Skip to main content

YOUNG D: NI KWELI NILIPATA AJALI WAKATI NATOKA KWENYE SHOW YA SIMBA.

Rapper Young Dar es salaam amekiri kwamba alipata ajali usiku wa jumapili wakati akitoka kufanya show ya club ya Simba kusherehekea ubingwa wake wa ligi kuu Dar Live Mbagala Dar es salaam. D amesema hiyo ndio sababu kubwa iliyomfanya hata ashindwe kuperform kwenye show ya Rachel wa THT Maisha Club. Chanzo cha ajali ni dereva Taxi akiwa kwenye spidi kubwa kujaribu kumkwepa mvuka barabara hivyo ikabidi afanye maamuzi ya ghafla na kugonga nguzo na kuingia mtaroni kitendo ambacho kilimfanya Young D apoteze fahamu hapohapo kwenye eneo la ajali, alipelekwa hospitali kuanzia hiyo saa tano usiku na kuruhusiwa kutoka saa nane usiku huo huo. Hata hivyo mbali na hiyo ajali, D amekubali kwamba amelipwa zaidi ya shilingi milioni moja kwa kuwa msanii pekee wa bongofleva kualikwa kwenye show hiyo ya Simba ambayo mashabiki wake waliutumia wimbo wake wa dada anaolewa na kuuita Yanga anaolewa baada ya kuishinda Yanga kwenye fainali, hiyo ndio sababu kubwa iliyofanya D aalikwe kuperform.

Popular posts from this blog

Goog music from tng jojo yatakwisha hii apa

DownLoad Na Sikiliza Joint Mpya Ya Squizer Ft Belle 9 - Mtemi Pesa

Tugumiane tanga flevani 10_00AM-12_00PM 106.1Mhz @mwambaofm_ fm radio tanga