Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2015

DOWNLOAD NAY WA MITEGO - LOWASSA - MP3.

CLIIP NYUMA YAPAZIA TV ONLINE 1

Yaliyojiri Jijini Tanga leo

 Pamoja na Wapeperusha Bedera za Vyama vyao kuwania Ubunge jimbo la tanga walivyorudisha fomu: Mbunge mtetezi na mwakilishi wa CCM mh.  Omari R Nundu  Alingia kimnya kimnya Ofisini kwa Mkurugenzi wa Jiji la Tanga kunako saa nne Asubuhi akisindikizwa na Wana CCM wapatao nane mpaka 10 hivi.   Pia Chama cha Wananchi CUF kiliingia kwa Vishindo kwa Msafara wa Magari na Honi wakimsindikiza Mpeperusha bendera wao Mh. Mussa Mbaruku, akina mama na baba wakiwa na vijana walionekana wakiwa na Hamasa katika kutimiza zoezi hilo la kurudisha Fomu. hii ilikuwa ni kama saasaba kasoro hiv

Tume ya Uchaguzi (NEC) imewaengua wagombea urais wa vyama vya Ada/Tadea, DP, CCK na AFP leo kwa maelezo kuwa wamekosa vigezo vya kugombea nafasi hiyo kubwa ya uongozi hapa nchini.

Kwa mantiki hiyo, Mchungaji Christopher Mtikila (DP), Godfrey Malissa (CCK) na John Chipaka (Ada-Tadea) hawatashiriki katika kinyang’anyiro hicho baada ya fomu zao kuonekana kuwa zina kasoro huku mgombea urais wa AFP, Omari Sombi akiungana na wanasiasa hao kutogombea baada ya kushindwa kurejesha fom u ya urais. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva, wagombea wa vyama vinane kati ya 12 vilivyochukua fomu, wamekidhi matakwa ya sheria ya mchakato huo, hivyo wanaruhusiwa kuanza kampeni rasmi kesho. Amewataja wagombea waliopitishwa na NEC ni Dk. John Magufuli (CCM), Edward Lowassa (Chadema), Fahmi Dovutwa (UPDP), Macmillan Lyimo (TLP) na Chief Lutalosa Yemba (ADC). Wengine ni Anna Mghwira (ACT-Wazalendo) na Hashimu Rungwe (Chaumma) na Malik Kasambala (NRA). (C) Mwananchi Je, Tutarajie Mchungaji Christopher Mtikila Kutinga Mahakamani kupinga katazo hilo??

Salva Kiir akataa kutia sahihi mkataba

Salva Kiir Serikali ya Sudan Kusini imekataa kusaini mkataba uliotarajiwa kuleta amani na kumaliza mapigano yaliyodumu nchini humo kwa zaidi ya miezi ishirini. Hata hivyo waasi na makundi ya upinzani wamesaini kwa upande wao. Serikali imeomba kuongezewa siku kumi na tano zaidi kushauriana juu ya mapendekezo hayo. Waziri kutoka Uingereza anayesimamia maswala ya Afrika ameitaka serikali ya Sudan Kusini kutia sahihi mkataba huo haraka iwezekanavyo. Amesema kuwa watu hawafai kusheherekea hadi pale rais Kiir atakapotia sahih

Tchetche, 3-5-2 tishio kwa Yanga

Kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm amesema hana wasiwasi na mfumo wa 3-5-2 unaotumiwa na Azam FC tayari ameshapata mbinu ya kuwamaliza katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Jumamosi kwenye

Kassim Mganga: Gwiji anayewaza kukuza utamaduni wa pwani

kassim Mganga  Kwa ufupi Ukimuona kwa mbali unaweza ukahisi kuwa ni kiumbe mzito, lakini ukimpa muda wa kurembesha jukwaa lako kwa burudani, utagundua kuwa umbo lake na sanaa anayofanya ni vitu viwili tofauti. By Henry Mdimu Ukiwa msikilizaji mzuri wa muziki, hasa wa kizazi kipya kuna wakati utakubaliana na kauli isemayo katika nyimbo bora zilizotoka mwaka huu ambazo zina mafunzo ambayo mabinti hupenda kuyasikia, hutaacha wimbo uitwao “Subira” wa kijana mdogo kutoka Tanga, Kassim Hemed Mganga. Ukimuona kwa mbali unaweza ukahisi kuwa ni kiumbe mzito, lakini ukimpa muda wa kurembesha jukwaa lako kwa burudani, utagundua kuwa umbo lake na sanaa anayofanya ni vitu viwili tofauti. Ana uwezo wa kusherehesha kwa takriban masaa matano bila kuchosha mashabiki wake. Kibao chake cha “Subira” ndiyo habari ya mjini; kwenye pub, baa, klabu, bodaboda, bajaj, redioni na simu za mikononi ni “Subira, Subira Subira”. Ni kibao kilicho katika miondoko ya pwani, hasa chakacha, n

