Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2013

BALAA JUU YA BALAA: MASOGANGE NA MWENZAKE MELISA WARUDISHWA RUMANDE! HAKUNA DHAMANA WALA NINI!!!! CHEKI HAPA YANI HADI HURUMA.

         Dawa za kulevya.   Huku  akiwa hajui nini hatima ya kesi inayomkabili ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini, Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ amep ata balaa jipya.   Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo nchini humo, Masogange na mwenzake aliyekamatwa naye, Melisa Edward wamefutiwa dhamana hivyo wamerudi tena rumande. Agnes Gerald ‘Masogange’. KWA NINI DHAMANA IFUTWE ?. Habari zinadai kuwa, dhamana za wawili hao zimefutwa kufuatia kuhisiwa kwamba wana mpango wa kuondoka nchini huko kinyemela na kurejea Tanzania, jambo ambalo limetafsiriwa kama jaribio la kuikimbia kesi hiyo.   “Unajua huku Sauzi si kila mtu anawaonea huruma Masogange na Melisa kwa tatizo lililowapata, sasa utakuta maskani mtu anaropoka vitu vya ajabu pengine vya uongo bila kujua kuwa si kila mtu anayesikiliza atayaachia hapohapo, wengine ni ‘mainfoma’ wanayafikisha mbele. “Hicho ndicho kilichomtokea Masogange,

HUYU NDO MSANII ALIYETANGAZA KUMPORA MUME WA AUNT EZEKIEL..

KATIKA hali isiyo ya kawaida msanii anayechipukia katika filamu za Kibongo, Isabella Fransis ‘Vai wa Ukweli’ anamtafuta ubaya gwiji katika tasnia hiyo, Aunt Ezekiel kwa kusema anamtamani mumewe. Vai wa Ukweli bila ya kupindisha maneno amedai kuwa hapati usingizi kutokana na kumzimia Sunday Demonte ambaye ni mume wa Aunt. Akizungumza na mwandishi wetu, Vai alisema ili kuonesha kuwa anachokisema kinatoka moyoni mwake, amekata vipande vya picha za Dimonte na kuvibandika chumbani kwake.  “Kusema ukweli nampenda sana Sunday na sijaanza kumpenda leo wala jana kwani namfahamu tangu zamani alipokuwa Kariakoo,” alisema Vai. Msanii huyo chipukizi alisema anamuonea wivu Aunt kwa kuamini kuwa anafaidi sana kwa kuwa na mwanaume huyo.   Kwa upande wake Aunt alishangazwa na taarifa hizo na akaomba atafutwe baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili ajue cha kufanya.

RAY C ATANGAZA KURUDI UPYA KWENYE GAME LA MUZIKI.....

Mabibi na mabwana mko tayari kwa ujio mwingine wa Ray- C. Malkia wa kiuno bila mfupa Rehema Chalamila aka Ray-C ametangaza ujio wake rasmi baada ya kuwa chimbo kwa kipindi kirefu toka apate matatizo miezi kadhaa iliyopita. Ni baada ya siku chache kupita toka Ray-C atamke kuwa anapenda sauti ya ‘dogo lake’ Recho na kuwa atakuja kufanya naye kazi, leo amethibitisha kuwa mwezi Agosti ndio anarudi rasmi kutoka chimboni. Kupitia akaunti ya Instagram Ray-C aliweka picha ya gazeti moja lililoandika ‘Ray-C kuonekana hadharani mwezi Agosti’, na baada ya followers wake kutaka ufafanuzi ndipo alifunguka kwa kusema “For Sure it’s bout time nw nimewapa muda sana watoto sasa mdada is coming back”. Ray C aliwauliza marafiki zake wa Instagram kama wapo tayari kwa ‘come back’ yake, wengi wameonekana kutamani muda ufike waweze kumuona tena Ray-C akirudi katika muziki. Hizi ni baadhi ya comments kutoka kwa mashabiki wake.

Kikwete: Atakayethubutu kuigusa Tanzania atakiona

Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete ametuma ujumbe kwa wale wanaoitishia Tanzania. Amewaambia wakithubutu watakiona cha mtemakuni kama ilivyokuwa kwa Idd Amin wa Uganda. Alisema mamlaka za ulinzi na usalama zilimdhibiti Amin alipofanya uvamizi katika ardhi ya Tanzania mwaka 1978 na kwamba hazitashindwa kufanya hivyo kwa mtu mwingine yeyote atakayechezea usalama wa nchi. Wakati Rais akisema hayo, Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange amewahakikishia wananchi kuwa wakati wote jeshi liko imara na kuwataka wasiogope lolote. Viongozi hao walisema hayo jana katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa iliyofanyika katika Kambi ya Jeshi ya Kaboya iliyopo Muleba, Kagera. “Sihitaji kusema tena, mmeshamsikia Mkuu wa Majeshi, atakayejaribu atakiona cha mtemakuni, laleni usingizi na msiwe na wasiwasi, msisikilize maneno ya mitaani,” alisema Rais Kikwete na kuongeza: “Wakati wowote, saa yoyote tuko tayari kulinda nchi yetu. Hatuko tayari kuona amani inaharibika nchini, hatuwe