Skip to main content

Kassim Mganga na Tip Top connection Bado Damu Damu

Pamoja na kwamba picha mitaani bado inaonekana mwimbaji Kassim Mganga hayuko kwenye uhusiano mzuri hata wa kirafiki na kundi lake la zamani la Tip Top Connection kwa sababu hajawahi kuonekana nao pamoja kwenye showz, Night Clubs hata kwenye mazingira mengine kama wanavyofanya wengine waliojiondoa kwenye kundi hilo, nimefurahi kuona Kassim Mganga amekubali kufungua kinywa chake kuondoa hiyo picha mbovu kwenye fikra za watu. Kassim amesema “huu ni mwaka wa pili toka nimetoka Tip Top na kuingia Manzabay, hakuna tofauti yeyote mi naona bado wale ni ndugu zangu tumefanya vitu vingi na tumetunziana siri nyingi sana, Madee tunawasiliana kila siku na tunakutana hata Deso pia” Kwenye sentensi nyingine Kassim amesema “Babtale pia napiga nae sana mazoezi kila asubuhi Mwembe Chai pale, unajua watu walio nje kuna vitu vingine hawavioni lakini wao wanavijengea picha kwa hiyo inabidi waelewe hivyo kwamba Tip Top bado ni familia yangu, naweza kumfata Meneja Tale hata leo nikamuomba msaada wowote na naamini hawezi kukataa kwa sababu binadamu nyuso zimeumbwa na haya… tumefanya vingi”

Popular posts from this blog

Goog music from tng jojo yatakwisha hii apa

DownLoad Na Sikiliza Joint Mpya Ya Squizer Ft Belle 9 - Mtemi Pesa

Tugumiane tanga flevani 10_00AM-12_00PM 106.1Mhz @mwambaofm_ fm radio tanga