Skip to main content

ALIYEDHURIKA MUHIMBILI BADO MAHUTUTI INDIA

MTOTO Imrani Mwerangi (3) ambaye alipelekwa nchini India kwa matibabu baada ya kudungwa sindano iliyomsababishia mtindio wa ubongo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam, bado amelazwa katika Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) cha Hospitali ya Hyderabad, India. Taarifa iliyotolewa jana na wazazi wa mtoto huyo kutoka nchini India, ilisema hali ya Imrani bado ni mbaya. Machi mwaka huu Imrani alipelekwa nchini India na Serikali baada ya kulazwa katika ICU ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu Julai 28, 2011. “ Tangu kipindi hicho madaktari wamekuwa wakipigania kuokoa maisha yake lakini bado amelazwa katika ICU ya Hospitali ya Hyderabad,India,” ilisema taarifa hiyo. Taarifa hiyo ilisema madaktari wanaomhudumia wamesema mtoto huyo ataendelea kutegemea matibabu katika maisha yake yote. “ Asante Mungu kwa kuendelea kumpigania mtoto wetu Imrani, leo anatimiza miezi kumi tangu alazwe katika ICU za Muhimbili na hapa India,” ilisema taarifa hiyo. Taarifa hiyo ya wazazi ilisema maisha kwao yamekuwa yenye changamoto kubwa lakini jambo kubwa sasa ni kutanguliza maombi kwa Mungu. Kwa mara ya kwanza mtoto huyo alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Julai 28, 2011 kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa nyama zilizokuwa puani ambapo alipokewa na kufunguliwa jalada IP.No.A586301. Kesho yake Julai 29, 2011 mtoto huyo aliingizwa katika chumba cha upasuaji mdogo wa nyama za puani lakini kabla ya upasuaji huo alidungwa sindano ya usingizi ambayo ndiyo iliyomsababishia matatizo mtindio wa ubongo. Habari na - Raymond Kaminyoge Picha - http://sundayshomari.com/2012/02/13/muhimbili-katika-kashfa-nyingine/ Chanzo - http://www.mwananchi.co.tz

Popular posts from this blog

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2013 wilaya ya tanga mjini pekee!!!

ARAFAH ENG-MED PRIMARY SCHOOL - P2007029 AVICENNA ENG -MD PRIMARY SCHOOL - P2007051 AZIMIO PRIMARY SCHOOL - P2007032 BOMBO PRIMARY SCHOOL - P2007001 BURHANI ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007055 CHANGA ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007033 CHANGA PRIMARY SCHOOL - P2007002 CHUDA PRIMARY SCHOOL - P2007034 CHUMA PRIMARY SCHOOL - P2007003 CHUMBAGENI PRIMARY SCHOOL - P2007004 DARAJANI PRIMARY SCHOOL - P2007005 DAYSTAR ENG - MD PRIMARY SCHOOL - P2007053 DONGE PRIMARY SCHOOL - P2007035 EBEN EZER ENG- MD PR SCHOOL - P2007048 ECKERNFORDE ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007044 GOFU-JUU PRIMARY SCHOOL - P2007006 INDIAN OCEAN ENG-MED PR SCHOOL - P2007049 JABIR BIN ZAID ENG- MED PRIMARY SCHOOL - P2007052 JUHUDI PRIMARY SCHOOL - P2007036 KANA CENTRAL ENGMED PRIMARY SCHOOL - P2007054 KANA PRIMARY SCHOOL - P2007007 KISOSORA PRIMARY SCHOOL - P2007008 KOMBEZI PRIMARY SCHOOL - P2007009 KWAKAEZA PRIMARY SCHOOL - P2007026 KWANJEKA PRIMARY SCHOOL - P2007010 MABAW...

Coastal ipo tayari kuanza ligi kuu, yashinda 3-0 ikiwa kambini Moshi.

Wachezaji wa Coastal Union wakifanya mazoezi mepesi muda mfupi kabla ya kukabiliana na Machava FC kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi, anayeonekana pichani mwenye jezi namba 17 ni haruna Moshi 'Boban'. Mtokeo ya mechi hiyo ni ushindi wa 3-0 kwa Wagosi. Mazoezi yamekolea, uwanja wa Ushirika Moshi. Uhuru Suleiman amesifiwa na kocha kuwa ni kiungo mwenye kasi nyingi na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. Mshambuliaji anayetumia mguu wa kushoto kutoka Uganda, Yayo Lutimba Kato amefunga bao lake la kwanza tangu kujiunga na Coastal Union ambayo imeweka kambi mjini Moshi tangu jana. Kato ambaye ametoka URA inayoshiriki ligi kuu nchini Uganda, alipatia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Machava FC kwenye uwanja wa Ushirika mjini humo, bao hilo alilifunga kwa ufundi mkubwa katika kipindi cha pili baada ya kupokea pasi murua na kupiga shuti kali akiwa nje ya 18. Akitoa taarifa kutoka Moshi, mwenyekiti wa Wagosi Hemed Hilal ‘Aurora’ amesema “Katika dakika za lal...

Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Dk John Magufuli   Dar es Salaam.   Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge. Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012. Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni. “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. T...