Skip to main content

Posts

Kendrick Mabeste kusaini ‘deal’ la kutangaza maduka yenye bidhaa za watoto

Mtoto wa rapper Mabeste, Kendrick ambaye ana miezi mitatu sasa, ataanza kuonekana akitangaza maduka yanayouza bidhaa za watoto (pampers,diapers na n.k). Mabeste amesema tayari amemfungulia mwanae akaunti kwenye mitandao ya kijamii,Facebook page yake 'Kendrick Mabeste' na pia kupitia blog hii ya  www.mabestevenance.blogspot.com  ambako huko ndiko atakuwa akipromote maduka hayo. "Soon kwanzia mwezi ujao tu anaweza akaanza kupromote maduka hayo kupitia mitandao hiyo" alisema Mabeste.

AFANDE SELE ASHTUMIWA NA WASANII WENZAKE KWA LIPI?

Msanii  nguli wa muziki wa kizazi kipya Bongo,  Selemani Msindi a.k.a AFANDE SELE kutoka Mji Kasoro bahari  Morogoro,  ameshtumiwa kuwa ndio chanzo cha mvunjiko wa kundi la Watu Pori licha ya kutafutwa mara kwa mara na wasanii wenzake akiwemo  Mc Koba  kwa nia ya kulirudisha kundi katika gemu.  Akipiga Stori na  Chumba cha Sindano  kupitia kipindi cha  Kali za Bomba  cha Kituo cha redio  Bomba FM Mbeya  msanii  MC Koba  anafunguka  "Kiukweli hakuna mtu anayependa mvunjiko mimi kama mimi binafsi roho inaniuma sana kwa sababu nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kupigania uwepo wa Kundi la Watupori, lakini kushindikana kwake au ugumu wake unaletwa na Btother tunayempa nafasi, niseme nini tunampa dhamana ya kutuongoza kwa sababu Koba hawezi kuwa kiongozi, Dito hawezi kuwa kiongozi". MC Koba  akimshtumu  Afande Sele  kuwa ndo chanzo cha mvunjiko  "Afande alikuwa anatutupia sisi mzigo...

SHOW,,,,,SHOW....SHOW,,,2/11/2013 NDANI YA BARAKUDA CLUB PANGANI,

JUMAMOSI HII YA TAREHE  2/11/2013 NDANI YA  BARAKUDA ATAKUWEPO  DOGO JANJA- KWA KIINGILIO  CHA SHILINGI 3000 TU!!!!!!!!

DOWNLOAD / SIKILIZA TANGA HIP-HOP ALL STARS _ MZIKI SUPER {Audio}

Walionaswa wakiuza mkono wa mtu wafikia wane

Mwanza.  Jeshi la Polisi limemnasa mtu mwingine na kumuunganisha katika kesi ya kukutwa na kiganja cha mkono wa binadamu. Kukamatwa kwa mtu huyo, kunafanya watuhumiwa waliotiwa nguvuni mpaka sasa kufikia wanne. Taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zilizothibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi, Joseph Konyo zimesema mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuwa ni mtumishi wa Serikali Idara ya Afya, ndiye aliyefanikisha kupatikana kwa kiganja hicho. “Tumefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mwingine, kwa sasa tunafanya uchunguzi, siwezi kuthibitisha kama ni mtumishi wa Serikali au la,” alisema Konyo. Watuhumiwa wengine watatu walinaswa Novemba 28 mwaka huu eneo la Ziwani, Uwanja wa Ndege wa Mwanza wakiwa katika jitihada za kuuza mkono huo baada ya kuwekewa mtego na polisi. Konyo alisema kazi ya kuwakamata watuhumiwa wengine kuhusiana na tukio hilo inaendelea. “Kufanikiwa kumnasa mtuhumiwa huyu ni mafanikio makubwa kwa vile inaonekana ndiye anafahamu kila kitu kuhusu kiganja hicho k...

M23 yachakazwa, viongozi watimka

Msemaji wa JWTZ,Meja Eric Komba PICHA|MAKTABA  Na George Njogopa, Mwananchi Dar es Salaam.  Kuna ripoti kwamba Kundi la Waasi la M23 ambalo limekuwa likisababisha mapigano katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), limesambaratishwa katika operesheni kali iliyoendeshwa kwa ushirikiano baina ya vikosi vya nchi hiyo na vile vya Umoja wa Mataifa. Taarifa za kusambaratishwa kwa kundi hilo zimekuja siku chache baada ya kuzuka mapigano makali yaliyosababisha kuuawa kwa askari mmoja wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Rajab Ahmed Mlima aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiwa katika operesheni ya kuwaokoa raia, waliokuwa wamenasa kwenye eneo la mapigano. Wanajeshi wa Tanzania ni sehemu ya vikosi vya Umoja wa Mataifa vya Kulinda Amani huko Congo (Monusco) vyenye askari pia kutoka Afrika Kusini na Malawi, vikiwa na kazi ya kupambana na kupokonya silaha za vikundi vya waasi wanaopigana kwenye nchi hiyo. Mkuu wa Vikosi ...

DALILI ZA KUACHIWA HURU BABU SEYA NA MWANAYE: PICHA 13 HIZI HAPA WALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI JANA

Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.  Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.  Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson Nguza wakiteta jambo na wakili wao, Mabere Marando  Mahakamani.  Watu waliohudhuria mahakama hapo wakifuatilia kesi hiyo.  Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson Nguza 'Papii' wakiwa na nyuso za furaha wakati wakitoka katika Mahakama ya Rufaa baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kusikiliza maombi yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia hukumu iliyoitoa mwaka 2010.  Nyuso za ...