Huenda wagonjwa wa Ukimwi
wakanufaika na dawa mpya ambayo itawawezesha kutumia tembe moja kwa
siku. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya nchini Marekani.Jarida la
Afya Lancet limesema tembe hiyo inajumlisha dawa zote nne
zinazokabiliana na makali ya ukimwi na kwamba ni salama.Utafiti unasema
hii itawarahisishia wagonjwa katika
kuhakikisha wanafuata maagizo ya madaktari wao.
Ukimwi hauna tiba lakini watafiti wameweza kutoa dawa za kukabiliana na maradhi nyemela.
Watafiti pamoja na kampuni za dawa wamechanganya dawa nne na kutengeneza tembe moja ili kurahisisha utumizi wa dawa hiyo miongoni mwa wagonjwa.
Tembe inayofanyiwa majaribio na ambayo imechanganywa dawa nne inauwezo wa kudhibiti virusi vya HIV kuongezeka mwilini.
Paul Sax mtafiti mkuum katika Hospitali ya Wanawake ya Brigham huko Boston,Massachussetts ambaye pia ni mwanazuo wa ziada wa taasisi ya afya ya Harvard ameelezea umuhimu wa tembe hii kwa kuimarisha afya ya wagonjwa.
Dk. Sax ameongoza utafiti huu ambapo pia wamefanyia majaribio tembe hii kwa wagonjwa 700 na kusema inafanya kazi, japo kulitokea matatizo ya figo miongoni mwa waliotumia.
Licha ya mafanikio ya sasa watafiti wanasema raia wengi hawafahamu hali zao ambapo wameendelea kuishi na maambukizi bila kujua.