Skip to main content

Posts

KALA JEREMIAH NAYE ATANGAZA NIA YAKE YA KUMPIGIA KAMPENI LOWASSA....ANADAI LOWASSA NI JEMBE

Msanii wa Hip Hop na mshindi wa tuzo 3 za KTMA 2013, Kala Jeremiah amefunguka kwa kuandika waraka mrefu kuelezea jinsi anavyomkubali waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kwamba anafaa kuiongoza nchini. Usome waraka wake huo wote; Mimi Kala Jeremiah nilikuwa msanii wa kwanza Tanzania kumsema mheshimiwa Edward Lowassa kupitia wimbo wangu uitwao wimbo wa taifa baada ya mheshimiwa kukumbwa na kashfa ya ufisadi wa Richmond. Kwa kipindi kile kila mmoja wetu alihamaki sana na kuona kweli mzee wa watu ni fisadi.Kwenye wimbo huo kuna mistari nilisema, ‘mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowassa. Kwa kuwa mimi ni mzuri sana kwenye kufanya uchunguzi binafsi nilitumia muda mwingi sana kulichunguza swala hili la kashfa hii na baadae niligundua kuwa ni swala la kisiasa, na yalikuwa ni mapito ambayo mwanadamu yoyote hupewa muda wa kupitia magumu ili kupimwa imani yake kwa Mungu. Baada ya kugundua hayo mwaka jana nilitengeneza wimbo unaoitwa ...

HIZI NDIZO MECHI ZA NYUMBANI NA UGENINI ZA COASTAL UNION MZUNGUKO WA KWANZA LIGI KUU BARA.

  24/08/2013 JKT Oljoro Vs Coastal Union, Sheikh Amri Abeid Arusha. 28/08/2013 Yanga Vs Coastal Union, National Stadium Dar es Salaam. 14/09/2013 Coastal Union Vs Tanzania Prisons, Mkwakwani Tanga. 18/09/2013 Coastal Union Vs Rhino Rangers, Mkwakwani Tanga. 22/09/2013 Coastal Union Vs Ruvu Shootings, Mkwakwani Tanga. 28/09/2013 Mbeya City Vs Coastal Union, Sokoine Stadium Mbeya. 05/10/2013 Coastal Union Vs Azam FC, Mkwakwani Tanga. 13/10/2013 Ashanti United Vs Coastal Union, Azam Complex Dar es Salaam. 19/10/2013 Kagera Sugar Vs Coastal Union, Kaitaba Kagera. 23/10/2013 Coastal Union Vs Simba SC, Mkwakwani Tanga. 26/10/2013 Coastal Union Vs Mtibwa Sugar, Mkwakwani Tanga. 30/10/2013 Mgambo JKT Vs Coastal Union Mkwakwani Tanga. 02/11/2013 JKT Ruvu Vs Coastal Union, Azam Complex Dar es Salaam. COASTAL UNION 22/07/2013 DAR ES SALAAM, TANZANIA

NILIJUA TU KWAMBA WANAFIKI WATAFURAHIA MATESO YANGU" ....AGNESS MASONGANGE

"NILIJUA TU KWAMBA WANAFIKI WATAFURAHIA MATESO YANGU" ....AGNESS MASONGANGE VIDEO Queen ambaye hivi karibuni alidaiwa kukamatwa na madawa yanayosadikiwa ni ya kulevya ‘unga’ nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’, Agness Gerald ‘Masogange’ amefunguka kuwa alijua watu wengi watafurahia kilichompata kwa kumuongelea kila wakati. Akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu akiwa Sauzi, Masongange ‘alishauti’ kuwa watu wengi wanamuongelea vibaya bila kujua nini kilichompata  hivyo anaamini hata marafiki zake wa karibu wamefurahia tatizo alilopata. “Najua kabisa kuna watu wengi wamefurahia tatizo nililopata lakini watambue kuwa kila mtu anaweza kupata tatizo hivyo wapunguze kuongea sana bila kujua ni kitu gani kilichotokea juu yangu,” alisema Masogange ambaye atapanda kizimbani kwa mara ya pili mwezi ujao.

HAPPY BIRTHDAY MKALI JOJO AKILI MAPENE FBI >>>>kama mdau rafiki wa blog hii basi nasi tunakutakia siku njema kaka HAPPY BIRTHDAY!!!!!!!!!

Picha: Mkuu wa nchi katika moja ya wakati 'mzuri' kabisa aliokuwa nao leo na Rais Barack Obama.

Rais Barack Obama awasili Tanzania

Rais Barack Obama wakati wa ziara yake Afrika Kusini Rais wa Marekani Barack Obama, amewasili nchini Tanzania katika mkondo wake wa mwisho wa ziara yake barani Afrika. Ziara ya Obama inasemekana kulenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika huku kukiwa na wasiwasi kuwa Marekani inaachwa nyuma na China katika uhusiano wao na Afrika. Taarifa zinazohusiana Tanzania Obama amewasili Tanzania baada ya ziara yake ya Afrika Kusini ambako rais mstaafu Nelson Mandela anaugua. Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na familia yake pamoja na maafisa wake wa serikali na wacheza densi za kitamaduni walimkaribisha Obama na familia yake mjini Dar es Salaam. Baadhi ya wananchi wa Tanzania kupitia mitandao ya kijamii wamekosoa ziara ya Obama katika nchi yao, wakisema kuwa ziara yake imeathiri shugh...

Wanajeshi wa UN kuanza kazi Mali

Umoja wa mataifa hii leo umeanza kupeleka wanajeshi wake nchini Mali na kufikisha idadi ya wanajeshi wanaoshika doria nchini humo na ambao watakuwa chini ya UN hadi, 6,000. Idadi ya wanajeshi inatarajiwa kufika 12,640 mwisoni mwa Disemba. Taarifa zinazohusiana afrika magharibi Umoja wa Mataifa utachukua jukumu la kushika doria kutoka kwa jeshi la Ufaransa ambalo lilisimamia operesheni ya kuwafurusha wapigananji wa kiisilamu kutoka Kaskazini mwa nchi mwezi Januari. Jukumu lake la kwanza litakuwa kuhakikisha kuna usalama kabla ya uchaguzi wa urais kufanyika tarehe 28 mwezi huu. Wapiganaji wa kiisilamu walianza kufanya harakati zao baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomwondoa mamlakani rais wa taifa hilo huku wapigana...