Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2013

Zitto, Lema katika vita ya maneno

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu hali ya vurugu  zinazoendelea Mtwara katika sakata la mradi  Gesi asilia kuja Dar es Salaam.PICHA NA VENANCE NESTORY  Na Neville Meena, Mwananchi Dodoma:  Wabunge Wawili Maarufu wa Chadema, Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini) na Godbless Lema (Arusha Mjini) wameingia katika vita ya maneno ambayo chanzo chake ni kauli ya Lema aliyotoa katika kikao cha wabunge (briefing) kilichofanyika mjini Dodoma Jumanne wiki hii. Lema akizungumza katika kikao hicho, anadaiwa kutoa maneno ambayo yalitafsiriwa na wabunge wengi kuwa yalikuwa yakimlenga Zitto kuhusu hatua yake ya kukataa posho na kumtuhumu kwamba ana ukwasi ambao unapaswa kuhojiwa. Gazeti hili lilimtafuta Lema likirejea taarifa iliyotolewa na Zitto akilalamika kwamba Lema alimshambulia katika kikao hicho cha wabunge wote na kwamba alikuwa akimlenga yeye. Lema, hata hivyo, alikiri kuzungumzia suala hilo akise

SERIKALI YATANGAZA VIWANGO VIPYA VYa ALAMA ZA UFAULU ELIMU YA SEKONDARI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya upangaji wa viwango vya alama, matumizi ya alama endelevu ya mwanafunzi na ufaulu leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalasesa. Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome (hayupo pichani). Waandishi wa habari na maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome(hayupo pichani). Picha zote na Eliphace Marwa (MAELEZO). ======== ======= ======== UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU UTANGULIZI Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi

INDUSTRY SOUND KUANDAA TAMASHA LA KUITAMBULISHA STUDIO' TANGA

Akizungumza na blog hii kwa niaba ya mkurugenzi wa studio hiyo prudyuza chapsy, amesema tamasha hilo litafanyika mwanzoni mwa mwezi ujao ambalo litawakusanyisha  takribani nusu ya wasanii  wa tanga wakisindikizwa na wakali wengine ktk dar. tamasha hilo ambalo limepewa nguvu kubwa na  kampuni inayojishulisha na mambo ya kiburudani ya ZECHA ENTERTAINMENT ikshirikiana na umoja wa wasanii  waliorikodi studio hiyo litakuwa ni la kihistoria  kwani mpaka sasa maandalizi  yako vizuri tu, kwa upande wa prodjuza chapsy amesema, ''ninatahakikisha na ninaahidi kufanya kazi nzuri  kwa kila atakaye rikodi kwetu na mifano ipo namtaiona kwani mpaka sasa nimefanya kazi nawasanii wengi tu km wizaman,shaksi msela,man o na baguje zikiwa tayari mtazisikia

MAKAMBA AZIPIGA TAFU SHULE ZA SEKONDARI BAGA NA TAMOTA TANGA

MH! Januar makamba pichani Na Raisa Saidi, Bumbuli,    Mbunge  wa  jimbo  la  Bumbuli  January Makamba  amekabidhi  msaada  wa  shilingi  milioni mbili  katika  shule  ya  sekondari  ya Baga na  Tamota   kwa  ajili  ya  ujenzi  wa  Maabara   kwa lengo la  kuinua  masomo  ya  sayansi. Pamoja na msaada huo wa milioni moja moja kwa kila shule pia ametoa  msaada  wa  mabati  mia moja kwa kila shule kwa ajili ya  kuezekea  vyumba  vya  madarasa  na nyumba  za walimu   katika  shule hizo. Alitoa msaada huo wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne kwenye shule hizo. Makamba  ambae  pia  ni  Naibu  Waziri wa  Mawasiliano  Sayansi  na  Tenknolojia  alisema  kuwa  lengo  la  kutoa  misaada  hiyo  ni  kutaka  kuongeza  na  kuinua  kiwango  cha   elimu   katika  shule   zilizopo  katika  jimbo hilo. Mbunge huyo  alisema kuwa msaasa huo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa serikali katika kuhakikisha kila shule ya kata inakuw

Mtuhumiwa SUGU akamatwa SIMIYU, akutwa na silaha 45 za vita, 17 za kienyeji na idadi kubwa ya risasi