Hamahama ya wanasiasa yatikisa vyama

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja akizungumza na waandishi wa habari wakati yeye na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita (wa pili kulia), wakitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema.  Kulia ni Sheikh Sadick Burhani kutoka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu na Shura ya Maimam. Picha na Said Khamis  Kwa ufupi Kundi la waliohama linajumuisha mawaziri, wabunge, madiwani By Fidelis Butahe, Mwananchi Dar es Salaam.  Wimbi la wanasiasa kuhama vyama wakati wa uchaguzi limekuwa la kawaida, lakini miaka 20 baada ya siasa za vyama vingi kurejeshwa, hali hiyo inaonekana kutikisa vyama hasa baada ya kutawaliwa na mawaziri, wabunge na madiwani. Tangu Rais Jakaya Kikwete atoe hotuba yake ya mwisho kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano, wanasiasa wamekuwa wakitangaza kukimbia vyama vyao, na hali hiyo ilikolezwa baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuihama CCM na kujiunga na Chadema mwishoni mwa Julai, baada ya jina lake ku

Wadau wakosoa kambi ya Stars

Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa mazoezini kujiandaa kwa mchezo wa michuano ya awali ya Mataifa ya Afrika ya 2017 (Afcon) dhidi ya Nigeria. Mazoezi hayo yanafanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Picha na Said Khamis  Kwa ufupi Kocha Charles Mkwassa amelazimika kuita wachezaji 10 wa ziada kujaza nafasi za wachezaji kutoka Yanga na Azam  zilizoweka kambi nje ya  Dar es Salaam. Stars inajiandaa kwa mechi ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Nigeria. By Oliver Albert, Mwananchi Dar es Salaam.  Uamuzi wa Shirikisho la Soka Tanzania  (TFF) kuitisha kambi ya timu ya Taifa wakati klabu zikiwa kwenye maandalizi ya msimu mpya wa ligi, umepokewa kwa hisia tofauti na wadau wa mchezo huo, baadhi wakizilaumu Yanga na Azam kwa kuzuia wachezaji wao na wengine wakiliponda shirikisho hilo kwa kutokuwa makini. Kocha Charles Mkwassa amelazimika kuita wachezaji 10 wa ziada kujaza nafasi za wachezaji kutoka Yanga na Azam  zilizoweka kambi nje ya  Dar es Salaam. Stars inajiandaa kwa

Lowassa: Sitaki mchezo

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowasa akiwapungia mkono wafuasi wa chama hicho baada ya kuwasili katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya jana. Picha na Godfrey Kahango.  Kwa ufupi Umati wa watu ulikuwa ukimsubiri nje ya uwanja huo na alipotoka ilianza safari ya kuelekea katikati ya jiji na msafara wa zaidi ya magari 20 pamoja na pikipiki. By Lauden Mwambona na Godfrey Kahango, , Mwananchi Mbeya.  Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa jana alipokewa na maelfu ya watu mjini hapa ambao kwenye uwanja wa Ruanda, Nzovwe, aliwaambia wananchi kuwa hatataka mchezo katika serikali atakayoiongoza. Pamoja na Jeshi la Polisi kutangaza kuzuia msafara wakati wa ziara ya waziri huyo mkuu wa zamani, hali ilikuwa tofauti jana wakati zaidi ya magari 20 yalimsindikiza kutoka Uwanja wa Ndege wa Songwe huku wananchi wakijitokeza barabarani kumshangilia hadi kwenye uwanja huo, ulio nje kidogo ya mji wa Mbeya ambako alihutubia. Polisi walinda msa

SINGASINGA WA ESCROW ATUA CHADEMA RASMI NA CHAMA KUZIDI KUIMALIKA.

mmiliki wa kampuni ya IPTL Herbinder Singh Seth almaarufu kama SINGASINGA saa na wakati wowote anatarajiwa kujiunga Na CHADEMA na kwamba inasemwa mipango yote ya kufanya hivyo imekamilika. Taarifa zinasema SETH ambaye amekumbwa na SKENDO maarufu ya ESCROW ameamua kuhamia CHADEMA baada ya kugundua kwamba Chama hicho ndio eneo pekee anapoweza kusafishwa na kuonekana Hana hatia kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake EDWARD LOWASSA. taarifa zinazidi kutonya kwamba SINGASINGA anatarajiwa Kutua nchini saa yoyote kutoka Sasa na kwamba atapokelewa kwa maandamano makubwa kuanzia uwanja wa ndege mpaka makao makuu ya CUF Buguruni Kisha makao makuu ya Nccr Mageuzi yaliyopo ilala na baadae makao makuu ya chadema yaliyopo kinondoni UFIPA ambapo anatarajiwa kufanya Press conference akiambatana na wabia wake wa kibiashara akiwemo James Rugemalila wa kampuni ya VIP na wamiliki wa kampuni ya Simba Trust. Kitendo cha SINGASINGA kuamua kujiunga na CHADEMA kinatarajiwa kuwa cha kusisimua na cha aina

DOWNLOAD JUX FT JOH MAKINI - LOOKING FOR YOU - MP3.

