Lord Eyez (kulia) akiwa na wakili wake wakati wakiongea na waandishi wa habari |
Mweusi
toka A- City, Lord Eyez amekutana na waandishi wa habari akiwa na
wakili wake ili kuzungumzia kesi inayomkabiri ya wizi wa vifaa vya gari
ambayo ili-make headlines sana siku kadhaa zilizopita.
Lord
eyez amesema yeye kwa sasa anaiachia mahakama ambayo ndiyo itaweza
kuchukua maamuzi ya kisheria kama yeye alihusika ama hakuhusika katika
wizi huo wa vifaa vya gari.
Wakili
wa msanii huyo anayejulikana kwa jina la Peter Kibatala amesema kesi
hii imefanya mpaka Lord Eyez kuonekana kwamba yeye ndiye mhusika wa wizi
wa vifaa hivyo lakini kwa sasa hivi wanaiachia kwanza mahakama ndiyo
itakayoweza kuchukua uamuzi sahihi kuhusiana na kesi hiyo.
Hizi
kauli za mweusi huyu na wakili wake zinaonekana zimepimwa na ruler ya
kisheria kwa sababu ni kosa kisheria kujadili kesi ambayo iko mahakamani
(commenting on a pending case).
Weusi
nao walisema ‘neno’ kuhusu tuhuma zinazomkabili member huyo na kwamba
tukio hili limewaathili hasa pale wanapokutana na watu mbalimbali na
kusikia story toka kwa watu kwamba wote watakuwa wanahusika katika tukio
hilo wakati ni story ambazo sio za kweli.
Kesi hiyo inatarajiwa kusomwa katika mahakama ya mwanzo jijini Dar es Salaam tarehe 13, 14 na 15 mwezi huu wa Novemba.
Hata
hivyo the N2N soldier amesema kwa sasa anachotaka kufanya ni
kudondonsha ngoma yake mpya kali ambayo anataka kufanya ‘surprise’ kwa
mashabiki wake katika industry ya muziki wa Bongo.
Lord
eyez alituhumiwa na msanii mwenzake Ommy Dimpoz kuwa alishirikiana na
wenzake kumuibia vifaa vya gari lake na tuhuma hizo nzito ambazo ni pigo
kwa kundi la weusi kiujumla zilipelekea Lord Eyez kukamatwa na
kushikiliwa kwa na jeshi la polisi kwa siku kadhaa na baadae kufunguliwa
kesi mahakamani ambapo alipewa dhamana.