Maelfu ya wachimba migodi wa
Afrika Kusini wamekataa kurejea kazini, katika kampuni ya dhahabu nyeupe
kubwa kabisa duniani iitwayo Anglo American, Amplats
Mwezi Oktoba Amplats iliwafukuza makazini wachimba migodi 12,000 kwa sababu walishiriki kwenye mgomo katika migodi ya Rustenberg.
Tangu wakati huo uchimbaji wa dhahabu nyeupe umeathirika sana.
Amplats ni kampuni kubwa ya mwisho ya Afrika Kusini ambayo bado inaathirika na migomo - migomo iliyokuwa na ghasia ambapo watu zaidi ya 50 wamekufa.
Wachimba migodi 34 walipigwa risasi na polisi katika mgodi wa kampuni ya Lonmin mwezi wa Agosti.