Skip to main content

MAMBO MANNE YANAYOWAVUTIA WATALII MAPANGO YA AMBONI TANGA

Hussein Semdoe, Tanga








KUMBE mapango maarufu ya Amboni yaliyopo katika Kata ya Kiomoni, Tarafa ya Chumbageni wilayani Tanga, Mkoa wa Tanga, ni sehumu muhimu ya kujivunia na ya kihistoria ya nchi yetu, kutokana na miamba ya mapango hayo kituo cha hija kwa watu mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania .
 
Kutokana na umuhimu wa mapango hayo watu 42, wamekuwa wakitembelea kila siku kwa ajili ya kufanya matambiko na kutoa sadaka kwa kizimu.

Mambo yanayovutia Mapango ya Amboni
Mambo manne yanayowavutia wataliii katika mapango hayo ni: mawe yakua kama mimea, sanamu ya Bikira Maria, maandiko ya Quran takatifu, miamba inayofanana na kochi na meli, na barabara zinazopita ndani ya mapango hayo. 
Kwa mujibu wa utafiti, miamba hiyo inakua kwa kasi zaidi katika kipindi cha mvua, ukilinganisha na msimu wa kiangazi. Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ukuaji wa miamba hiyo ulikuwa kwa  milimeta 0.5 na iliwahi kuongezeka kwa kasi ya milimeta saba katika kila baada ya miaka 100.
 
Mkuu wa Kituo cha Hifadhi ya Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora anasema mawe yanakua kama mimea hai na mengine kushuka chini kama mizizi.

"Kuna miamba inayokua ama kuongezeka, kutokana na mabadiliko ya kikemikali katika miamba ya chokaa. Mabadiliko haya yanasababishwa na maji yenye tindikali kuyeyusha madini ya 'Calcium Carbonate,' kuyahamisha na kuyarundika katika eneo lingine, matokeo ni kupata miamba inayokua," anasema Gekora.

Mkuu wa Kituo cha Hifadhi ya Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora, anasema katika mapango hayo kuna njia ndani ya mapango hayo kutoka hapo kwenda Mombasa nchini Kenya, kwenda mkoani Kilimanjaro na kuibukia Maweni nje kidogo ya Jiji la Tanga.

Pia katika mapango hayo kuna sanamu ya ajabu ambayo inafananishwa na ya Bikira Maria. Sanamu hiyo ipo ndani ya mapango hayo ambayo inamshangaza kila mtalii anatembelea mapango hayo.

Mbali na sanamu hiyo pia sehemu ya miamba hiyo kuna maandishi ya asili, yanaelezwa ni ya kitabu kitukufu cha Quran takatifu, yakiwa yameandikwa katika miamba hiyo.
 
Vivutio vingine vilivyopo katika mapango hayo ni miamba yenye maumbo yanayofanana na kochi, meli, na wanyama kama mamba na Tembo.

Gekora, anasema miamba hiyo ni aina ya chokaa, na inawavutia watu mbalimbali kwa kuwa ni eneo maalumu la kiimani ambalo watu wanamaliza matatizo ya kijamii, yakiwamo kuwaombea wagonjwa na mengine.
Historia ya Mapango ya Amboni
Inasadikika kwamba mapango hayo yalianza kutumika miaka zaidi ya miaka 500 iliyopita. Anasema Wazigua, Wambondei na Wasambaa walianza kufanya matambiko na kupata matibabu ya jadi.

Pia zipo simulizi za Osale Otango (Samwel Otango) na Paulo Hamis. Watu hao waliwahi kutumia kituo namba tatu ndani ya pango kubwa, kama sehemu yao ya kujificha kati ya mwaka 1952 na 1956, huku wakiendesha harakati za kupambana na walowezi waliokuwa wamewekeza katika maeneo ya Tanga.
 
Mwaka 1957, Paulo Hamisi, alipigwa risasi maeneo ya Lushoto na kufariki dunia na wananchi wa kawaida wanawakumbuka kama mashujaa walioendesha harakati za ukombozi wa watu wanyonge kutoka katika mikono ya walowezi na watawala wa kikoloni.
Anasema haijulikani mapango hayo yaligunduliwa lini, lakini taarifa zilizopo zinaonyesha kwamba, watu wa makabila yaliyoishi jirani na eneo la Mapango ya Amboni, walikuwa wakiyatumia kwa matambiko tangu Karne ya 16,  na lilijulikana kama eneo la ‘mzimu wa mabavu.
 
"Watu wanaoamini habari za nguvu za mizimu kutatua matatizo ya uzazi, kuongeza kipato, kuondoa magonjwa wamekuwa wakitoka sehemu mbalimbali katika Bara la Afrika Mashariki na kuja kuomba ama kutambikia mizimu katika mapango mbalimbali hapa Amboni," anasema mkuu wa hifadhi hiyo.

Kampuni ya kigeni ya Amboni Limited ilimiliki mashamba ya Mkonge katika eneo la Tanga na kuweka eneo hilo chini ya himaya yake mwaka 1892. Wamiliki wa kampuni hiyo walitumia eneo hilo kama sehemu ya kupunzikia kutokana na eneo hilo kuwa na mazingira mazuri ya kupunzikia na yenye utulivu. Baadaye mwaka 1922, Serikali ya kikoloni ilitanga eneo hilo kuwa hifadhi.

