Skip to main content

Serikali ikiheshimu bajeti, bei za bidhaa zitashuka

File:Prof. Lipumba (left) and Seif Shariff Hamad (right) in their victory press conference after the by-elections, 19 May 2003, Chake Chake town, Pemba, Tanzania.JPGMtaalamu wa masuala ya Uchumi,Profesa Ibrahim lipumba



UKIPITA madukani, sokoni utawaona watu wakiomba wapunguziwe bei ya bidhaa na nyingine zimekuwa zikikaa muda mrefu licha kupungua kwa mfumuko wa bei. Achilia mbali sokoni na dukani, lakini pia katika ‘supermarket’ ukisimama kwa mbali utaona wateja wakiingia na kutoka bila kununua bidhaa yeyote kutokana na kushindwa kumudu bei ya bidhaa. Pia ukipita katika mitaa mbalimbali ya watu, utakuta watu wakilalamikia ukosefu wa ajira na ugumu wa maisha. Wakati wakazi wakilalamikia ugumu wa maisha unavyowaumiza, baadhi yao wamekuwa wakipunguza idadi ya milo kwa siku. Kwa kawaida ratiba ya milo ni mara tatu kwa siku: asubuhi, mchana, na jioni, lakini kutokana na ugumu wa maisha baadhi wamekuwa wakila mlo mmoja kwa siku. Wakati wananchi wakilalamika kuhusu ugumu wa maisha, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), imetoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei na kubainisha kwamba umepungua kutoka asilima 15.7 Julai hadi kufikia asilimia 14.9, Agosti mwaka huu. Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa anasema, kupungua kwa mfumuko wa bei Agosti mwaka huu kunamaanisha kwamba kasi ya kupanda kwa bei za bidhaa na huduma zimeendelea kupungua. Dk Chuwa anasema mfumuko wa bei umekuwa na mwenendo wa kupanda kutoka asilimia 14.1 Agosti mpaka kufikia asilimia 19.8 Desemba mwaka jana. “Kuanzia Januari mwaka huu, mwenendo wa mfumuko wa bei ulianza kushuka kutoka asilimia 19.7 hadi kufikia asilimia 14.9 mwezi uliopita,” anasema Dk Chuwa. Wachumi Mtaamalu wa uchumi, Profesa Ibrahim Lipumba anaeleza kwamba licha ya mfumuko wa bei kushuka, lakini bado bei ya bidhaa ipo juu. Anasema mfumuko huo umeshuka, lakini katika masomo mbalimbali, bei ya vyakula zipo juu. Kwa mfano, mkoani Tabora katika kipindi kama hiki cha mavuno kwa kawaida debe moja la mahindi limekuwa likiuzwa Sh6,000 mpaka Sh7,000, lakini hivi sasa katika kipindi hiki linauzwa Sh 9,000. “Serikali inatakiwa kuwa makini na matumizi ya fedha endapo matumizi yakiwa mabaya ni dhahiri mfumuko utapanda tena na kurudi tulilkotoka,” anaeleza Profesa Lipumba. Wakati Profesa Lipumba akieleza bei ya bidhaa katika Mkoa wa Tabora, uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa makala hii katika masomo mbalimbali ya Dar es Salaam amebaini bei ya mchele na maharagwe bado ipo juu. Bei ya mchele wa Mbeya ni kati ya Sh1,600 mpaka Sh2,700, maharagwe yamekuwa yakiuzwa kati ya Sh1,700 na Sh1,200 kwa kilo. Gunia la kilo 100 la maharagwe ya Mbeya ambalo mwaka jana lilikuwa Sh120,000, sasa linauzwa Sh135,000 mpaka Sh150,000. Maharagwe kutoka Bukoba mkoani Kagera na Arusha yanauzwa kati ya Sh1,300 mpaka Sh1,400 kwa kilo. Licha ya Serikali kupitia NBS kutangaza kushuka kwa mfumuko wa bei bado wateja katika masoko mbalimbali wamepungua na kusababisha wafanyabiashara kuwa katika wakati mgumu. Mhadhiri wa Chuo Cha Mzumbe, Dk Prosper Ngowi anasema tabia ya mfumuko wa bei kushuka imeanza tangu Januari mwaka huu kwa kiwango kidogo. Dk Ngowi anasema licha ya kushuka kwa mfumuko wa bei, bado bei ya bidhaa bado iko juu kwamba hali hiyo haionyeshi tofauti ya maisha kwa wananchi. Anasema kupungua kwa mfumuko wa bei kumesababishwa na