EDWARD LOWASSA ASEMA CCM NI HODARI WA KUIBA KURA, SOMA ZAIDI

Mgombea wa urais kupitia Chadema, Edward Lowassa ameituhumu CCM kuwa ni hodari wa kuiba kura hivyo akawataka wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura ili hata sehemu ya kura hizo ikiibiwa, Ukawa ishinde kwa kishindo. Lowassa ambaye ni waziri mkuu wa zamani aliuambia umati wa wafuasi wa Ukawa uliojitokeza jana kumpokea katika ofisi za makao makuu ya CUF yaliyopo Buguruni kuwa ili kufanikisha ushindi wa kuwawezesha kuingia ikulu hawana budi kushikamana, kushawishiana kupiga kura kwa wingi na kuzilinda Oktoba 25. Kauli hiyo ya Lowassa ambaye amelelewa kisiasa na CCM tangu alipojiunga akiwa mdogo mwaka 1977, inaendeleza tuhuma ambazo hutolewa na vyama vya upinzani kuwa chama hicho huchakachua matokeo wakati wa uchaguzi. Hata hivyo, Lowassa hakuwa na vielelezo wala kuthibitisha kuhusu tuhuma hizo dhidi ya chama chake cha zamani. “Tukiwa na umoja, tukiwa na mshikamano tutawaondoa Jumapili asubuhi sana. Tutahitaji mshikamano, tatahitaji ushawishi wa kupiga kura tupate an

Picha mbalimbali Mh Edward Lowassa Mgombea wa UKAWA alipokwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya Chadema.

Chris Brown avamiwa nyumbani kwake na watu wenye silaha za Moto.

Hili litakuwa ni tukio la pili la uvamizi ambalo litakuwa limempata Chris Brown katika mwaka huu, ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwezi may mwezi huu ambapo alivamiwa na watu wenye silaha Nyumbani kwake. Chris Brown anaishi katika mitaa ya Tarzana Mjini Los Angeles Calfonia nchini Marekani, wakati majambazi hayo yalipovamia nyumbani kwa Chris hawakuweza kumkuta na walifanikiwa kuiba vitu vyenye thamani kubwa. Kwa mujibu wa Mtandao wa TMZ wamesema kuwa Tukio hilo lilitokea siku ya tarehe 15 mida ya sa 8 wakati Chris Brown akiwa kwenye starehe.

Rais Kikwete azuia ‘ULAJI ’ Trafiki.......Ataka Baraza la Usalama Lianzishe Mfumo wa Kulipa Faini Kwa Njia ya Benki

RAIS Jakaya Kikwete ameliagiza Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, kuanzisha mara moja mfumo wa ulipaji faini kwa njia ya Benki na mitandao ya simu za mkononi ili kupunguza ushawishi wa vitendo vya rushwa kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani nchini. Pia, ameagiza kuanzishwa mfumo wa kuweka alama kwenye leseni za madereva wanaokiuka sheria na kutumia njia hiyo kuwafungia, ikiwa ni hatua mojawapo ya kudhibiti wimbi la ajali za barabarani hapa nchini. Rais Kikwete alitoa agizo hilo jana katika viwanja vya Tangamano wakati alipokuwa akizindua Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa, inayofanyika mkoani Tanga, ikiwa imebeba kaulimbiu inayosema ‘Endesha Salama, Okoa Maisha’. Alisema asilimia 56 ya ajali za barabarani, zinatokana na uzembe na ukosefu wa umakini kwa madereva na kwamba hatua hiyo inasababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali na hata kuathiri ustawi wa Kaya na Uchumi wa Taifa. “Hivi mpaka sasa Baraza na Kikosi cha usalama barabarani wanashin

Batuli 'Amwaga Machozi' Baada ya Picha zake za Nusu Uchi Kusambazwa Mitandaoni

Staa wa mrembo wa Bongo Movie, Batuli ameonyesha kuchukizwa kwake kwa kitendo cha staa mwenzake, Kitale kuvujisha picha hizi  akiwa faragha na mwigizaji chipukizi, Stanbakora ikiwa ni kati ya moja ya kipande cha kazi yao mpya, kwa madai kuwa anaipa ‘promo’.     Kupitia ukurasa wake mtandao Batuli ameeleza kuwa Kitale alimpa picha hizo Mateja ambaye ndiye aliezisambaza kwenye mtandao wa Instagram.     “Kwanza mniwie radhi Watanzania mnachokiona na kinachoelezewa ni vitu viwili tofauti mwenye akili timamu anapata jibu kamili. @mkudesimbaoriginal  nikuulize hivi wakati unampa @matejamusa picha ulimwambia ni za nini!? hivi naweza kuwa faragha mbele ya camera!?      "Hata kama unapromote movie hii sio kiivyo kama kupromote kitu ndio hivi basi fani yetu imejaa mazumbukuku, hii ni scene iliyopo kwenye movie sioni sababu ya kunichafua kijinga hivi, kizuri kinajiuza @mkudesimbaoriginal   kuandika shit sio njia sahihi ya kupromote kazi yako” - Batuli aliandika.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya August 4

Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Jumanne  ya  August  4