Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwandishi wetu lilitokea Jumatano
iliyopita katika mahakama hiyo ambapo Hakimu Riyad Shamshama alimfutia
mashitaka mtuhumiwa huyo na kumuachia huru kutokana na makosa
yaliyofanyika wakati wa kumfungulia kesi hiyo.
Hakimu huyo aliuambia upande wa mashitaka kuwa, kama wanataka kumbadilishia mashitaka mtuhumiwa, wanatakiwa kumsubiri nje ili wamkamate na kumfungulia mashitaka upya.
Kama walivyoshauriwa, baada ya kutoka nje, polisi walimkamata Abdullatif wakati akikumbatiana na ndugu zake waliokuwa wakiamini kuwa kesi hiyo imekwisha.

Polisi walimsweka Abdullatif katika mahabusu ya mahakama hiyo ili
kujiandaa kumpeleka kituoni na kisha katika ofisi ya mwendesha mashitaka
mkuu kwa ajili kumfungulia kesi upya.
Hali hiyo iliwafanya baadhi ya ndugu waliokuwepo mahakamani hapo kububujikwa na machozi kwani awali walishaanza kuchekelea.