msimu huu wa mavuno. “Bado maisha ya wananchi yapo juu na hayaendani na takwimu hizo. “Lengo la sera ya Serikali ni kuhakikisha mfumuko wa bei unafikia asilimia tano na hivi sasa ni asilimia 14.7, bado safari ni ndefu ya kufika tunakotaka kwenda,” amsema Dk Ngowi. Mhadhiri wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dk Bill Kiwia anasema kushuka kwa mfumuko wa bei unatakiwa uendane na upatikanaji wa ajira kwa vijana. Dk Kiwia anasema Kampuni ndogo ndogo zinatakiwa kutoa ajira kwa wingi kwa vijana, lakini hivi sasa ni tofauti na kwamba hali haiendani na kushuka kwa mfumuko wa bei nchini. Anasema kushuka kwa mfumuko huo hauendani na hali halisi ya maisiha ya Watanzania. Dk Kiwia anasema mfumuko wa bei katika nchi ya Kenya na Uganda upo chini na kwamba unaendana na hali ya kiuchumi ya wananchi. Kwa mjibu wa taarifa za mfumuko wa bei nchini Uganda, imekuwa ukishuka kutoka asilimia 18.0 Juni mwaka huu mpaka kufikia asilimia11.9 mwezi uliopita. Kenya mfumuko ulifika asilimia 6.09 mwezi uliopita kutoka asilimia 10.05 Juni mwaka huu na Zambia umetoka asilima 6.7 Juni mwaka huu na kufikia asilimia 6.4 mwezi uliopita. Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Semboja Hadji anaeleza kwamba mfumuko wa bei unaonyesha unafuu katika shida. Dk Hadji anaitahadharisha Serikali kuzingatia matumizi yake ya fedha kama yalivyopitishwa na Bunge la bajeti, Julai mwaka huu. Anaeleza endapo Serikali itakuwa na matumizi makubwa tofauti na ilivyopitishwa na Bunge, matumizi hayo yatasababisha kupanda kwa mfumuko wa bei. “Kwa kawaida, Serikali ikifanya matumizi kuzidi bajeti itasababisha kupanda kwa mfumuko wa bei. “Zile sababu ambazo zimesababisha mfumuko wa bei kushuka inatakiwa izingatiwe ili kuhakikisha tunafikia asilimia tano na kuendana na hali halisi ya maisha ya Watanzania,” anasema Dk Hadji. Kwa kawaida Serikali ikibana matumizi na kuimarisha sekta nyingine za uchumi wananchi mfumuko wa bei unapungua na kuendana na hali halisi ya wananchi. Dk Hadji anasema Serikali inatakiwa kuweka kipaumbele katika sekta ya kilimo ambayo kama itasimamiwa ipasavyo iitasaidia kushuka kwa mfumuko wa bei. “Unakuta mkulima analima mazao ya chakula tu na hii inatokana na hamasa inayotolewa na Serikali, hivyo juhudi za makusudi zinahitajika. “Tukifanye kilimo kiwe kilimo cha biashara, tuondokane na kilimo cha mazoea kwani tutapiga hatua endapo tukitumia ardhi yetu vizuri,” anasema Dk Hadji. Mhadhiri huyo amewashauri wakulima kuzingatia kulima mazao ambayo yatakuwa ya ushindani katika soko na kuacha kulima mazao yasiyokuwa na ushindani. Wananchi Mkazi wa Tegeta Dar es Salaam, Paulo Vitus anaeleza kuwa hafahamu kama kweli mfumuko wa bei umepungua kwani hakuna tofauti yeyote. Vitus anasema ukipita katika maduka, sokoni na sehemu zingine wanazouza bidhaa mbalimbali huwezi kubaini kama ma mfumuko wa bei umeshuka. “Hizo zitakuwa ni takwimu tu, lakini kihalisia bado maisha ni magumu na sijaona tofauti yeyote labda kwa vingozi wakubwa wa serikalini ndio wanafahamu kushuka kwa mfumuko huo,” anaeleza Vitus. Naye Suzana Andrew mkazi wa Ilala Dar es Salaam anasema hali ya maisha ni ngumu na hakuna mabadiliko yeyote yanayoendelea. Andrew anasema bei ya vyakula kama mchele na maharage bado ipo juu na hawezi kusema mfumuko wa bei umeshuka. “Kama kweli kilimo kikitumika kama uti wa mgongo wa Mtanzania, ni dhahiri mfumuko huu tunaoambiwa umeshuka utaendana na hali halisi ya maisha ya mwananchi,” anaeleza Andrew.

