Watangazaji
wa kituo cha radio cha Sunrise cha jijini Arusha wamegoma kufanya kazi
kutokana na uongozi wa kituo hicho kushindwa kuwatimizia matakwa yao
ikiwa pamoja na kulipwa ujira mdogo na wengine kufanya kazi bila kupewa
mikataba.
Hii ni barua waliyoiandika:
Ndugu
wanahabari sisi baadhi ya wafanyakazi wa Sunrise Radio Arusha kuanzia
tarehe 22/8/2012 tumeamua kugoma kuendelea kufanya kazi na Aspire Media
Company Limited ambao ndio wamiliki wa Sunrise Radio 94.8 FM Arusha
baada ya kushindwa kutimiziwa mambo kadha wa kadha tuliyokuwa
tunayahitaji.
Mgomo
huu ulianza kama mgomo baridi mnamo tarehe 10/8/2012 baada ya sherehe
za wakulima nane nane na hii ni baada ya kutokea tofauti kati ya
mkurugenzi wa ufundi wa Sunrise Radio ndugu Dionis Idowa Sikutegemea
Moyo na kamati ya sherehe za wakulima nane nane mwaka 2012 ambao ndiyo
waliokuwa na jukumu ya kurusha matangazo ya moja kwa moja yaani live
kutoka katika viwanja vya taso nane nane Njiro.
Ndugu
wanahabari mgomo huu umesababishwa pia na kutofanyiwa kazi kwa madai
ya wafanyakazi, wafanyakazi tumekua tukifanya kazi katika mazingira
magumu kwani:-
a) Tunalipwa mishahara midogo isiyokidhi mahitaji (mshahara wa 100,000 na wengine 170,000)
b) Kufanyishwa kazi bila kuwa na mikataba, tukidai mikataba tunapigwa tarehe
c) Kutokatwa makato kwenye mishahara kwaajili ya pensheni
d) Baadhi ya wafanyakazi kufanyishwa kazi bila kulipwa
e) Hakuna overtime payment
f) Wafanyakazi kutishiwa kufukuzwa mara kwa mara pale wanapodai haki zao
g) Hakuna likizo
h)
Waandishi wa habari walioripoti live ya uchaguzi wa Arumeru Mashariki
tarehe 1/4/2012 kutolipwa posho zao hadi leo na wengine walidai na
hatimaye wakafukuzwa kazi
i)
Mishahara wa wafanyakazi kucheleweshwa kulipwa kwani utakuta mshahara
wa mwezi huu tunaweza kulipwa mwezi ujao katikati au mwishoni
j) Mkurugenzi wa ufundi kutishia kumfukuza kazi mhasibu kwa maslahi yake binafsi
k)
Wafanyakazi wanaofanya vipindi vya usiku kutopewa usafiri wakati wa
kwenda na kurudi kitu ambacho kinamlazimisha mtangazaji kulala studio
kwa lazima
l) Gari la ofisi kutotumika kwa mahitaji ya ofisi bali kwa maslahi ya mkurugenzi wa ufundi
m)
Mishahara ya mwezi July ya baadhi ya wafanyakazi kuzuiliwa kuanzia
tarehe 1/8/2012 hadi leo hii tarehe 22/8/2012 kwa sababu zisizo za
msingi
Ndugu
wanahabari, kwa madai hayo hapo juu sisi wafanyakazi wa sunrise radio
hatupo tayari kurudi kazini mpaka pale mkurugenzi wa ufundi ndugu
Dionis Idowa Sikutegemea Moyo atakapojiuzulu nafasi yake na madai ya
wafanyakazi yatakapokua yametatuliwa.
Dionis Idowa |
Tunaipenda
sana Sunrise Radio bila kuwasahau wasikilizaji wetu pia tunawapenda
sana ila tumeona ni vyema kuyaweka bayana haya yote ili mtuelewe na pia
ni majibu ya baadhi ya maswali mliyokuwa mnatuuliza wasikilizaji wetu
wapendwa.
NDUGU WANAHABARI WAFANYAKAZI WA SUNRISE RADIO WALIOGOMA KUFANYA KAZI IDADI YAO NI KUMI NA WAWILI (12) WAKIWEMO
a) WATANGAZAJI 4
b) MARIPOTA 2
c) WATU WA MASOKO 3
d) WAZALISHAJI WA VIPINDI 2 NA
e) MHASIBU 1
WAFANYAKAZI HAO WAMEGOMA KUTOKANA NA MADAI YAO HAPO JUU PAMOJA NA MADAI MENGINE MENGI AMBAYO HAYAJAORODHESHWA
MAJINA YA WAFANYAKAZI WALIOGOMA NI HAYA YAFUATAYO
1. SEVERINUS MWIJAGE Jr – MTANGAZAJI
2. BEATRICE GERALD NANGAWE – MTANGAZAJI
3. EMMANUE MWAKALUKWA – MTANGAZAJI
4. JALACK ALLY – MTANGAZAJI
5. HAMIS ABTWAY (DJ HAAZU) – MTANGAZAJI, MZALISHA VIPINDI NA DJ
6. BERTHA ISMAIL – RIPOTA
7. ONESMO LOY – RIPOTA
8. JOSEPH AMANI – MZALISHAJI WA VIPINDI
9. ALLY CHARO – MENEJA WA MASOKO
10. RODGERS I. NELSON – MHASIBU
11. WITNESS RAYMOND – MASOKO
12. HAPPYNESS ALPHONCE – MASOKO