OPERESHENI  Maalumu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu kukabiliana na vitendo vya Ujambazi, Ujangiri wa uwindaji haramu pamoja na wahamiaji haramu umefanikisha kukamatwa kwa silaha 45, zikiwemo za Kivita na 17 za kienyeji na risasi 892 na magazine 24 huku watuhumiwa sugu wa ujambazi na ujangiri wakitiwa mbaroni. Akizungumza jana na mbele ya waandishi wa Habari ofisini kwake, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Salum Msangi (pichani) alisema kuwa opresheni hiyo ilitokana na kuwepo vitendo vya uhalifu katika Wilaya tano za Mkoa huo na kwenye maeneo ya mbalimbai ya Mapori Tengefu ya Uwindaji kwa kipindi cha mwaka moja tangu kuanzishwa kwake Desemba 2012. Kamanda Msangi alieleza kuwa miongoni mwa silaha hizo 45 na magazine 28 zilikamatwa ni pamoja na SMG 7 risasi 763 na G3 moja ikiwa na risasi zake 35 iliyokuwa ikitumiwa na mwanamke mmoja aliyekamatwa Hollo Mabuga (28) mkazi wa Wilayani Bariadi, silaha nyingine 13 zilisalimishwa kwa hihali na baadhi ya watu wali

Saini zakusanywa kumng’oa Makinda

Spika wa Bunge, Anne Makinda (kulia) akizungumza na Mbunge wa Viti Maalumu, Clara Mwatuka na Mbunge wa Kilolo, Profesa Peter Msola katika Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana.PICHA NA EDWIN MJWAHUZI  Na Sharon Sauwa,Mwananchi  Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, (CCM), leo anatarajiwa kuanza kukusanya saini za wabunge akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa madai kwamba amekuwa akikiuka kanuni za Bunge. Dk Kigwangalla aliibua hoja ya kutokuwa na imani na Spika katika kikao cha wabunge wote cha kuelezea shughuli zitakazofanywa na Bunge katika mkutano wa 13, kilichofanyika juzi jioni kwenye ukumbi wa Pius Msekwa. Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, jana alithibitisha kuwapo kwa mjadala huo katika kikao cha wabunge, lakini hakuwa tayari kueleza kwa undani na badala yake alisema kwamba leo ataanza kukusanya saini za wabunge kwa ajili ya kukamilisha hoja ya ku

Wakenya kuripoti rushwa kwa Rais

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata amezindua Mtandao kwa ajili ya Watu kuripoti moja kwa moja kwake taarifa za matukio ya rushwa. Watumiaji wa Mtandao huo watakuwa wakiweka picha za mnato na video pia na vielelezo vingine na kuelekeza malalamiko yao katika idara mbalimbali za serikali zilizoorodheshwa. Taarifa zinazohusiana ufisadi Pia watu watapata fursa ya kupeleka malalamiko yao juu ya vitendo vya rushwa kwa kutumia ujumbe mfupi wa maandishi moja kwa moja kwenda kwa Rais Kenyata. Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Transparency International ni nadra kwa Watu kutoa taarifa juu ya vitendo vya rushwa nchini Kenya kwa kuwa wanahisi kuwa hakuna hatua zozote zitakazochukuliwa. Kenya ni inaelezwa kuwa nchi ya 139 kati ya 176 zilizo katika nchi yenye rekodi ya kuhusika na vitendo vya rushwa. Rais Kenyatta analenga kuisafisha Serikali yake na kupambana dhidi ya vitendo vya rushwa nchini Kenya.

Kendrick Mabeste kusaini ‘deal’ la kutangaza maduka yenye bidhaa za watoto

Mtoto wa rapper Mabeste, Kendrick ambaye ana miezi mitatu sasa, ataanza kuonekana akitangaza maduka yanayouza bidhaa za watoto (pampers,diapers na n.k). Mabeste amesema tayari amemfungulia mwanae akaunti kwenye mitandao ya kijamii,Facebook page yake 'Kendrick Mabeste' na pia kupitia blog hii ya  www.mabestevenance.blogspot.com  ambako huko ndiko atakuwa akipromote maduka hayo. "Soon kwanzia mwezi ujao tu anaweza akaanza kupromote maduka hayo kupitia mitandao hiyo" alisema Mabeste.