Skip to main content

KIONGOZI WA MGOMO WA MADAKTARI APIGWA VIBAYA ONA PICHA

http://3.bp.blogspot.com/-wdBDq5F7ZAE/T-r7qMnK0fI/AAAAAAAAA0Q/gpRIlkEqNvw/s1600/dr.jpgDkt. Ulimboka:Dkt. Helen Kijo-Bisimba wa LHRC akinukuliwa katika EA Redio amekariri maelezo ya Dkt. Ulimboka ambayo pia yamesikika yakitamkwa na mwenyewe (Dkt. Ulimboka Steven), kupitia kituo cha redio cha CloudsFM, kwamba walikuja watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Watu hao walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na namba na kuanza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa usoni, kamba mikononi na miguuni kisha wakampiga huku wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu na kama wangekuwa na sindano ya sumu wangemmaliza kabisa. ---
UPDATE:
Dkt. Ulimboka amefikishwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma. Hali yake ni mbaya ila "stable".
------

Baadhi ya watu wa shirika la Tanzania Legal Human Rights Center (LHRC) walifanya juhudi za kumtafuta kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Ulimboka Steven aliyekamatawa (? tekwa) jana usiku.

Taarifa iliyotoka kwa mmoja wa wanaharakati hao inasema, walifanikiwa kumpata Dkt. Ulimboka kaitka eneo la Mwabepande, Dar es Salaam ) akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hajitambui (unconscious) na asiyeweza kuzungumza.

Taarifa hiyo inaongez akuwa, Dkt. Ulimboka alikuwa amepigwa vibaya sana katika sehemu mbalimbali za mwili wake na anahitaji matibabu ya haraka.

Juhudi zinafanywa kumpatia msaada unaohitajika Dkt. Ulimboka Steven.

Popular posts from this blog

Goog music from tng jojo yatakwisha hii apa

DownLoad Na Sikiliza Joint Mpya Ya Squizer Ft Belle 9 - Mtemi Pesa

MAJINA YA WASHIRIKI NA WA WEZESHAJI WA FILM YA HOUSE GIRL!

CAST SELEMANI MOHAMED / BUNTO ANDREW / C-O YORAM MWETA / MGANGA MWANTUMU / MKE WA C-O JOHN / MCHUNGAJI BI FURURATU / JINI WAOMBOLEZAJI SAUMU HUSENI HASHIMU BABA RASTA MAN YOHANNA TAMILWAI SAIDI MWALUBADU SEMY STIR SELEMANI MOHAMEDI  AND ANDREW C-O LOCATION ATHUMANI HAMADI MAKE UP MWASHAMBA RAMADHANI BEDUI DEREVA DAUDI SPOONSER SAIDI SHABANI AND THE FRESH2012 GLOB SOUND PRODUCER J-B LIGHT YOHANNA TAMILWAI THENK YOU THE FRESH ENERTAINMENT AND THE FRESH2012 BLOG CONTACTS 0653785027 +255714091786 ZAIDI TEMBELEA www.the-fresh.blogspot.com ADRESS Thefresh@ymail.com AU Saidshabani60@gmai.com