Mheshimiwa Philipo Mulugo
Kuanzia juzi taarifa na
video ya Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi wa Tanzania Philipo
Augustino Mulugo zimeanza kusambaa kwa watanzania wengi kuhusu
alichosema akiwa Afrika Kusini kwenye mkutano wa kimataifa kwamba Tanzania ni muungano wa visiwa vya bahari ya Hindi, Pemba na Zimbabwe.
Mulugo leo amezungumza na
Power Breakfast ya CLOUDS FM na kusema kabla ya yeye kupanda kuanza
kuzungumza kulikua na kiongozi wa Zimbabwe ambae alitoka kuzungumza na
nina mkariri akisema
“sasa
ilibidi lazima baada ya kufika pale ni lazima umshukuru mwenzako
aliepita sasa kama mawazo ndiyo yaliyokua yamedhania hivyo kwamba basi
hapa naitamka Zimbabwe kwa sababu zote zimeanzia na Z labda ilitokea
hivyo lakini nakiri kabisa kwamba sikua na makusudio kwamba naitamka
Zimbabwe lakini kule kwenye power
presentation inaonekana kabisa ukifungua pale ni Tanzania imeungana na
Zanzibar Pemba na Tanganyika kama ambavyo tunajua kwa sababu ile ni
historia hakuna asiejua hata mtoto wa darasa la tatu”
“Niseme tu kwamba hiyo ni kuteleza
kwa ulimi na nilikua namfikiria yule waziri wa Zimbabwe kwa sababu
alikua ametoka kuhutubia kabla ya mimi, nilikua naomba ieleweke
hivyo…………
na
wengi wameongea wanahoji lugha kiingereza, jamani tukubaliane kwamba
kusema Zimbabwe badala ya Zanzibar sidhani kama inaendana na drama
yenyewe kwa sababu mimi nimekua mwalimu mda mrefu nimefundisha wanafunzi
wangu na wananifahamu uwezo wangu mkubwa na tena mimi ni mwalimu wa
historia hata degree yangu ni mimi ni mwalimu wa historia na Economics,
labda
niliongea nilikua sijielewi na ningegundua nimetamka Zimbabwe ningeweza
kuomba radhi, mataifa yote wawe waafrika wawe wazungu wengi huwa
tunazingatia kuangalia kwenye power point pale, wengi huwa hawasikilizi
sauti” – Mulugo
Kuhusu kukosea kutaja mwaka, Namkariri naibu waziri akisema “mimi
pale nia yangu ilikua ni kusoma namba moja moja nikashtukia nakwenda
kusoma mbili, haijakaa kama nimekosea kiingereza kama watu wanavyoipanua
kwa mfumo huo lakini kama watu wamenielewa hivyo niombe tu msamaha”
Unaweza kumsikiliza hapo chini kwa maelezo zaidi…