Popular posts from this blog

MAJINA YA WASHIRIKI NA WA WEZESHAJI WA FILM YA HOUSE GIRL!

CAST SELEMANI MOHAMED / BUNTO ANDREW / C-O YORAM MWETA / MGANGA MWANTUMU / MKE WA C-O JOHN / MCHUNGAJI BI FURURATU / JINI WAOMBOLEZAJI SAUMU HUSENI HASHIMU BABA RASTA MAN YOHANNA TAMILWAI SAIDI MWALUBADU SEMY STIR SELEMANI MOHAMEDI  AND ANDREW C-O LOCATION ATHUMANI HAMADI MAKE UP MWASHAMBA RAMADHANI BEDUI DEREVA DAUDI SPOONSER SAIDI SHABANI AND THE FRESH2012 GLOB SOUND PRODUCER J-B LIGHT YOHANNA TAMILWAI THENK YOU THE FRESH ENERTAINMENT AND THE FRESH2012 BLOG CONTACTS 0653785027 +255714091786 ZAIDI TEMBELEA www.the-fresh.blogspot.com ADRESS Thefresh@ymail.com AU Saidshabani60@gmai.com

Sababu ya Alicia Keys kumuita mwanae Misri (Egypt)

Siku chache kabla ya Mother’s Day Alicia Keys alihojiwa kwenye talk show iitwayo  ‘The Conversation’ inayotayarishwa na Demi Moore na mtangazaji akiwa Amanda de Cadenet. Waliongea mengi kuhusu maisha yake kama mama, umbo lake baada ya kuzaa, kunyonyesha na sababu iliyomfanya amuite mwanae Misri. “Well, Misri ilikuwa safari muhimu katika maisha yangu” Alisema Alicia. Ilikuja katika pointi ambayo nilikuwa nimefanya kazi mno bila kupumzika na sikuwa na idea yoyote kuhusu kuchukua likizo ya kweli na ilikuja katika muda huo ambao niliihitaji.  Hivyo nilipoenda, ilinipa nguvu sana, ikanifungua macho, safari ya kihistoria, yenye nguvu na experience ya pekee iliyonifanya niipende Misri.  Alicia, Demi na Amanda Hivyo  ulipokuja wakati wa kumpa jina mtoto wetu, nililipenda, wote tulilipenda na tuliamua miezi kadhaa hata kabla hajazaliwa” Egypt na baba yake Swizz Beatz Kuhusu kwanini alienda peke yake nchini Misri alisema “Muda huo nilihitaji sana kwenda

Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Dk John Magufuli   Dar es Salaam.   Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge. Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012. Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni. “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba