Skip to main content

Utafiti wabaini: Wanawake wafupi hatarini kwa vifo vya uzazi

Baadhi ya wanawake wakiwa kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Temeke,wakisubiri kujifungua. Picha na Emmanuel Herman Na Maimuna Kubegeya SIKU zote mwanamke awapo mjamzito huwa na matarajio makubwa ya kukipata kiumbe chake ambacho huwa ni faraja ya pekee maishani mwake. Lakini inapotokea mwanamke huyo akashindwa kukipakata kiumbe alichokisubiri kwa hamu kwa muda mrefu wa miezi tisa, huwa ni msiba … majuto na upweke wa aina yake. Hiyo ndiyo hali iwakumbayo wanawake wengi wanaopoteza watoto wao wakati wakujifungua . Zipo sababu chekwa zisababishazo vifo vya watoto wachanga na moja ya sababu hizo ni maumbile ya wanawake wenyewe. Wengine si tu hupoteza vichanga bali hata maisha yao wenyewe huenda yakawekwa rehani katika kipindi hiki. Kwa mujibu wa Hadija Kimwaga, Ofisa Muuguzi na Mkunga kutoka Hospitali ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, wanawake wafupi wako katika hatari ya kupata matatizo wakati wa kujifungua ingawaje si kila mwanamke wa aina hiyo kwani wapo wengine ambao hujifungua kwa njia ya kawaida. “Baadhi ya wanawake walio na urefu ulio chini ya sentimita 150 huwa na nyonga ndogo. Hivyo, inashauriwa mara watakapokuwa na ujauzito kwenda kwanye vituo vikubwa vya afya ama hospitali kubwa kwani huko wanaweza kupata huduma sahihi”, anaeleza. Anaongeza kuwa na hii ni miongoni mwa sababu zinazowafanya wataalamu wa afya kuwashauri kufika kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya mtoto na afya zao kwa ujumla katika kipindi hicho. Kwa wale wanaopata tatizo mara nyingi njia pekee ya kuwanusuru imekuwa ni upasuaji. Hivyo, ikithibitika kuwa nyonga za mwanamke husika hajitanuki kwa kiwango kinachohitajika basi huduma hiyo hutolewa kwa lengo la kunusuru maisha ya mama na mtoto.Lakini hatari kubwa hutokea pale wanapocheleweshwa anasisitiza. Pamoja na kuwa suala la kimo mara nyingi hutegemea na hali ya kijenetiki, wakati mwingine ufupi husababishwa na ukosefu wa lishe bora wakati wa utotoni. Mmoja wa wanawake waliofikwa na msiba wa kupoteza kichanga ni Margreth Mwenda. Magreth anasema: “NI siku ambayo siwezi kuisahau maishani kwangu. Ninakumbuka kuwa ilikuwa mwezi wa Januari mwaka 2000, nikiwa kwenye moja ya kitanda katika wodi ya wazazi, kwenye Hospitali ya St. Francis Wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro”, anasemaMwenda. Kwa wakati huo, kitu pekee alichokuwa akitarajia ni kumkumbatia mwanawe ambaye alikuwa akitarajia kujifungua muda mfupi ujao. “Huwezi kuamini, mtoto ambaye nilikuwa namsubiri kwa hamu, tena nikimsikia anavyonipiga mateke tumboni, alifariki muda mfupi kabla ya kujifungua. Alifia njiani,” anasema mwanamke huyu mwanye umri wa makamo. “Kwani nilishindwa kujifungua kwa njia ya kawaida kutokana na nyonga zangu kushindwa kutanuka. Jambo hilo lilisababisha mtoto kushindwa kushuka kwenye njia yake ya kawaida’’, anafafanua Mwenda. “Pamoja na uchungu nilionao, lakini naweza kueleza kuwa sababu moja wapo iliyochangia kumpoteza mwanangu, ni kuchelewa kufika hospitalini na hivyo kupoteza damu nyingi sana kabla ya kujifungua”, anasema kwa huzuni mama huyo. Dk. Hassan Saad kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids)anasema kimo kifupi mara nyingi husababisha matatizo wakati wa kujifungua kutokana tatizo la kushindwa kutanuka kwa nyonga Anasema tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa mara nyingi lishe duni wakati wa utotoni hupelekea kudumaa. Jambo linalochangia hupelekea mtoto husika kuwa mfupi. Baadhi ya mambo yanayochangia hali hiyo ni ukosefu wa vitamini D na ukosefu wa mwanga wa jua wa kutosha unaosababisha kupata matege na magonjwa mengine ya mifupa ikiwamo hilo la kutokuongezeka kwa nyonga. “Lishe bora ina nafasi kubwa ya kuongeza kimo na pia kuongeza kimo cha mji wa uzazi” alisema. Imebainishwa kuwa wanawake walio katika tatizo hili kwa sasa, huwa wameathiriwa wakiwa wadogo. Dk Maggie Blott, mshauri wa masuala yanayohusu magonjwa ya wanawake, kutoka Uingereza ameandika kwenye mtandao wake kuwa baadhi ya wanawake walio na kimo kifupi wana nyonga ndogo, ambazo hushindwa kushindwa kutanuka wakati wa kujifungua na hivyo kusababisha madaktari kuchukua uamuzi wa kuwafanyia upasuaji . “Mara nyingi ili kuokoa maisha ya mama na mtoto, tumekuwa tukitumia njia ya upasuaji”, anaandika daktari huyo. “ Katika nchi zinazoendelea umasikini na ukosefu wa lishe bora kwa watoto unasababisha watoto hao kukua , wakati mifupa ya wasichana inakuwa haijakomaa. Hali hii ya kudumaa husababisha matatizo wakati wa kujifungua na pia fistula”, anasisitiza. Tatizo hili limekuwa ni la kawaida kwa nchi masikini na hasa kwa wanawake na wasichana walio na hali ya chini kimaisha. Vifo vya wajawazito mara nyingi vinasababishwa na matatizo wakati wa kujifungua na vimekuwa vikiongezeka zaidi katika nchi zinazoendelea hasa kutokana na huduma duni za afya zinazotolewa hususani na wakunga jadi. Wakati mwingine mzazi hupoteza damu nyingi sana kabla ya kujifungua, kutokana na mtoto kukandamiza njia ya uzazi na kusababisha majeraha yanayosababisha kuvuja kwa damu. Jambo linalosababisha mwanamke husika kufanyiwa upasuaji. Ulaji wa chakula bora tangu kipindi cha mimba na baada ya kuzaliwa, ni njia mojawapo ya kuepuka tatizo hili. Kwani ikiwa mama atakula chakula bora wakati wa ujauzito, ni wazi kuwa atajifungua mtoto mwenye afya bora. Mtoto huyo pia akipata chakula bora wakati wa makuzi yake, ni wazi kuwa atakuwa katika hali bora kiafya. Hali hiyo huchangia kuondoa udumavu, unaopelekea hatari wakati wa kujifungua. Lakini, kwa wanawake kama Magreth Mwenda hawana jinsi ya kurekebisha maumbile yao, isipokuwa ni kuhakikisha wanajifungua sehemu salama yenye madaktari wenye ujuzi wa kutosha. Pia, kuwapa chakula bora watoto wao pindi watakapojifungua ili kuwaepusha na tatizo kama hilo.

