Skip to main content

ASKARI ALIYEPIGA PICHA NA LEMA ATOROKA JESHINI

JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema askari anayedaiwa kuwa jeshi hilo aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ametoroka. Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema jana kwamba pamoja na hatua yake ya kutoroka, jeshi litaendelea kumsaka kwa udi na uvumba ili kumhoji na kujiridhisha kama kweli ni mwanajeshi wake kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Kifungu cha 147 cha Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya 1977. “Huyu kijana inasemekana alishawahi kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), lakini wakati tunaendelea na uchunguzi alitoroka katika nyumba aliyokuwa amepanga bila ya taarifa kwa baba mwenye nyumba,” alisema Kanali Mgawe na kuongeza: “Askari huyo alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga mita chache karibu na Kituo cha Polisi cha Simanjiro, Arusha na alikuwa akijishirikisha na ulinzi shirikishi.” Alipoulizwa jina la askari huyo, Kanali Mgawe alijibu: “Yeye alikuwa anafahamika mtaani hapo kwa jina la kamanda.” Hata hivyo, Kanali Mgawe alisema jeshi hilo litahakikisha linatoa ripoti kamili kwa umma baada ya kumkamata na uchunguzi kukamilika ili kuondoa utata uliogubika suala hilo. Alipoulizwa kama kuna tofauti gani kati ya mwanajeshi kuingia kwenye mikutano ya wanasiasa na wale wanaofanya kazi za kisiasa kama wakuu wa wilaya na mikoa, Kanali Mgawe alijibu:” Wanajeshi wanaofanya kazi za U-DC au RC, wanaruhusiwa kisheria.” Alifafanua kuwa iwapo mwanajeshi atateuliwa kufanya kazi katika taasisi yeyote ya Serikali nje ya jeshi, atatakiwa kuvua magwanda ya jeshi na kufanya kazi hiyo mpaka atakapomaliza muda wake na baada ya hapo ataruhusiwa kurejea jeshini. “Kuna kitu kinaitwa ‘secondment.’ Mwanajeshi anaruhusiwa kufanya shughuli zozote nje ya jeshi iwapo atahitajika kufanya hivyo. Ila kwa masharti ya kuvua magwanda, hivyo wananchi wasishangae kuwaona baadhi ya askari wetu ni wakuu wa wilaya na mikoa na baadaye kurudi jeshini kuendelea na majukumu yao,” alisema Kanali Mgawe na kuongeza: “Askari akiwa katika majukumu yake mapya, atafanya kazi zote atakazopewa zikiwamo za kisiasa kama ilivyo kwa wakuu wa wilaya na mikoa, lakini akirudi jeshini, anarudi kuwa askari mwenye utii na kufuata kanuni za jeshi zisizofungamana na siasa.”

Popular posts from this blog

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2013 wilaya ya tanga mjini pekee!!!

ARAFAH ENG-MED PRIMARY SCHOOL - P2007029 AVICENNA ENG -MD PRIMARY SCHOOL - P2007051 AZIMIO PRIMARY SCHOOL - P2007032 BOMBO PRIMARY SCHOOL - P2007001 BURHANI ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007055 CHANGA ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007033 CHANGA PRIMARY SCHOOL - P2007002 CHUDA PRIMARY SCHOOL - P2007034 CHUMA PRIMARY SCHOOL - P2007003 CHUMBAGENI PRIMARY SCHOOL - P2007004 DARAJANI PRIMARY SCHOOL - P2007005 DAYSTAR ENG - MD PRIMARY SCHOOL - P2007053 DONGE PRIMARY SCHOOL - P2007035 EBEN EZER ENG- MD PR SCHOOL - P2007048 ECKERNFORDE ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007044 GOFU-JUU PRIMARY SCHOOL - P2007006 INDIAN OCEAN ENG-MED PR SCHOOL - P2007049 JABIR BIN ZAID ENG- MED PRIMARY SCHOOL - P2007052 JUHUDI PRIMARY SCHOOL - P2007036 KANA CENTRAL ENGMED PRIMARY SCHOOL - P2007054 KANA PRIMARY SCHOOL - P2007007 KISOSORA PRIMARY SCHOOL - P2007008 KOMBEZI PRIMARY SCHOOL - P2007009 KWAKAEZA PRIMARY SCHOOL - P2007026 KWANJEKA PRIMARY SCHOOL - P2007010 MABAW...

MAJINA YA WASHIRIKI NA WA WEZESHAJI WA FILM YA HOUSE GIRL!

CAST SELEMANI MOHAMED / BUNTO ANDREW / C-O YORAM MWETA / MGANGA MWANTUMU / MKE WA C-O JOHN / MCHUNGAJI BI FURURATU / JINI WAOMBOLEZAJI SAUMU HUSENI HASHIMU BABA RASTA MAN YOHANNA TAMILWAI SAIDI MWALUBADU SEMY STIR SELEMANI MOHAMEDI  AND ANDREW C-O LOCATION ATHUMANI HAMADI MAKE UP MWASHAMBA RAMADHANI BEDUI DEREVA DAUDI SPOONSER SAIDI SHABANI AND THE FRESH2012 GLOB SOUND PRODUCER J-B LIGHT YOHANNA TAMILWAI THENK YOU THE FRESH ENERTAINMENT AND THE FRESH2012 BLOG CONTACTS 0653785027 +255714091786 ZAIDI TEMBELEA www.the-fresh.blogspot.com ADRESS Thefresh@ymail.com AU Saidshabani60@gmai.com

Video: Blackchild – Put Inside

David Abdulichel, also known as BlackChild is a Ghanaian from Asanti origin, born and raised in Lagos Nigeria. BlackChild, who is a recording artist, song writer and performer started his music career back in 2000 and since then has released four singles. He has also worked with top producers in Nigeria such as Fliptyce, Spanky, Meca E & BrainMix to mention but few. BlackChild Abdul rose to prominence with his hit songs “Treasure”, “Ele” featuring Rock Steady, “Could It Be Love” featuring Cartiar, “All I Need” featuring Solid Star. This time around he comes out with “Put Inside” which sees him delivering lines in french and his native language and is steadily generating buzz and enjoying airplay on radio stations within and outside Lagos. Listen up!