Mapango hayo yapo umbali wa kilomita nane kutoka Jijini Tanga kupitia barabara kuu inayoelekea Mombasa nchini Kenya. Kwa mujibu wa taarifa za historia,  hifadhi hiyo ilitokana na  mabadiliko ya nguvu za asili zilizobadilisha maumbile ya miamba ya chokaa kipindi cha ‘Jurasiki' (jurassic period) kama miaka 150 milioni iliyopita.
 
Tafiti hizo zinaonyesha kwamba eneo hilo la Amboni lilikuwa chini ya maji miaka milioni 20 iliyopita na linakadiriwa kuwa na ukubwa wa kilomita za mraba 234 lenye mazingira ya miamba ya chokaa. Ni eneo ambalo linapitiwa na mito ya maji na limejaa uoto wa asili.

Hatari ya Mapango ya Amboni kuvunjika
Licha ya eneo hilo kuwa kivutio muhimu na urithi wa Taifa, lakini eneo hilo linakabiliwa na matatizo mengi kutokana na kuzunguukwa na milipuko ya baruti inayotokana na uvunjaji wa mawe ya chokaa.
 
Serikali isipopiga marufuku uvunjaji wa miamba, kuna hatari ya miamba hiyo kupasuka na kuanguka. Pia watalii wanaotembelea mapango hayo na kuingia ndani ya mapango wanaweza kuangukiwa na mapande ya miamba baada ya kuvunjika.
 
Wakati nikikaribia eneo hilo nilikuta kiwanda kikubwa cha chokaa kikiwa kinafanya kazi zake za kuzalisha chokaa, lakini hali ya hewa katika eneo hilo haifai kwa afya ya binadamu wala wanyama waishio pembezoni. Eneo hilo limejaa vumbi na moshi hewani, hali iliyofanya niwahi kuondoka katika eneola Kiomoni.
 
Muda mfupi baadaye nikasikia mlio ambao ulinishtua nikauliza na walieleza kwamba milio hiyo siyo mabomu ya kivita bali ni milipuko ya baruti inayotumiwa kupasua miamba ya kuzalishia chokaa, waliniambia kwamba hata wao wanaishi kwa taabu kutokana na milio hiyo pamoja na uchafuzi wa mazingira.
 
Wakazi hao wanasema licha ya kukerwa na sauti za milio hiyo pamoja na hewa kuchafuka, pia milipuko hiyo imesababisha nyumba kupata nyufa.
 
Msimamizi wa kituo hicho cha Amboni anaomba mamlaka zinazohusika ikiwamo Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Tamisemi, kudhibiti ulipuaji wa miamba hiyo iliyopo jirani na Mapango ya Amboni.
  
Anasema milipuko hiyo inatisha wageni hivyo isipodhibitiwa huenda ikapunguza idadi ya wageni wanaotembelea eneo hilo na kusababisha kupungua kwa mapato.
 
Anasema gharama kutembelea mapango hayo kwa watu kutoka ndani ya nchi ni Sh1,000 na wanafunzi Sh500. Kwa wageni wanalipa Sh 20,000 na wanafunzi wageni Sh10,000.

Popular posts from this blog

MAJINA YA WASHIRIKI NA WA WEZESHAJI WA FILM YA HOUSE GIRL!

CAST SELEMANI MOHAMED / BUNTO ANDREW / C-O YORAM MWETA / MGANGA MWANTUMU / MKE WA C-O JOHN / MCHUNGAJI BI FURURATU / JINI WAOMBOLEZAJI SAUMU HUSENI HASHIMU BABA RASTA MAN YOHANNA TAMILWAI SAIDI MWALUBADU SEMY STIR SELEMANI MOHAMEDI  AND ANDREW C-O LOCATION ATHUMANI HAMADI MAKE UP MWASHAMBA RAMADHANI BEDUI DEREVA DAUDI SPOONSER SAIDI SHABANI AND THE FRESH2012 GLOB SOUND PRODUCER J-B LIGHT YOHANNA TAMILWAI THENK YOU THE FRESH ENERTAINMENT AND THE FRESH2012 BLOG CONTACTS 0653785027 +255714091786 ZAIDI TEMBELEA www.the-fresh.blogspot.com ADRESS Thefresh@ymail.com AU Saidshabani60@gmai.com

Sababu ya Alicia Keys kumuita mwanae Misri (Egypt)

Siku chache kabla ya Mother’s Day Alicia Keys alihojiwa kwenye talk show iitwayo  ‘The Conversation’ inayotayarishwa na Demi Moore na mtangazaji akiwa Amanda de Cadenet. Waliongea mengi kuhusu maisha yake kama mama, umbo lake baada ya kuzaa, kunyonyesha na sababu iliyomfanya amuite mwanae Misri. “Well, Misri ilikuwa safari muhimu katika maisha yangu” Alisema Alicia. Ilikuja katika pointi ambayo nilikuwa nimefanya kazi mno bila kupumzika na sikuwa na idea yoyote kuhusu kuchukua likizo ya kweli na ilikuja katika muda huo ambao niliihitaji.  Hivyo nilipoenda, ilinipa nguvu sana, ikanifungua macho, safari ya kihistoria, yenye nguvu na experience ya pekee iliyonifanya niipende Misri.  Alicia, Demi na Amanda Hivyo  ulipokuja wakati wa kumpa jina mtoto wetu, nililipenda, wote tulilipenda na tuliamua miezi kadhaa hata kabla hajazaliwa” Egypt na baba yake Swizz Beatz Kuhusu kwanini alienda peke yake nchini Misri alisema “Muda huo nilihitaji sana kwenda

Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Dk John Magufuli   Dar es Salaam.   Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge. Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012. Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni. “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba