Skip to main content

Ndege ya Tanapa yaanguka, yajeruhi rubani

  NDEGE ndogo ya abiria mali ya Hifadhi ya Taifa ya Tanapa  yenye uwezo wa kubeba  watu  wanne aina ya C 182, imeanguka katika  eneo la Kasimba  umbali wa kilometa moja  kutoka katika  Uwanja wa Ndege wa Mpanda  uliopo katika Mkoa wa Katavi  na kumjeruhi rubani wa ndege hiyo.
Akizungumza na vyombo vya habari, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, Maulid  Mohamed alisema ajali  hiyo  ilitokea jana  majira saa 10 .55 jioni  katika   eneo la Kasimba lililopo ndani ya Kijiji  cha Nsemlwa   wilayani hapo.
Mohamed aliitaja ndege hiyo iliyoanguka na kusababisha majeraha kwa rubani aliyetajwa kwa jina la Adam Athuman Kajwaa kuwa  ni aina ya C182.
Mohamed  alieleza kuwa  ndege  hiyo   ilikuwa imetoka  katika uwanja wa ndege wa Mpanda ikielekea  katika Hifadhi ya Wanyamapori  ya Katavi.   
Hata hiyo alisema kuwa ajali hiyo  ilitokea   umbali wa  kilometa  moja na  nusu  kutoka Uwanja wa Ndege wa Mpanda  mara  baada  ya  kuondoka  katika uwanja huo ambapo imeharibika sana sehemu ya bawa lake na upande wa injini.
Meneja wa uwanja  huo wa ndege  alisema  taarifa za awali   zinaonyesha  chanzo   cha ajali  hiyo  kilitokana na kufeli kwa  injini  ya ndege  na kuwa rubani wa ndege hiyo   alipata msaada  wa kuokolewa na  wananchi  waliokuwa  wakifanya  shughuli  za  kilimo  kwenye  mashamba.
Mmoja wa  wa mashuhuda wa tukio hilo Credo Mwanisenga   alieleza  kuwa wakati   akiwa  anafanya shughuli  zake  za kilimo  ghafla  aliona  ndege  hiyo ikiwa  angani  ikizimika  na baada ya  muda  mfupi   ikaanguka   jirani  na mti wa mwembe.
Hata hivyo alisema kuwa zoezi la kumuokoa rubani huyo lilichukua muda kuanza kutokana na mti wa mwembe  kuwa na nyuki wengi.
Hata hivyo  alisema mara baada ya   kufanikiwa kumtoa  rubani  huyo,   huku akiwa  amepata  majerahi makubwa sehemu ya  uso  na maumivu  sehemu ya kifua   na kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa matibabu zaidi,
Pia akiwa anakohoa damu,  rubani huyo aliwahishwa  haraka katika Hospitali ya wilaya ya Mpanda baada ya kupata  msaada wa gari la meneja wa uwanja wa ndege aliyefika  eneo   la tukio.

Popular posts from this blog

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2013 wilaya ya tanga mjini pekee!!!

ARAFAH ENG-MED PRIMARY SCHOOL - P2007029 AVICENNA ENG -MD PRIMARY SCHOOL - P2007051 AZIMIO PRIMARY SCHOOL - P2007032 BOMBO PRIMARY SCHOOL - P2007001 BURHANI ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007055 CHANGA ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007033 CHANGA PRIMARY SCHOOL - P2007002 CHUDA PRIMARY SCHOOL - P2007034 CHUMA PRIMARY SCHOOL - P2007003 CHUMBAGENI PRIMARY SCHOOL - P2007004 DARAJANI PRIMARY SCHOOL - P2007005 DAYSTAR ENG - MD PRIMARY SCHOOL - P2007053 DONGE PRIMARY SCHOOL - P2007035 EBEN EZER ENG- MD PR SCHOOL - P2007048 ECKERNFORDE ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007044 GOFU-JUU PRIMARY SCHOOL - P2007006 INDIAN OCEAN ENG-MED PR SCHOOL - P2007049 JABIR BIN ZAID ENG- MED PRIMARY SCHOOL - P2007052 JUHUDI PRIMARY SCHOOL - P2007036 KANA CENTRAL ENGMED PRIMARY SCHOOL - P2007054 KANA PRIMARY SCHOOL - P2007007 KISOSORA PRIMARY SCHOOL - P2007008 KOMBEZI PRIMARY SCHOOL - P2007009 KWAKAEZA PRIMARY SCHOOL - P2007026 KWANJEKA PRIMARY SCHOOL - P2007010 MABAW...

Coastal ipo tayari kuanza ligi kuu, yashinda 3-0 ikiwa kambini Moshi.

Wachezaji wa Coastal Union wakifanya mazoezi mepesi muda mfupi kabla ya kukabiliana na Machava FC kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi, anayeonekana pichani mwenye jezi namba 17 ni haruna Moshi 'Boban'. Mtokeo ya mechi hiyo ni ushindi wa 3-0 kwa Wagosi. Mazoezi yamekolea, uwanja wa Ushirika Moshi. Uhuru Suleiman amesifiwa na kocha kuwa ni kiungo mwenye kasi nyingi na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. Mshambuliaji anayetumia mguu wa kushoto kutoka Uganda, Yayo Lutimba Kato amefunga bao lake la kwanza tangu kujiunga na Coastal Union ambayo imeweka kambi mjini Moshi tangu jana. Kato ambaye ametoka URA inayoshiriki ligi kuu nchini Uganda, alipatia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Machava FC kwenye uwanja wa Ushirika mjini humo, bao hilo alilifunga kwa ufundi mkubwa katika kipindi cha pili baada ya kupokea pasi murua na kupiga shuti kali akiwa nje ya 18. Akitoa taarifa kutoka Moshi, mwenyekiti wa Wagosi Hemed Hilal ‘Aurora’ amesema “Katika dakika za lal...

Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Dk John Magufuli   Dar es Salaam.   Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge. Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012. Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni. “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. T...