Skip to main content

Binadamu wa kwanza kufika mwezini afariki kwa ugonjwa wa moyo

NAIL Armstrong linaweza lisiwe jina maarufu enzi hizi, lakini hilo ndilo jina lililoshika chati mwishoni mwa miaka ya 1960 kwani alikuwa binadamu wa kwanza kukanyaga mwezini.Hata hivyo gwiji huyo wa mambo ya anga , amefariki akiwa na umri wa miaka 82 akiacha rekodi yake hiyo iliyotikisa dunia.
Neil Armstrong alitua mwezini Julai  20, 1969 akiwa katika chombo kilichoitwa Apollo na kusema ''hiyo ilikuwa hatua ndogo ya binadamu, lakini mapinduzi makubwa kwa ubinadamu''.
Armstrong na mwanaanga mwenzake Buzz Aldrin walitumia saa mbili na nusu wakitembea juu ya mwezi .  Neil Armstrong na wanaanga wenzake watatu Novemba mwaka 2011, walitunukiwa tuzo ya Congressional Gold Medal ambayo ndiyo ya juu zaidi inayotolewa kwa raia nchini Marekani.  Armstrong amefariki  dunia jana katika hospitali ya Columbus jimboni Ohio ambako alifanyiwa upasuaji wa moyo mapema mwezi huu.
Kulingana na wasifu wa Armstrong ambao umechapishwa na Shirika la Anga la Marekani, NASA, mwanaanga huyo aliyezaliwa jimboni Ohio mwaka 1930, alisafiri kwa ndege kwa mara ya kwanza akiwa na miaka sita, na kupata leseni ya kuendesha ndege akiwa na miaka 16, hata kabla ya kujua kuendesha gari.  Alitumikia Jeshi la Marekani kama rubani wa ndege za kivita wakati wa vita vya Korea, na baadaye akajiunga na masomo ya sayansi ya anga.   Baadaye aliajiriwa kama rubani wa kuzifanyia ndege majaribio.

Neil Armstrong alijiunga na programu ya anga mwaka 1962, na kurusha chombo cha kwanza cha anga miaka minne baadaye.   Aliteuliwa kuwa kiongozi wa wanaanga walioshiriki katika safari ya Apollo, ambayo iliwafikisha wanadamu wa kwanza mwezini.

Hatua yake ya kwanza mwezini iliangaliwa na mamilioni ya watu duniani kwa njia ya televisheni.Baada ya kutangazwa kwa kifo cha mwanaanga huyo, Mkuu wa Shirika la Anga la Marekani, NASA, Charles Bolden ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Armstrong.Charles Bolden amesema wakati wowote kutakapokuwa na vitabu vya historia, jina la Neil Armstrong litaandikwa kwenye kurasa za vitabu hivyo.
Amesifia jinsi Neil Armstrong alivyoishi maisha ya unyenyekevu, na kusema kuwa mfano wake ni wa kuigwa.   Pia Rais Barack Obama  wa Marekani ametoa salamu za rambirambi zake, na kusema mwanaanga huyo ni miongoni mwa mashujaa wakubwa wa Marekani.Amesema Armstrong pamoja na wenzake 11 katika chombo cha Apollo, walibeba matarajio ya taifa zima la Marekani katika safari yao ya anga mwaka 1969. 
''Waliionyesha dunia ari ya Marekani kuangalia mbali zaidi ya yale yanayofikirika, na kuthibitisha kuwa penye juhudi na maarifa, kila kitu kinawezekana,'' amesema Obama, na kuongeza kuwa ujumbe alioutoa Armstrong baada ya kukanyaga kwenye ardhi ya mwezini, ni mafanikio ya binadamu ambayo kamwe hayatasahaulika.  
Katika tangazo lililotolewa na familia ya Armstrong kufuatia kifo chake, mwanasayansi huyo ametajwa kuwa shujaa wa Marekani, ambaye muda wote yeye alisisitiza kuwa alichokifanya kilikuwa wajibu wake kikazi.  Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Familia yake imesema kuwa kifo chake kimetokana na matatizo yaliyofuatia upasuaji wa moyo.
Familia ya Armstrong imesema kuwa mwanaanga huyo aliendelea kufuatilia maendeleo ya safari za anga, na kila alipofanya hivyo shauku yake ya ujana ilijitokeza tena.  Neil Armstrong alistaafu kutoka NASA mwaka 1971 na alifanya kazi kwenye bodi ya wakurugenzi.   Hakupenda kuwa mtu wa kujionyesha onyesha, isipokuwa mara chache tu kwenye kumbukumbu za safari ya kwanza mwezini, au akiunga mkono kuendelea kwa utafiti wa anga.

