Soko la Samaki la Kasanga.
Mazungumzo
yakiendelea Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Kutoka kulia ni Kaimu
Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Rukwa Emmanuel Kachewa, Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a, Mrs. Katyega, Mkurugenzi Mkuu
Msaidizi Uwekezaji wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO Maneno Katyega,
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Katibu Tawala Mkoa wa
Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo
Florence Mtepa.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkurugenzi Mkuu
Msaidizi Uwekezaji wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO Maneno Katyega
Ofsini kwake jana alipotembelea Mkoani Rukwa kwa ajili ya kufuatilia
miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo alitembelea Soko la Samaki la
Kasanga pamoja na kujionea maendeleo ya mradi wa umeme kwenda Wilaya ya
Nkasi.
Hakika
ziara ya Mkurugenzi huyo Msaidizi imekuwa ya mafanikio makubwa kwani
baada ya kutembelea Soko kubwa la Samaki la Kasanga na kujionea umuhimu
uliopo wa nishati ya umeme katika kuendesaha soko hilo ameahidi kupitia
Shirika lake kuwa soko hilo litapatiwa Jenereta kubwa mbili kila moja
ikiwa na uwezo wa 50KV. Alisema kuwa Umeme utakaozalishwa kutokana na
Jenereta hizo utaweza pia kuhudumia Vijiji vya jirani vinavyolizunguka
Soko hilo.
Jitihada
za kulipatia Soko hilo umeme zimekuwa zikipewa msukumo mkubwa na Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ambae amekuwa akilifuatilia kwa
karibu ambapo amefanikiwa kumpeleka kiongozi huyo wa Tanesco hadi eneo
la mradi huo ikiwa ni katika jitihada zake za kutekeleza agizo la Mhe.
Makamu wa Rais alipofanya ziara yake Mkoani Rukwa na kutoa agizo kwa
uongozi wa Mkoa ushirikiane na Tanesco kuhakikisha Soko hilo linapatiwa
umeme.
Akiwa
Mkoani hapa Kiongozi huyo wa Tanesco alikuta baadhi ya mapungufu katika
utekelezaji wa mradi utakaopeleka umeme Wilayani Nkasi ambapo
walishauriana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambapo walikubaliana litafutwe
suluhu la changamoto hizo badala ya kulaumiana ili kukamilisha mradi
huo muhimu kwa Wilaya ya Nkasi na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla.
huo muhimu kwa Wilaya ya Nkasi na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla.