoma/Dar.  Mtafiti binafsi na kada wa CCM, Helena Elinawinga (41), amejitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama chake kuwania urais na kusema amefikia uamuzi huo ili kupunguza kujirudiarudia kwa adhabu za vifo kwa viongozi. Helena anakuwa kada wa 40 wa CCM kuomba ridhaa ya chama hicho kuteuliwa kupeperusha bendera yake katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Kada huyo ni mwanamke wa sita kuchukua fomu za kuomba kuwania nafasi hiyo katika chama hicho akitanguliwa na Balozi Amina Salum Ali, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk Mwele Malecela, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro, Monica Mbega na Ritta Ngowi. Helena alifika katika ofisi za Makao Makuu ya CCM saa saba mchana akiwa ndani ya bajaji lakini tofauti na wenzake, akiwa amevali

Kaimu Mufti akutana na rais Kikwete ikulu.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry Ikulu jijini Dar es salaam. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Sheikh Suleiman Lolila. aimu mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry amekutana na Rais Kikwete ikulu jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imebanisha kuwa sheikh Abubakar Zubeiry alifika Ikulu jana na kukutana na Rais Kikwete akiwa na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Sheikh Suleiman Lolila aliyeongoza naye.