Skip to main content

WANAFUNZI CHUO KIKUU WABAKWA, WALAWITIWA

WANACHUO wa Chuo Kikuu cha St John mjini Dodoma, leo wamegoma kuingia madarasani hadi wawasilishe malalamiko yao kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Zelothe Stephen kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kupigwa nondo, kuibiwa kadi za benki, kompyuta za mkononi, kulawitiwa na kubakwa. Hali hiyo ilisababisha wanafunzi kukusanyika huku wakiwa wamebeba mabango mbalimbali ambayo yalikuwa yakisomeka, ‘Tunaomba ulinzi ili kubaka na kulawitiwa kukomeshwe’, ‘Ulinzi ni haki yetu ya msingi polisi Mko wapi? Tumechoka kuwa wajinga katika jamii yetu na Ulinzi Shirikishi stop crime.’ Baadhi ya wanafunzi hao walilaani vitendo vya wenzao kubakwa na kulawitiwa na kudai kuwa katika siku za hivi karibuni, mwanafunzi wa kiume ambaye anasoma mwaka mwaka wa pili aliibiwa na kisha kulawitiwa hali iliyolazimu alazwe hospitali. “Kesi kadhaa zimepelekwa polisi lakini hakuna chochote kinachofanyika,” alisikika mwanachuo moja akizungumza kwa jazba. Walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na wakati mgumu kutokana na kuibiwa vifaa muhimu zikiwemo kompyuta za mkononi hali ambayo hulazimika kuishi kwa hofu. “Juzi wenzetu wamevamiwa usiku na kuporwa simu tano na laptop tatu sasa tunaona maisha yanakuwa magumu sana kwetu kwani usalama wetu sasa ni mdogo,” alisema mmoja wa wanafunzi hao. Walisema hali ni mbaya zaidi kwa wanafunzi ambao wanaishi nje ya chuo kwani hata kujisomea nyakati za jioni kumekuwa kwa mashaka kutokana na kuogopa kuvamiwa na vibaka. Walisema baadhi ya wenzao wanaanza mitihani Juni, hali ambayo inawatia hofu kama wimbi hilo la kuvamiwa na vibaka linaweza hata kupunguza ufaulu mioungoni mwao. Pia walitaja sababu kadhaa ambazo zinadhaniwa kuwa zinasababisha matukio hayo ni chuo hicho kukosa uzio na hivyo kufanya mwingiliano wa watu na wanachuo kuingia chuoni bila kuwa na utaratibu. Walisema kundi lisilojulikana limekuwa na kawaida ya kuvamia sehemu ambazo wanachuo wanakaa na baada ya kuiba vitu mbalimbali humalizia kwa kubaka wasichana au kwa kulawiti kama ni mvulana. Hata hivyo, juhudi za wanafunzi wao kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma hazikufanikiwa baada ya kuelezwa kuwa alikuwa na majukumu mengine ya kikazi, na kutuma mwakilishi wake ambaye ni Mkuu wa Polisi Wilaya, Dominic Mlei na Mkuu Mpya wa Polisi wa Wilaya atakayeanza kazi hivi karibuni, Thadeus Malingumu. Kwa upande wake, OCD Mlei alisema ulinzi unaanza rasmi leo, kufanya doria maeneo yanayozunguka chuo hicho na maeneo jirani, pia chuo kijenge hosteli za kutosha na kwa kila hosteli za nje na nyumba walizopanga wanafunzi zitakaguliwa kesho na mapungufu ya kiusalama kwenye makazi hayo yataainishwa na wamiliki wataitwa na hosteli zote zitatakiwa kuwa na mageti na ulinzi wa makazi hayo kuboreshwa. Pia alitaka kuundwa kwa mara moja kwa vikundi vya ulinzi shirikishi. Hata hivyo, mtumishi wa Chuo hicho, Mzee Muganda alishauri Kituo Kidogo cha Polisi kijengwe Kikuyu na bidii ya doria iongezwe Habari na - Sifa Lubasi, Dodoma Chanzo - http://www.habarileo.co.tz You might also like:

Popular posts from this blog

MAJINA YA WASHIRIKI NA WA WEZESHAJI WA FILM YA HOUSE GIRL!

CAST SELEMANI MOHAMED / BUNTO ANDREW / C-O YORAM MWETA / MGANGA MWANTUMU / MKE WA C-O JOHN / MCHUNGAJI BI FURURATU / JINI WAOMBOLEZAJI SAUMU HUSENI HASHIMU BABA RASTA MAN YOHANNA TAMILWAI SAIDI MWALUBADU SEMY STIR SELEMANI MOHAMEDI  AND ANDREW C-O LOCATION ATHUMANI HAMADI MAKE UP MWASHAMBA RAMADHANI BEDUI DEREVA DAUDI SPOONSER SAIDI SHABANI AND THE FRESH2012 GLOB SOUND PRODUCER J-B LIGHT YOHANNA TAMILWAI THENK YOU THE FRESH ENERTAINMENT AND THE FRESH2012 BLOG CONTACTS 0653785027 +255714091786 ZAIDI TEMBELEA www.the-fresh.blogspot.com ADRESS Thefresh@ymail.com AU Saidshabani60@gmai.com

Sababu ya Alicia Keys kumuita mwanae Misri (Egypt)

Siku chache kabla ya Mother’s Day Alicia Keys alihojiwa kwenye talk show iitwayo  ‘The Conversation’ inayotayarishwa na Demi Moore na mtangazaji akiwa Amanda de Cadenet. Waliongea mengi kuhusu maisha yake kama mama, umbo lake baada ya kuzaa, kunyonyesha na sababu iliyomfanya amuite mwanae Misri. “Well, Misri ilikuwa safari muhimu katika maisha yangu” Alisema Alicia. Ilikuja katika pointi ambayo nilikuwa nimefanya kazi mno bila kupumzika na sikuwa na idea yoyote kuhusu kuchukua likizo ya kweli na ilikuja katika muda huo ambao niliihitaji.  Hivyo nilipoenda, ilinipa nguvu sana, ikanifungua macho, safari ya kihistoria, yenye nguvu na experience ya pekee iliyonifanya niipende Misri.  Alicia, Demi na Amanda Hivyo  ulipokuja wakati wa kumpa jina mtoto wetu, nililipenda, wote tulilipenda na tuliamua miezi kadhaa hata kabla hajazaliwa” Egypt na baba yake Swizz Beatz Kuhusu kwanini alienda peke yake nchini Misri alisema “Muda huo nilihitaji sana kwenda

Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Dk John Magufuli   Dar es Salaam.   Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge. Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012. Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni. “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba