NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameita kambini wachezaji 24 kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu nchini humo.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameita kambini wachezaji 24 kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu nchini humo.
Wachezaji
hao wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 29 mwaka huu kabla ya saa 1
kamili usiku. Kambi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager itakuwa kwenye hoteli ya Accommondia jijini Dar es Salaam.
Makipa
walioitwa katika timu hiyo Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam),
Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris
(Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Nadir Haroub
(Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar) na David
Luhende (Yanga).
Viungo
Khamis Mcha (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Dilunga (Ruvu
Shooting), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Haruna Chanongo
(Simba), Amir Kiemba (Simba), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva
(Yanga), John Boko (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo) na Juma Liuzio (Mtibwa Sugar).
