Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2013

Mzigo huo hapo Ijumaa hii 28 - 6 - 2013 REDD'S MISS KANDA NYANDA ZA JUU KUSINI

Mzigo huo hapo Ijumaa hii 28 - 6 - 2013 REDD'S MISS KANDA NYANDA ZA JUU KUSINI Kuanzia saa 1:00 USIKU ndani ya Ukumbi wa MTENDA SUNSET. Warembo 18 kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Katavi, Njombe na Ruvuma ndani ya Stage moja katika Kinyang'anyiro hicho. Kiingilio ni kama Ifuatavyo VIP Tsh 25,000/= pamoja na CHAKULA BURE na KAWAIDA Tsh 10,000/= Burudani FM ACADEMIA watakuwa wakisindikiza burudani safi kabisa.... REDD'S MISS KANDA NYANDA ZA JUU KUSINI. Imedhaminiwa na R EDDS, MOUNTAIN DEW, MICHUZI MEDIA GROUP, BOMBA FM, MAN COMPANY LTD, EBONY FM, SWEET FM & ROCK FM ....... Karibuni Njoo ushuhudie mwenyewe nani kuibuka mshindi?.

MAMA KANUMBA APANGA KUZIFANYIA SHEREHE TUZO ZA MWANAYE...!!

MAMA wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka kuwa yupo katika maandalizi ya sherehe (mnuso) ya tuzo za mwanaye ambazo amezipata kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu afariki dunia. Akichonga na Nasi juzikati, mama huyo alisema tangu Kanumba afariki dunia amepata tuzo zipatazo tano hali inayompa faraja na wakati mwingine kuhisi kama mwanaye bado yupo hai.  “Niko kwenye maandalizi ya kufanya sherehe ya tuzo za mwanangu Kanumba kwani nimepewa tuzo zake zipatazo tano ambazo zimekuwa faraja sana kwangu na kujiona kama niko naye, kutokana na heshima ambayo anapewa najiandaa muda wowote nitazifanyia pati tuzo hizo,” alisema mama Kanumba.

HATIMAYE BIBI YAKE OBAMA SARAH OBAMA ATIA TIM TZ !

SIKU CHACHE KABLA YA ZIARA YA RAIS WA MAREKANI KUJA NCHINI TANZANIA IMEFAHAMIKA KUWA BIBI YAKE NA RAIS ''OBAMA'' MAMA SARAH OBAMA ANATARAJIA KUJA NCHINI TANZANIA KUJA KUMSALIMIA MJUKUU WAKE HUYO. AKIZUNGUMZA  JUZI KIJIJINI KWAKE ENEO LA KWEGERO HUKO KISUM BIBI HUYO ALIEZALIWA MWAKA 1922 AMESEMA KUWA HAJISKII VIBAYA OBAMA KUTOITEMGELEA KENYA KWANI ANAJUA KUWA OBAMA NI RAIS WA TAIFA KUBWA DUNIANI,HIVYO ANAKUWA NA RATIBA AMBAYO INAZINGATIA MAMBO MENGI NA NI VIGUMU SANA KUIVUNJA. BIBI HUYO AMEENDELEA KUSEMA KUWA ANAJISIKIA FURAHA KUONA MJUKUU WAKE HUYO KUJA TANZANIA KWANI HISTORIA INAONYESHA KUWA KABILA LA KIJALUO LINAMUINGILIANO MKUBWA KATI YA NCHI HIZI MBILI ZA TANZANIA NA KENYA HIVYO WAO WANAAMINI KUWA OBAMA AMEITEMBELEA NCHI YA NYUMBANI KWAO.#

Wakesha wakimuombea Mzee Mandela

Mandela bado anaugua sana hospitalini Raia wa Afrika kusini wamekesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson mtaani Soweto. Rais Jacob Zuma amesema kuwa afya ya shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo inaendelea kuimarika. Taarifa zinazohusiana Afrika Kusini Mandela aliye na umri wa miaka 94 amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa maambukizi ya mapafu. Awali mwanawe wa kike, Makaziwe amesema afya ya babaake inaendelea kuwa njema. Aidha Makaziwe amevikashifu vyombo vya habari kwa kukita kambi nje ya hospitali alikolazwa shujaa huyo akisema wanahabari wanapaswa kumheshimu babaake. Rais Jacob Zuma alisema Alhamisi kuwa hali ya Mandela iliimarika lakini bado yuko hali mahututi.

Waziri wa Fedha, Dr Mgimwa awasilisha Bajeti ya serikali 2013/14

Wana jamii, leo ndiyo siku ambayo hatma ya maisha ya mtanzania kiuchumi kwa mwaka wa fedha 2013/2014 inaenda kuainishwa na waziri wetu wa fedha dr W.Mgimwa pale atakapo wasilisha bajeti ya serikali. =================== Isome: Bajeti-2013/14 - Tanzania Kifupi: - Katika kipindi cha Julai hadi Aprili 2013, Serikali ilikopa shilingi bilioni 1,364.7 kutoka soko la ndani la mitaji kwa ajili ya kulipia dhamana za Serikali zilizoiva pamoja na shilingi bilioni 809.1 kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo. - Mwaka 2012/13 Serikali ilikadiria kupata mikopo yenye masharti ya kibiashara shilingi bilioni 1,254.1, sawa na Dola za Kimarekani milioni 800 kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika bajeti ya mwaka 2012/13 iliyopitishwa na Bunge lako tukufu. Hadi kufikia Mei 2013, Serikali ilipokea shilingi bilioni 947, sawa na dola milioni 600 kutoka benki ya Stanbic, na shilingi bilioni 59.2, sawa na dola milioni 37 kutoka benk ya Credit Suisse.

KISHINDO CHA BAJETI LEO NCHI NZIMA MASIKIO YOTE NA MACHO DODOMA!

Macho na masikio ya Watanzania leo yataelekezwa kwa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa wakati atakapoisoma hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kuanzia saa 10.00 jioni bungeni, mjini Dodoma. Sambamba na Mgimwa, pia mawaziri wa fedha za nchi za Kenya na Uganda nao katika muda huo watasoma bajeti za nchi zao. Waziri mpya wa Fedha wa Kenya, Henry Rotich atasoma bajeti ya kwanza ya nchi hiyo ikiwa chini ya utawala mpya wa Rais Uhuru Kenyatta wakati ya Uganda itasomwa na Waziri wa Fedha, Maria Kiwanuka. Mwelekeo wa Bajeti Dk Mgimwa aliwaambia waandishi wa habari, Dodoma jana kuwa Serikali imetenga kiasi cha Sh18.2 trilioni kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha wa 2013/14. Alisema wameweka vipaumbele kadhaa ambavyo ni nishati vijijini, miundombinu, maji na upatikanaji wa pembejeo za kilimo. Bajeti hiyo itatanguliwa na ile ya mwelekeo wa hali ya uchumi ambayo itasomwa asubuhi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira.

BREAKING NEWS: MSANII LANGA AFARIKI DUNIA

Langa Kileo (msanii wa Hip Hop Tanzania, pichani) Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba msanii Langa amefariki dunia.. Habari zinadai  kuwa , Msanii huyu alikumbwa na Malaria kali sana hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili jana. ENDELEA KUWA NASI....

WAFANYAKAZI WA SUPERMARKET HUKO MOSHI WAANDAMANA KUPINGA RUSHWA YA NGONO WANAYOOMBWA NA BOSS WAO

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama  WAFANYAKAZI wa Supermarket ya Nakumatt, iliyopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wameulalamikia uongozi wa duka hilo kwa madai ya kuwanyanyasa na kuwaomba rushwa ya ngono. Wafanyakazi hao ambao tayari walishafikisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama walidai wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya unyanyasaji ikiwemo kuombwa rushwa ya ngono na Meneja Mkuu na na msaidizi wake. Walisema imekuwa kawaida kwa kila msichana anayefika kuomba nafasi kazi, lazima aombwe rushwa ya ngono huku wanaume wakitakiwa kinyume na maumbile:  “Kila msichana anaefika hapa kuomba nafasi ya kazi, anaombwa rushwa ya ngono ndipo apatiwe kazi huku wanaume wakiingiliwa kinyume na maumbile,” walisema. Aidha walisema sababu iliyowafanya wafikie maamuzi ya kuandamana hadi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa  kutaka msaada ni kukithiri kwa vitendo hivyo. Akizungumzia tuhuma hizo, Meneja wa Nakumatt Moshi, Alfrick Milimo alikanusha tuhuma

PICTURES 3 ZA HARUSI YA H.BABA NA FLORA MVUNGI

KALA JEREMIAH NA OMMMY DIMPOZ WATISHA BAADA YA KUJINYAKULIA TUZO TATU TATU KILA MMOJA

Mwaka huu umekuwa mwaka mzuri zaidi kimuziki kwa msanii toka rock City Mwanza Kala Jeremiaha ambae maombi yake kwa ‘Dear God’ yamesikika na amepata majibu kwa njia ya kipekee na wimbo wake ‘Dear God’ umeweza kuchukua tuzo tatu katika Kilimanjaro Music Awards 2013.     Kala Jeremiah ametumia mkuki mmoja kunasa ‘swala’ wake watatu muhimu mwaka huu, Dear God imeweza kumpa nafasi kubwa na kushinda tuzo katika kipengele cha wimbo bora wa Hip Hop. Nguvu ya wimbo huo hapana shaka ndiyo imemuwezesha pia kuondoka na tuzo ya msanii bora wa Hip Hop na Mtunzi bora wa mashairi ya Hip Hop. Kala aliweza kuwapenya wasanii wazito kama Fid Q, Joh Makini, Mwana FA, Profesa Jay na mdogo wake katika game Stamina wa Moro Town waliokutana nae katika vipengele vya Hip Hop. Wimbo huu ulitengenezwa na mtayarishaji chipukizi Dee Classic ambae pia alikuwa anawania tuzo katika kipengele cha mtayarishaji chipukizi wa Mwaka lakini hakuweza kushinda tuzo hiyo ambayo ilienda kwa Mesen Sele

Ngono kwa njia ya mdomo husababisha saratani

Dar es Salaam. Saratani imeendelea kuwa tishio hapa nchini huku hofu ikiendelea kuikumba jamii kutokana na wataalamu wa afya kushindwa kufahamu tiba halisi ya maradhi hayo hatari. Takwimu kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha ongezeko la saratani ya mdomo na koo kwa kiasi kikubwa kutoka kesi 167 mwaka 2006 hadi 277 mwaka 2012. Mkurugenzi wa Idara ya Kinga Ocean road, Julius Mwaiselage anaeleza kuwa watanzania wasipende kuiga mambo ambayo si sahihi bila kujua madhara yake kama kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo. “Saratani ya mdomo ipo, na nyingine zinasababishwa na zinaa “ anasema Dk Mwaiselage Tafiti mbalimbali zimewahi kufanyika nchini na kubaini kuwepo kwa ongezeko la saratani ya mdomo.Utafiti uliofanywa na Dk Innocent Mosha wa Kitengo cha Patholojia cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), umebaini aina za saratani 1,594, kati ya hizo 509 zikiwa ni za midomo kwa mwaka 2003 pekee. Matokeo hayo yanaonyesha kuwa kati ya saratani 509 za mdomo, sara