Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2013

UEFA CHAMPIONS LIGI 2013/2014

Group A: Manchester United, Shakhtar Donetsk, Bayer Leverkusen, Real Sociedad. Group B: Real Madrid, Juventus, Galatasaray, FC Copenhagen. Group C: Benfica, Paris Saint-Germain, Olympiacos, Anderlecht Group D: Bayern Munich, CSKA Moscow, Manchester City, Viktoria Plzen Group E: Chelsea FC, Schalke 04, Basel, Steaua Group F: Arsenal FC, Marseille, Borussia Dortmund, Napoli. Group G: FC Porto, Atletico Madrid, Zenit St. Petersburg, Austria Wien. Group H: Barcelona, AC Milan, Ajax,Celtic."

WAASI WA M23 WAMUUA MWANAJESHI WETU WA JWTZ HUKO KONGO

TAARIFA KUHUSU TUKIO LA KUFARIKI KWA AFISA WA JWTZ KATIKA JUKUMU LA KULINDA AMANI - DRC, GOMA 1. Kama mnavyofahamu, JWTZ linashiriki katika operesheni za Umoja wa Mataifa huko Goma DRC. Kikosi chetu kimeendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda amani kama kinavyopangiwa na Jeshi la Umoja wa Mataifa nchini DRC lijulikanalo kama MONUSCO. 2. Tarehe 28 Agosti 2013 wanajeshi wetu wakiwa katika eneo lao la Ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na kusababisha majeruhi. Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu, na hali zao zinaendelea vizuri. 3. MONUSCO inaandaa utaratibu wa kuleta mwili wa marehemu. Imetolewa na: Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi. Dar es Salaam.

Coastal ipo tayari kuanza ligi kuu, yashinda 3-0 ikiwa kambini Moshi.

Wachezaji wa Coastal Union wakifanya mazoezi mepesi muda mfupi kabla ya kukabiliana na Machava FC kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi, anayeonekana pichani mwenye jezi namba 17 ni haruna Moshi 'Boban'. Mtokeo ya mechi hiyo ni ushindi wa 3-0 kwa Wagosi. Mazoezi yamekolea, uwanja wa Ushirika Moshi. Uhuru Suleiman amesifiwa na kocha kuwa ni kiungo mwenye kasi nyingi na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. Mshambuliaji anayetumia mguu wa kushoto kutoka Uganda, Yayo Lutimba Kato amefunga bao lake la kwanza tangu kujiunga na Coastal Union ambayo imeweka kambi mjini Moshi tangu jana. Kato ambaye ametoka URA inayoshiriki ligi kuu nchini Uganda, alipatia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Machava FC kwenye uwanja wa Ushirika mjini humo, bao hilo alilifunga kwa ufundi mkubwa katika kipindi cha pili baada ya kupokea pasi murua na kupiga shuti kali akiwa nje ya 18. Akitoa taarifa kutoka Moshi, mwenyekiti wa Wagosi Hemed Hilal ‘Aurora’ amesema “Katika dakika za lal

KAULI YA FAMILIA YA AGNESS MASOGANGE MAADA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO AFRIKA KUSINI

  FAMILIA ya Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ inadaiwa kumwachia Mungu ishu ya binti huyo kukamatwa na madawa ya kulevya Julai 5, mwaka huu nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa ndugu mmoja wa familia hiyo aliyeomb a jina lake lisitiriwe, wameamua kumwachia Mungu ishu hiyo kwani ndiye anayejua ukweli. “Unajua baba wa Masogange (mzee Gerald Waya) ni mlokole, sasa amekabidhi ishu nzima mikononi mwa Mungu kwa hiyo hayuko tayari kusemasema maneno ambayo hayatakuwa na faida,” alisema ndugu huyo. Habari zinazidi kudai kwamba, mzee huyo aliwahi kuchukizwa na kitendo cha binti yake huyo kujiingiza kwenye sanaa, hadi kuonekana akinengua kwenye muziki.

MZEE GURUMO ASTAAFU MUZIKI,AMWAGA CHOZI. SOMA ALICHOKISEMA HAPA

Mzee Muhidin Gurumo (katikati) akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kustaafu rasmi kazi ya muziki katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni mdau wa muziki Juma Mbizo na Meneja wa Msondo Ngoma, Said Kibiriti (kushoto). (Picha na Magreth Kinabo). Mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma Mzee Muhidin Gurumo leo amestaafu rasmi kazi ya muzika alioifanya kwa muda wa miaka 53. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mzee  Gurumo mwenye umri wa miaka 73 amesema ameamua kustaafu kazi hiyo kwa hiari yake mwenyewe kutokana na umri wake kuwa mkubwa. Mzee Gurumo amesema “Muziki kwangu umekuwa kama asili yangu na kazi yangu lakini nimeamua kustaafu kutokana na umri wangu na nitabaki kuwa mshauri tu kwa mwanamuziki yeyote atakayetaka ushauri wangu”. Pamoja na kufanya kazi ya muziki Gurumo amesema kuwa hakupata mafanikio makubwa zaidi ya kujenga nyumba anayoishi na familia yake. Amesema ameimba kwa muda mrefu sana laki

Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Dk John Magufuli   Dar es Salaam.   Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge. Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012. Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni. “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba

TUKIO LILILOJIRI JIJINI DAR: KILE KIDUME KILICHOPIGA PICHA ZA UTUPU NA MABINTI NA KUZISAMBAZA SASA KIPO MIKONONI MWA POLISI! PICHA HIZI HAPA

Jeshi la polisi kanda ya Dar es Salaam linadaiwa kumtia mbaroni msanii anaetuhumiwa kupiga picha chafu na wanawake mchanganyiko wakiwema mamiss maarufu na baadae kusambaza kwenye mitandao yote ya kijamii pamoja na kuripotiwa kwenye magazeti pendwa.  Gazeti hili katika upekenyuaji wake limenasa picha hizi kwenye mtandao mmoja maarufu wa kijamii ukimuonesha Manaiki akiwa kwenye kibano kikali cha polisi huku akiwa amevishwa pingu na kurukishwa kichurachura. Habari za uhakika  zinasema kuwa msanii huyo aliyeshiriki kwenye filamu za Tikisa, Love Position, Last Coin na Sory my Soni alikamatwa siku chache baada kuvuja kwa picha zake za aibu zikimuonesha akiwa na wanawake tofauti tofauti. Aidha picha zaidi za tukio hilo la kukamatwa kwa Manaiki na haikufahamika kama alikamatwa kwa kosa jingine tofauti na kosa la kudhalilisha wanawake ambapo hali hiyo iliwalazimu waandishi wetu kufatilia kwa ukaribu tukio hilo la kukamtwa kwa msanii huyo aliyejitapia usataa

SOMA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO HAPA!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .