Skip to main content

HIKI NDO CHANZO CHA AJALI YA SHARO MILIONEA PAMOJA NA SIKU KAMILI YA MAZISHI

 Habari za uhakika kuhusiana na chanzo cha kifo cha msanii Hussein Ramadhan a.k.an Sharo milionea ni kwamba gari yake aina ya Toyota harrier ilipata pancha tairi la upande wa kulia na kukosa mwelekeo kisha ikaacha njia na kuelekea mtaroni lakini ule mtalo haukuizuru sana gari hiyo ikaruka na kuingia katika shamba la maindi.

 Kitu kilichoshangaza wengi ni sehemu ambayo si hatarishi sana kiudereva sababu iko tambarare na kona si kali eneo hilo.
 
 Chanzo cha habari kinaendelea kufafanua kuwa baada ya gari kuacha njia ilienda kugonga mti mkubwa na kuung'oa baada ya kuuchana katikati kutokana na gari ilivyokuwa mwendo kasi.

Mwili wa marehemu ulitupwa nje ya gari baada ya kugonga mti huo ambapo gari hiyo iliharibika vibaya kuanzia kwenye roof hadi vioo vyote kupasuka japo vizuizi vilifunguka lakinini havikusaidia.
 Kishindo kikubwa cha mlio wa pancha kilisikika kwa wakazi wa kijiji hiko na kuamua kujitokeza kujua nini kimejili pale na wakati wanafika hapakuwa na mwili wa marehemu katika  eneo la tukio,ndipo mama mmoja aligundua mwili wa msanii huyo mita chache kutoka gari ilipogonga mti na kuharibika vibaya.

 Mganga mkuu wa hospitali teule ya Muheza amesema kuwa chanzo cha kifo cha Sharo ni kubonyea kwa kichwa ikiambatana na majeraha yaliopo kichwani na sehemu ya mabega ndiyo yalipelekea msanii huyo kupoteza maisha papo hapo.

 Hata hivyo jeshi la polisi lilikuja masaa mawili baada ya kutokea ajali hiyo,ambapo gari la Tanesco ndilo lililotumika kuvuta gari hiyo hadi kituo cha polisi wilayani humo.


Mwili wa Sharo utazikwa kesho jioni .


Popular posts from this blog

Goog music from tng jojo yatakwisha hii apa

DownLoad Na Sikiliza Joint Mpya Ya Squizer Ft Belle 9 - Mtemi Pesa

MAJINA YA WASHIRIKI NA WA WEZESHAJI WA FILM YA HOUSE GIRL!

CAST SELEMANI MOHAMED / BUNTO ANDREW / C-O YORAM MWETA / MGANGA MWANTUMU / MKE WA C-O JOHN / MCHUNGAJI BI FURURATU / JINI WAOMBOLEZAJI SAUMU HUSENI HASHIMU BABA RASTA MAN YOHANNA TAMILWAI SAIDI MWALUBADU SEMY STIR SELEMANI MOHAMEDI  AND ANDREW C-O LOCATION ATHUMANI HAMADI MAKE UP MWASHAMBA RAMADHANI BEDUI DEREVA DAUDI SPOONSER SAIDI SHABANI AND THE FRESH2012 GLOB SOUND PRODUCER J-B LIGHT YOHANNA TAMILWAI THENK YOU THE FRESH ENERTAINMENT AND THE FRESH2012 BLOG CONTACTS 0653785027 +255714091786 ZAIDI TEMBELEA www.the-fresh.blogspot.com ADRESS Thefresh@ymail.com AU Saidshabani60@gmai.com