Siku chache kabla ya Mother’s Day Alicia Keys alihojiwa kwenye talk show iitwayo
‘The Conversation’ inayotayarishwa na Demi
Moore na mtangazaji akiwa Amanda de Cadenet.
Waliongea mengi kuhusu maisha yake
kama mama, umbo lake baada ya kuzaa, kunyonyesha na sababu iliyomfanya amuite
mwanae Misri.
“Well, Misri ilikuwa safari muhimu katika maisha yangu”
Alisema Alicia. Ilikuja katika pointi ambayo nilikuwa nimefanya kazi mno bila
kupumzika na sikuwa na idea yoyote kuhusu kuchukua likizo ya kweli na ilikuja
katika muda huo ambao niliihitaji.
Hivyo nilipoenda, ilinipa nguvu sana, ikanifungua
macho, safari ya kihistoria, yenye nguvu na experience ya pekee iliyonifanya
niipende Misri.
Alicia, Demi na Amanda |
Hivyo ulipokuja wakati wa
kumpa jina mtoto wetu, nililipenda, wote tulilipenda na tuliamua miezi kadhaa
hata kabla hajazaliwa”
Egypt na baba yake Swizz Beatz |
Kuhusu kwanini alienda peke yake nchini Misri alisema “Muda
huo nilihitaji sana kwenda mbali kiasi
ambacho nilitaka kuwa peke yangu. Nadhani ni kitu muhimu kwasababu ukienda
sehemu na watu lazima utakuwa ukifikiria kama wanafurahia ama wanapenda chakula unachopenda ama wanaufurahia mgahawa huu?
Nilikuwa nikisoma kitabu changu kwenye mgahawa na utaona mwanaume
anakuja kwangu nakuuliza “Kuna mtu unangoja? Na mimi najibu kama “ Hapana, tuko
hapa”. Ilikuwa safari yenye kusaidia sana”