Popular posts from this blog

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2013 wilaya ya tanga mjini pekee!!!

ARAFAH ENG-MED PRIMARY SCHOOL - P2007029 AVICENNA ENG -MD PRIMARY SCHOOL - P2007051 AZIMIO PRIMARY SCHOOL - P2007032 BOMBO PRIMARY SCHOOL - P2007001 BURHANI ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007055 CHANGA ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007033 CHANGA PRIMARY SCHOOL - P2007002 CHUDA PRIMARY SCHOOL - P2007034 CHUMA PRIMARY SCHOOL - P2007003 CHUMBAGENI PRIMARY SCHOOL - P2007004 DARAJANI PRIMARY SCHOOL - P2007005 DAYSTAR ENG - MD PRIMARY SCHOOL - P2007053 DONGE PRIMARY SCHOOL - P2007035 EBEN EZER ENG- MD PR SCHOOL - P2007048 ECKERNFORDE ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007044 GOFU-JUU PRIMARY SCHOOL - P2007006 INDIAN OCEAN ENG-MED PR SCHOOL - P2007049 JABIR BIN ZAID ENG- MED PRIMARY SCHOOL - P2007052 JUHUDI PRIMARY SCHOOL - P2007036 KANA CENTRAL ENGMED PRIMARY SCHOOL - P2007054 KANA PRIMARY SCHOOL - P2007007 KISOSORA PRIMARY SCHOOL - P2007008 KOMBEZI PRIMARY SCHOOL - P2007009 KWAKAEZA PRIMARY SCHOOL - P2007026 KWANJEKA PRIMARY SCHOOL - P2007010 MABAW...

Coastal ipo tayari kuanza ligi kuu, yashinda 3-0 ikiwa kambini Moshi.

Wachezaji wa Coastal Union wakifanya mazoezi mepesi muda mfupi kabla ya kukabiliana na Machava FC kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi, anayeonekana pichani mwenye jezi namba 17 ni haruna Moshi 'Boban'. Mtokeo ya mechi hiyo ni ushindi wa 3-0 kwa Wagosi. Mazoezi yamekolea, uwanja wa Ushirika Moshi. Uhuru Suleiman amesifiwa na kocha kuwa ni kiungo mwenye kasi nyingi na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. Mshambuliaji anayetumia mguu wa kushoto kutoka Uganda, Yayo Lutimba Kato amefunga bao lake la kwanza tangu kujiunga na Coastal Union ambayo imeweka kambi mjini Moshi tangu jana. Kato ambaye ametoka URA inayoshiriki ligi kuu nchini Uganda, alipatia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Machava FC kwenye uwanja wa Ushirika mjini humo, bao hilo alilifunga kwa ufundi mkubwa katika kipindi cha pili baada ya kupokea pasi murua na kupiga shuti kali akiwa nje ya 18. Akitoa taarifa kutoka Moshi, mwenyekiti wa Wagosi Hemed Hilal ‘Aurora’ amesema “Katika dakika za lal...

Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Dk John Magufuli   Dar es Salaam.   Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge. Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012. Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni. “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. T...