Masoud Kipanya
Habari kutoka Bujumbura zinasema nchi hiyo inatarajiwa kutuma wawakilishi wake wawili kuingia katika shindano la Maisha Plus 2012.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mtangazaji wa Radio Puplique Africaine, Aisha Amuri Ndimubandi ambaye ndiye mratibu wa zoezi hilo alisema "Maandalizi yote yako ta
yari, tunachosubiri ni fomu tu kutoka Tanzania ili tuanze zoezi la usaili".
Akifafanua zaidi alisema anaamini hiyo itakuwa ni moja kati ya nafasi adimu sana kwa nchi yao ambayo ina makabila makubwa mawili yaliyowahi kuwa hasimu kujifunza namna ambavyo watanzania wameweza kuishi kama ndugu licha ya uwepo wa makabila zaidi ya 120.
Burundi inakuwa nchi ya kwanza kufungua mwelekeo wa Maisha Plus kuingia katika ukanda wa Afrika ya mashariki ambapo mwakani, nchi karibu zote nne zinatarajiwa kuleta washiriki wake na kulifanya kuwa ni shindano la kwanza kutoka Tanzania lenye hadhi ya kimataifa.
Mshindi wa Maisha Plus 2012 anatarajiwa kuondoka na kitita cha shilingi 20,000,000 wakati mshindi wa MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2012 anatarajiwa kuondoka na zana kali za kilimo na mkwanja wa kutosha.