Skip to main content

ULIMBOKA ANA SIRI NZITO, ASEMA ATAANIKA KILA KITU BAADAYE, ASEMA ACHWE APUMZIKE, MKUU WA JOPO LA MADAKTARI WANAOMTIBU ASEMA ALING'OLEWA KUCHA, MENO MAWILI NA KUPATA MTIKISIKO WA UBONGO

[Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk Steven Ulimboka, akiwa amelazwa katika Chumba maalum cha wagonjwa mahututi (ICU)akiendelea na matibabu katika Taasisi ya mifupa (MOI)jijini Dar es Salaam jana.] Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk Steven Ulimboka, akiwa amelazwa katika Chumba maalum cha wagonjwa mahututi (ICU)akiendelea na matibabu katika Taasisi ya mifupa (MOI)jijini Dar es Salaam jana. ASEMA ATAANIKA KILA KITU BAADAYE, ASEMA ACHWE APUMZIKE, MKUU WA JOPO LA MADAKTARI WANAOMTIBU ASEMA ALING'OLEWA KUCHA, MENO MAWILI NA KUPATA MTIKISIKO WA UBONGO Geofrey Nyang'oro MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari aliyetekwa nyara na kuumizwa vibaya usiku wa kumkia juzi, kisha kutupwa Msitu wa Pande, Dk Steven Ulimboka amesema atazungumza kwa kina yote yaliyomsibu baadaye na kuomba sasa aachwe auguze maumivu makali yanayomkabili. Dk Ulimboka aliokotwa na wasamaria wema juzi asubuhi katika Msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, baada ya kutekwa nyara na watu waliokuwa na silaha akiwa katika Viwanja vya Klabu ya Leaders, Kinondoni. Jana, Dk Ulimboka ambaye amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili huku hali yake ikiwa haijatengemaa vyema, alitoa kauli akisema ingawa ana maumivu makali anaendelea vizuri ikilinganishwa na siku ya kwanza. Dk Ulimboka alitoa kauli hiyo baada ya kutakiwa aeleze mkasa huo uliomfika wa kukamatwa, kuteswa na kutupwa msituni. Hata hivyo, hadi sasa wingu zito la nani alimteka na watekaji walitaka kujua nini kutoka kwa kiongozi huyo wa madaktari, bado limetanda. Siri nzito Akisimulia mkasa huo kupitia Kituo cha Redio cha Clouds FM, Dk Ulimboka alisema, akiwa katika klabu hiyo ya Leaders alipigiwa simu na rafiki yake ambaye alikuwa atokee Tandika na baada ya kumsubiri ndipo alipofika kwenye klabu hiyo, lakini, alianza kujisikia vibaya tofauti na siku nyingine na kuongeza; "Yaani sikuwa na amani." Alisema, "Mara, katikati ya maongezi tukaona mtu anaongea na simu. Ghafla tukiwa tunasema tuagane, wakaja watu kama watano hivi na bunduki, wakasema wewe na yule bwana mko free (huru), tunakuchukua wewe (Dk Ulimboka)," alieleza na kuongeza: "Sijakaa sawa, nikaona nimeshaburutwa nikaanguka kwenye lami, wakaniinua na kuniingiza kwenye gari nyeusi, lakini halikuwa na namba." Hata hivyo, jana Dk Ulimboka hakuonana na mwandishi wa habari hii, badala yake alirekodiwa, na Mwananchi kupata sauti yake akijibu swali kuhusu hali yake na tukio hilo, baada ya uongozi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) kuzuia watu kumwona. Daktari huyo wa magonjwa ya binadamu, amelazwa katika chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU). "Kidogo najisikia nafuu ikilinganishwa na nilivyokuja ingawaje, bado nina maumivu makali. Kwa hivyo, ingependeza niendelee na mapumziko na mtu yeyote anayetaka kuniona pengine hilo jambo lisifanyike sasa. Hivi sasa ni vizuri nipumzike," ilisikika sauti hiyo ya Dk Ulimboka. Lakini, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wodini alikolazwa Dk Ulimboka, kuna ulinzi mkali wa madaktari na hairuhusiwi watu kumwona kiholela siyo tu kwa sababu za kutaka aachwe apumzike, bali pia kutowaamini watu ovyo. Madaktari wanaolinda eneo hilo walisikika jana wakisema, “Huyu tunamlinda wenyewe na haiwezekani mtu asiyefahamika kuingia humu ndani, na hilo tutahakikisha sisi wenyewe,”alisikika akisema mmoja wa madaktari hao. Kiongozi jopo la madaktari Katika hatua nyingine, kiongozi wa jopo la madaktari wanaomuhudumia Dk Ulimboka, Profesa Joseph Kahamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa Dk Ulimboka ana majeraha mwili mzima. “Ingawa kwa sasa anaendelea vizuri, Dk Ulimboka ameumia sana, kwani mwili wake mzima una majeraha kutokana na kupigwa na watekaji hao,”alisema Profesa Kahamba na kuongeza: “Aliumia mbavuni,kifuani, miguuni, mikononi ambako aling’olewa baadhi ya kucha za vidole na kichwani na kinywani, ambako aling’olewa meno mawili,”alisema. Alifafanua kwamba, kutokana na maumivu hayo ya kichwa, Dk Ulimboka alipata tatizo la mtikisiko wa ubongo, lakini akasisitiza kuwa madaktari bingwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha yake. Uongozi wa Moi watoa neno Uongozi wa Taasisi ya Mifupa (Moi) umeeleza kuwa hali yake inaendelea vizuri ingawa bado amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi cha taasisi hiyo. Msemaji wa Moi, Almas Jumaa aliwaambia waandishi wa habari kuwa licha ya hali yake kuendelea vizuri, lakini haingewezekana kwa waandishi wa habari kuingia ndani ya chumba alikolazwa na kumwona Dk Ulimboka. “Mgonjwa anaendelea vizuri ukilinganisha na jana (juzi), anaongea, anawatambua watu wanaokwenda kumwona, lakini utaratibu wa kwenda kumwona kwa ninyi imeshindikana kwa sababu yupo (ICU) ni chumba chenye utaratibu wake,”alisema Jumaa. Jumaa aliongeza kwamba ili mtu aweze kuingia wodini analazimika kuvaa vazi maalumu na mavazi yaliyopo, yasingetosha, lakini pia wapo watu wanaoendelea kumpatia huduma ya matibabu. Tamko la Jumuiya ya Madaktari Wakati hali ya Dk Ulimboka ikiwa hivyo, madaktari wameipinga tume ya uchunguzi iliyoundwa na Jeshi la Polisi kuchunguza suala hilo, wakidai mazingira ya tukio hayaliondoi jeshi hilo kuhusika. Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitage aliwaambia waandishi wa habari kuwa wangependa kuundwa kwa tume huru itakayofanya kazi ya kuchunguza tukio hilo na kutoa taarifa kwa umma. “Madaktari kwa ujumla wetu tunalaani tukio la kutekwa nyara,kupigwa na kutupwa katika Msitu wa Pande, lakini pia hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la Polisi kwa sababu mazingira ya tukio hayaondoi kuhusika ama kutohusika kwa jeshi hilo,”alisema Dk Chitage. Chitage alitoa msimamo wa madaktari kuwa ni kuendelea na mgomo, huku akionya Serikali kuacha vitendo vya kuwatisha, kwa madai kuwa vitendo hivyo haviwezi kuwa suluhu ya mgogoro kati ya pande hizo mbili. “Kumekuwa na vitisho kwa madaktari katika maeneo mbalimbali nchini, hususan Dodoma, Mbeya, Arusha na Mwanza. Tunaionya Serikali kuacha mara moja na itambue kuwa mgogoro huo hauwezi kumalizwa kwa namna nyingine yoyote bali ni kwa Serikali kutekeleza madai ya madaktari,”alisema Chitega na kuongeza: “Sisi madaktari kwa umoja wetu, tumechoka kushuhudia Watanzania wakipoteza maisha kwa magonjwa tunayoweza kuyatibu, kufanya kazi katika mazingira magumu huku kukiwa hakuna mipango ya kuboresha mazingira ya kazi, kukosekana kwa dawa na vifaa tiba.” Mgomo huo wa madaktari leo unaingia siku ya saba tangu ulipotangazwa na mwenyekiti huyo kuwa, ungeanza rasmi Jumamosi iliyopita.

