Na Giden Mwakanosya, Songea ALIYEKUWA Katibu Mwenezi wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Kata ya Mjimwema iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa
ya Songea mkoa wa Ruvuma Magdalena Zuru Gama amejivua uwanachama wa
chama hicho na amejiunga katika Chama cha Democrasia na Maendeleo
(CHADEMA) na amedai kuwa amefanya uamuzi huo akiwa na akili timamu
ambapo ameeleza kuwa ameona chama hicho kinaendelea kukosa maendeleo na
baadhi ya viongozi wa mejaa ubinafsi. Magdalena Gama alitoa kauli hiyo
jana kwenye ofisi ya chadema kata ya Mjimwema wakati alipokuwa
akikabidhiwa kadi mpya ya CHADEMA baada yakuomba na chama hicho kwa
mwenyekiti wa CHADEMA wa tawi la Pachanne lililopo Mjimwema Swedi
Milanzi ambako kulihudhuliwa na wanachama wa chama hicho. Alisema kuwa
ameamua kukihama chama cha CCM baada ya kuona baadhi ya viongozi wa CCM
wamekuwa na tabia ya ubinafsi na kuonekana kuwa CCM ni ya kwao wao
wenyewe na kwamba kila nafasi inayotangazwa kugombea wanafanya kila njia
wagombee wao wenyewe na kuwakatisha tamaa wanachama wengine wanaotaka
kugombea nafsi hizo. Alifafanua zaidi kuwa alijiunga na uwananchama wa
CCM tangu mwaka 1981 baada ya kupata mafunzo ya elimu ya siasa kwa muda
wa miezi 3 hivyo alikuwa mwanachama wa muda mrefu na amewahi kushika
nyadhifa mbalimbali za chama hicho licha ya kuwepo mizengwe ya hapa na
pale iliyokuwapo ikifanywa na baadhi ya viongozi ambao walioifanya chama
cha CCM ni mali yao,hivyo ameamua kujiunga na chama cha Chadema ambacho
ndio chama pekee chenye sera nzuri zenye tija kwa watanzania. Kwa
upande wake mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya chama hicho Samweli
Chale alisema kuwa kitendo alichokifanya Magdalena Gama kukihama chama
cha Ccm na kukimbilia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ni cha
kiungwana kwani Ccm imejaa fitina hasa kwa wale Viongozi wanaoonekana
kwa jamii kuwa makini. Chale ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha
Democrasia na Maendeleo (Chadema) kata ya Bombambili alisema kuwa
msimamo wa Chadema ni kuboresha zaidi maendeleo mbalimbali ya wananchi
na kila malengo makini ya kuhakikisha kuwa chama kinashika dola kuanzia
ngazi ya uongozi wa Serikali za mitaa,vitongoji na vijiji na kwamba
hakuna chama kingine chenye kipaombele ni Chadema peke. Naye Mwenyekiti
wa Baraza la vijana Chadema(Bavicha) wa Kata ya Mjimwema John Mkina
alieleza kuwa nguvu ya chama inazidi kuongezeka na alidai kuwa baadhi ya
viongozi wa Chama cha Mapinduzi wameonesha nia ya kutaka kujiunga na
chama hicho hivyo Magdalena Gama ni sehemu ya wananchama wengi waliomba
kutaka kujiunga na Chadema ambao wanataraijwa kukaribishwa kwa mikono
miwili kujiunga na chama hicho
CAST SELEMANI MOHAMED / BUNTO ANDREW / C-O YORAM MWETA / MGANGA MWANTUMU / MKE WA C-O JOHN / MCHUNGAJI BI FURURATU / JINI WAOMBOLEZAJI SAUMU HUSENI HASHIMU BABA RASTA MAN YOHANNA TAMILWAI SAIDI MWALUBADU SEMY STIR SELEMANI MOHAMEDI AND ANDREW C-O LOCATION ATHUMANI HAMADI MAKE UP MWASHAMBA RAMADHANI BEDUI DEREVA DAUDI SPOONSER SAIDI SHABANI AND THE FRESH2012 GLOB SOUND PRODUCER J-B LIGHT YOHANNA TAMILWAI THENK YOU THE FRESH ENERTAINMENT AND THE FRESH2012 BLOG CONTACTS 0653785027 +255714091786 ZAIDI TEMBELEA www.the-fresh.blogspot.com ADRESS Thefresh@ymail.com AU Saidshabani60@gmai.com