Familia yake imesema kuwa, ingawa Neil Armstrong alipenda kuishi maisha yake bila bugudha, alifurahia ujumbe wenye nia njema kutoka kila pembe ya dunia kuhusu yeye na wenzake.

Popular posts from this blog

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2013 wilaya ya tanga mjini pekee!!!

ARAFAH ENG-MED PRIMARY SCHOOL - P2007029 AVICENNA ENG -MD PRIMARY SCHOOL - P2007051 AZIMIO PRIMARY SCHOOL - P2007032 BOMBO PRIMARY SCHOOL - P2007001 BURHANI ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007055 CHANGA ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007033 CHANGA PRIMARY SCHOOL - P2007002 CHUDA PRIMARY SCHOOL - P2007034 CHUMA PRIMARY SCHOOL - P2007003 CHUMBAGENI PRIMARY SCHOOL - P2007004 DARAJANI PRIMARY SCHOOL - P2007005 DAYSTAR ENG - MD PRIMARY SCHOOL - P2007053 DONGE PRIMARY SCHOOL - P2007035 EBEN EZER ENG- MD PR SCHOOL - P2007048 ECKERNFORDE ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007044 GOFU-JUU PRIMARY SCHOOL - P2007006 INDIAN OCEAN ENG-MED PR SCHOOL - P2007049 JABIR BIN ZAID ENG- MED PRIMARY SCHOOL - P2007052 JUHUDI PRIMARY SCHOOL - P2007036 KANA CENTRAL ENGMED PRIMARY SCHOOL - P2007054 KANA PRIMARY SCHOOL - P2007007 KISOSORA PRIMARY SCHOOL - P2007008 KOMBEZI PRIMARY SCHOOL - P2007009 KWAKAEZA PRIMARY SCHOOL - P2007026 KWANJEKA PRIMARY SCHOOL - P2007010 MABAW...

DOWNLOAD BERRY BLACK FT. ALI KIBA - ISHARA ZANGU

Msanii Dr Leader afiwa na mke,

Pole sana Dr Leader Kwa msiba mzito wa kuondokewa na mke, mzazi mwenzio na mpendwa  wako. mungu akupe roho ya uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. kila nafsi itaonja mauti.  mwenyezi mungu aiweke roho ya marahemu mahali pema peponi, You,  Selle Wamichanno  and  16 others  like this. Ally Mohamed   R.I.P SHEM.WE SASHA ALIKUWA AUMWA KWN AU? 9 hours ago  via  mobile  ·  Like Young Dutch Mahesabu   dah r.i.p shemeji yetu mpendwa ... natanguliza pole hiz kwa ndugu yetu dr.leader msambaa mungu akupe roho ya uvimilivu kwakipndi chote hki cha mpito 9 hours ago  via  mobile  ·  Like Baba Dailysuperstar   R.!.P 8 hours ago  via  mobile  ·  Like Rajab Kidagaa   R.I.P Xhem 8 hours ago  via  mobile  ·  Like Nick Regy   mung amlaze pem pepn 2ngulia n xx 2taft mpndw ri...