Popular posts from this blog

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2013 wilaya ya tanga mjini pekee!!!

ARAFAH ENG-MED PRIMARY SCHOOL - P2007029 AVICENNA ENG -MD PRIMARY SCHOOL - P2007051 AZIMIO PRIMARY SCHOOL - P2007032 BOMBO PRIMARY SCHOOL - P2007001 BURHANI ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007055 CHANGA ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007033 CHANGA PRIMARY SCHOOL - P2007002 CHUDA PRIMARY SCHOOL - P2007034 CHUMA PRIMARY SCHOOL - P2007003 CHUMBAGENI PRIMARY SCHOOL - P2007004 DARAJANI PRIMARY SCHOOL - P2007005 DAYSTAR ENG - MD PRIMARY SCHOOL - P2007053 DONGE PRIMARY SCHOOL - P2007035 EBEN EZER ENG- MD PR SCHOOL - P2007048 ECKERNFORDE ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007044 GOFU-JUU PRIMARY SCHOOL - P2007006 INDIAN OCEAN ENG-MED PR SCHOOL - P2007049 JABIR BIN ZAID ENG- MED PRIMARY SCHOOL - P2007052 JUHUDI PRIMARY SCHOOL - P2007036 KANA CENTRAL ENGMED PRIMARY SCHOOL - P2007054 KANA PRIMARY SCHOOL - P2007007 KISOSORA PRIMARY SCHOOL - P2007008 KOMBEZI PRIMARY SCHOOL - P2007009 KWAKAEZA PRIMARY SCHOOL - P2007026 KWANJEKA PRIMARY SCHOOL - P2007010 MABAW...

Coastal ipo tayari kuanza ligi kuu, yashinda 3-0 ikiwa kambini Moshi.

Wachezaji wa Coastal Union wakifanya mazoezi mepesi muda mfupi kabla ya kukabiliana na Machava FC kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi, anayeonekana pichani mwenye jezi namba 17 ni haruna Moshi 'Boban'. Mtokeo ya mechi hiyo ni ushindi wa 3-0 kwa Wagosi. Mazoezi yamekolea, uwanja wa Ushirika Moshi. Uhuru Suleiman amesifiwa na kocha kuwa ni kiungo mwenye kasi nyingi na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. Mshambuliaji anayetumia mguu wa kushoto kutoka Uganda, Yayo Lutimba Kato amefunga bao lake la kwanza tangu kujiunga na Coastal Union ambayo imeweka kambi mjini Moshi tangu jana. Kato ambaye ametoka URA inayoshiriki ligi kuu nchini Uganda, alipatia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Machava FC kwenye uwanja wa Ushirika mjini humo, bao hilo alilifunga kwa ufundi mkubwa katika kipindi cha pili baada ya kupokea pasi murua na kupiga shuti kali akiwa nje ya 18. Akitoa taarifa kutoka Moshi, mwenyekiti wa Wagosi Hemed Hilal ‘Aurora’ amesema “Katika dakika za lal...

Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Dk John Magufuli   Dar es Salaam.   Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge. Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012. Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni. “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. T...