'Ulikuwa wakati wa ajabu kwangu' alisema Hezekiah nduguye Ezekiel mwenye umri wa miaka 13.'Kila mtu kanisani alitupigia makofi kwa furaha na kutupongeza'
Micah, nduguye Hezekiah ana mumri wa miaka saba na tayari anataka kufuata nyayo zake hezekaih 'Tayari nimetayarisha mahubiri lakini nitayahubiri nitakapo hitimu miaka 10' alisema Micah kwa sauti ya unyenyekevu.
Sio nchi ya marekani tu ambayo ina watoto wanaohubiri, bali Brazil pia imeboboea katika jambo hili.Indonesia pia haijawachwa nyuma kwani ina kipindi cha runinga ambacho wahubiri wachanga wa dini ya kiislamu hishindana. ini se
'Jambo hili lina uwezo wa kuchipuka haswa katika dini ambazo husisistiza uwepo ya roho mtakatifu na pia jamii zilizotengwa' asema Edith Blumhofer mtaalam wa historia ya wakristo chuo cha Wheaten mjini Illinois.
Ted Lavigne kasisi aliye staafu na anaandika kitabu kilicho na mada hii ya watoto wahuburi,asema kuwa wahubiri wengi watoto walisikika sana miaka ya 1920 na 1930 wakati ambapo kanisa la pentekoste lilikuwa changa.
Fasihi za awali zinaelezea wakati huu ambapo watoto walisikika wakinena maneno yenye hekima kuliko miaka yao.Jambo hili lilipokelewa kwani lilikuwa thibitisho la uwepo wa Roho Mtakatifu.
Jambo la kushangaza ni kwamba,jinsi makanisa haya yalipoendelea kuwatumia watotohawa ndivyo waliendelea kuonekana wamejitenga.
Lavigne amegundua takriban mifano 500 tangu miaka ya 1500 na 1700 ya watoto hawa,wengi wao wakiwa na asili ya marekani na wengine uingereza.
'Kuna elimu ya nguvu ya kidini inayoendelea hapa nchini.Hapa Amerika kuna watu wanaopeda dini sana' asem Randall Balmer mwenyekiti wa kitengo cha dini chuo cha Dartmouth.
Kanuni zinazosema nani anayeweza kuanzisha kanisa zina posho kubwa kwa hivyo mtu yeyote anaweza kuanzisha kanisa mahali popote.Kanisa la familia ya Ezekiel ni kanisa ambalo halifuati madhehebu yoyote kwa hivyo wana uhuru wa kufanya mambo yao vyovyote.
Hata hiyo si vigumu kupata watu walio na wasiwasi kuhusu watoto wahubiri.Watu kama hawa huwa na dhana kuwa ni wachanga sana kuapishwa kama kasisi na wana ushahidi wa kesi za watoto wahubiri waliopotoka.
Ushahidi mkubwa haswa ni ule wa Marjoe Gortner,mtoto mhubiri aliyetangaza baada ya miaka mingi kuwa hakuamini kuwa kuna Mungu na alikuwa mhubiri kwa shinikizo ya wazazi wake na baadaye kama ajira.
Wazazi wa Ezekiel wanafahamu fika mambo haya na wako tayari kumtetea mtoto wao.Mamake asema kuwa watoto wake wana adabu na tabia nzuri.Maisha ya watoto wao ina uwianao,kwani hata ingawa ni wahubiri wao kufanya vitu ambavyo watoto wa kawaida hufanya kama kwenda shule,kucheza na watoto wengine na kadhalika.
Ezekiel bado hajaamua kazi atakayoifanya maishani. Hajaamua kama atakuwa mhubiri maisha yake yote ama ataifanya kazi ingine.
Siku hizi watoto wanao hubiri ni wachache nchini amerikani na amabao wako,huhubiri kwenye mitaani.