Skip to main content

HUYU NDIE ANASEMA SIASA ZA WAZIRI MEMBE NI ZA KINAFIKI, ANAFANYA MCHEZO WA KIHUNI NA ANAHUSIKA KUMCHAFUA RAIS KIKWETE

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi CCM, HUSSEIN BASHE
Mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa wa CCM Hussein Bashe amefikia hatua hiyo ya kumtaja Benarnd Membe kutokana na vipeperushi vinavyodaiwa kusambazwa Dodoma kwamba Bashe na kundi lake limepanga kuwashawishi wajumbe wa mkutano mkuu kupiga kura za maruhani ili Rais Kikwete asiwe na uongozi wa kofia mbili ikiwemo ile ya Uenyekiti wa Taifa wa CCM.
BASHE amesema kwa mfumo wa kiuongozi ndani ya CCM ni mwendawazimu pekee anayewaza kwamba suala hilo linawezekana na kwamba kauli iliyotolewa na mmoja wa kada wa chama hicho AGUSTINO MATEFU juu ya kumpunguzia kura rais ni mkakati uliopangwa ili kumdhalilisha Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Ili kuondoa utata wa juu ya anayehusika kuwatuma vijana wanaoeneza chuki na makundi ndani ya CCM, Bashe amemtaja mmoja wa Mawaziri wa awamu ya hii kwamba anaendesha mchezo mchafu ili kujisafishia njia ya Urais 2015.
Wakati hayo yakitokea tayari maandalizi ya shughuli za ufunguzi wa mkutano mkuu zimekamilika na wajumbe wameshawasili Dodoma tayari kuwachagua viongozi mbalimbali katika Ukumbi wa mikutano wa Kizota.
Namkariri Bashe akisema “anaewatumia hawa vijana ni Benard Membe ndio anaefanya huu mchezo wa kihuni ambao amekua akiufanya kwa muda mrefu ndani ya chama chetu, nilisema aache michezo hii… ameweza kubakia kwenye siasa za CCM kwa muda mrefu kwa kugawa watu, huu ni sehemu ya mpango wake amekua akitumia vijana hawa, kama mlikuepo hapa Dodoma wakati tunafanya uchaguzi wa vijana alikuja mpambe wake mkubwa kabisa ndugu Nyalandu kutuletea vurugu katika ukumbi wa uchaguzi
Kwenye line ya pili Bashe amesema “nataka kutumia fursa hii kumwambia Membe kwamba sina mpango wa kumnyima kura rais Jakaya bali nina mpango wa kumnyima yeye kura, kura yangu hatopata, kura ya wale wote wanaoweza kunielewa hatopata na kama atashinda NEC atashinda kwa kura za watu wengine na sio kura ya Hussein Bashe, kwa muda mrefu Membe amekua akisurvive kwa siasa za unafiki na uongo ndani ya chama chetu na bahati mbaya viongozi wanafamu, ni mwendawazimu tu anaeweza kufikiri ndani ya chama chetu tunaweza kufikiria tumuweke mwenyekiti mwingine na rais mwingine, huyo atakua aidha ana matatizo ya akili ama sio mwanachama wa CCM”
Kuhusu kipeperushi, Bashe amesema “kwanza kipeperushi hicho hata kukiona sijakiona, hakuna mpango huo na sijawahi kufikiri kuendesha hujuma/mkakati dhidi ya rais Jakaya Mrisho Kikwete”

Popular posts from this blog

MAJINA YA WASHIRIKI NA WA WEZESHAJI WA FILM YA HOUSE GIRL!

CAST SELEMANI MOHAMED / BUNTO ANDREW / C-O YORAM MWETA / MGANGA MWANTUMU / MKE WA C-O JOHN / MCHUNGAJI BI FURURATU / JINI WAOMBOLEZAJI SAUMU HUSENI HASHIMU BABA RASTA MAN YOHANNA TAMILWAI SAIDI MWALUBADU SEMY STIR SELEMANI MOHAMEDI  AND ANDREW C-O LOCATION ATHUMANI HAMADI MAKE UP MWASHAMBA RAMADHANI BEDUI DEREVA DAUDI SPOONSER SAIDI SHABANI AND THE FRESH2012 GLOB SOUND PRODUCER J-B LIGHT YOHANNA TAMILWAI THENK YOU THE FRESH ENERTAINMENT AND THE FRESH2012 BLOG CONTACTS 0653785027 +255714091786 ZAIDI TEMBELEA www.the-fresh.blogspot.com ADRESS Thefresh@ymail.com AU Saidshabani60@gmai.com

Sababu ya Alicia Keys kumuita mwanae Misri (Egypt)

Siku chache kabla ya Mother’s Day Alicia Keys alihojiwa kwenye talk show iitwayo  ‘The Conversation’ inayotayarishwa na Demi Moore na mtangazaji akiwa Amanda de Cadenet. Waliongea mengi kuhusu maisha yake kama mama, umbo lake baada ya kuzaa, kunyonyesha na sababu iliyomfanya amuite mwanae Misri. “Well, Misri ilikuwa safari muhimu katika maisha yangu” Alisema Alicia. Ilikuja katika pointi ambayo nilikuwa nimefanya kazi mno bila kupumzika na sikuwa na idea yoyote kuhusu kuchukua likizo ya kweli na ilikuja katika muda huo ambao niliihitaji.  Hivyo nilipoenda, ilinipa nguvu sana, ikanifungua macho, safari ya kihistoria, yenye nguvu na experience ya pekee iliyonifanya niipende Misri.  Alicia, Demi na Amanda Hivyo  ulipokuja wakati wa kumpa jina mtoto wetu, nililipenda, wote tulilipenda na tuliamua miezi kadhaa hata kabla hajazaliwa” Egypt na baba yake Swizz Beatz Kuhusu kwanini alienda peke yake nchini Misri alisema “Muda huo nilihitaji sana kwenda

Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Dk John Magufuli   Dar es Salaam.   Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge. Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012. Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni. “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba