Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata amezindua Mtandao kwa ajili ya Watu kuripoti moja kwa moja kwake taarifa za matukio ya rushwa.
Watumiaji wa Mtandao huo watakuwa wakiweka picha za mnato na video pia na vielelezo vingine na kuelekeza malalamiko yao katika idara mbalimbali za serikali zilizoorodheshwa.
Pia watu watapata fursa ya kupeleka malalamiko yao juu ya vitendo vya rushwa kwa kutumia ujumbe mfupi wa maandishi moja kwa moja kwenda kwa Rais Kenyata.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Transparency International ni nadra kwa Watu kutoa taarifa juu ya vitendo vya rushwa nchini Kenya kwa kuwa wanahisi kuwa hakuna hatua zozote zitakazochukuliwa.
Kenya ni inaelezwa kuwa nchi ya 139 kati ya 176 zilizo katika nchi yenye rekodi ya kuhusika na vitendo vya rushwa.
Rais Kenyatta analenga kuisafisha Serikali yake na kupambana dhidi ya vitendo vya rushwa nchini Kenya.