Jumuiya
na Taasisi za Kiislamu imepanga kwenda mahakamani kuzuia zoezi la sensa
na kupinga kauli iliyotolewa na Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislamu
(Bakwata), Mufti Issa Shaban Simba, kwamba Waislamu wamekubali
kuhesabiwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa
jumuiya hizo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema kauli ya Mufti Simba,
inaashiria kwamba Bakwata limekiuka makubaliano yaliyofikiwa mjini
Dodoma na jumuiya zote za waumini wa dini hiyo.
Alisema kauli hiyo haitakuwa na athari kubwa kwa msimamo wa Waislamu wemgi ambao hawatashiriki zoezi la sensa.
"Waislamu
tumepanga tarehe hiyo ya sensa kufanya maandamano ya amani nchi nzima
kwani sensa inayokusudiwa haitakuwa na matokeo sahihi kwakuwa asilimia
80 ya Waislamu ambao ni zaidi ya nusu ya Watanzania hawatahesabiwa,"
alisema Shekh Ponda.
Hivi
karibuni Mufti Simba, alitoa msimamo wa Bakwata, akiwataka Waislamu
wote nchini kushiriki Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 26,
mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE