Skip to main content

20 wauawa kwa shambulio Somalia


Moja ya mashambulio nchini Somalia

Karibu watu ishirini wameuawa katika shambulio la kujitoa mhanga kwenye kituo cha polisi nchini Somalia.
Shambulio hilo limetokea katika mji wa Beledweyne karibu na mpaka na Ethiopia. Mashuhuda wameiambia BBC kuwa gari lilipiga lango kuu la kuingia kwenye jengo la polisi na kulipuka kabla ya watu wenye silaha kushuka na kushambulia jengo hilo kwa risasi. Taarifa zinasema wengi waliofariki katika shambulio hilo ni maafisa wa polisi.

Wapiganaji wa kiislamu wa Al Shabaab wamekiri kuhusika na shambulio hilo. Mwezi uliopita wapiganaji hao wa Al Shabaab pia walikiri kuhusika na shambulio jingine ambapo watu 16 waliuawa katika hoteli moja maarufu mjini Mogadishu.Mwandishi wa habari wa BBC nchini Somalia Mohammed Moalimu amesema kituo hicho cha polisi kipo karibu na ngome ya majeshi ya Umoja wa mataifa yaliyopo nchini Somalia AMISOM.
Maafisa wa polisi nchini Somalia wamesema mlipuko huo ulikuwa ni mkubwa na umesababisha majeruhi kadhaa.
"Mlipuko ulikuwa ni mkubwa na pia wapo majeruhi kadhaa, hata hivyo hali imedhibitiwa," amesema Kanali Abdulkadir Ali, kamanda wa polisi wa mji huo wakati akiongea na shirika la habari la AFP.
Kamanda wa kundi la Al Shabaab Mohamed Abu Suleiman ameliambia shirika la AFP kuwa makomandoo wa Al Shabaab ndio waliofanya shambulio hilo.
Naye Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema shambulilo hilo ni la kujimaliza na linaonyesha kutojali maisha.
"Kipau mbele changu cha kwanza ni kutuma salamu za rambi rambi kwa waathirika na familia zilizoguswa na tukio hilo la kipumbavu", alisema katika taarifa yake
"Nimesema ni shambulio la kipumbavu kwa sababu maadui zetu wanapaswa kuelewa kwamba mashambulizi hayatawasaidia kuendeleza harakati zao zaidi sana yanawapotosha"

Mwezi Septemba, kundi la Al Shabaab lilisema kuwa lilifanya shambulizi la kigaindi katika kituo cha biashara cha Westgate nchini Kenya ambapo watu wapatao 67 waliuawa.

Popular posts from this blog

Goog music from tng jojo yatakwisha hii apa

DownLoad Na Sikiliza Joint Mpya Ya Squizer Ft Belle 9 - Mtemi Pesa

MAJINA YA WASHIRIKI NA WA WEZESHAJI WA FILM YA HOUSE GIRL!

CAST SELEMANI MOHAMED / BUNTO ANDREW / C-O YORAM MWETA / MGANGA MWANTUMU / MKE WA C-O JOHN / MCHUNGAJI BI FURURATU / JINI WAOMBOLEZAJI SAUMU HUSENI HASHIMU BABA RASTA MAN YOHANNA TAMILWAI SAIDI MWALUBADU SEMY STIR SELEMANI MOHAMEDI  AND ANDREW C-O LOCATION ATHUMANI HAMADI MAKE UP MWASHAMBA RAMADHANI BEDUI DEREVA DAUDI SPOONSER SAIDI SHABANI AND THE FRESH2012 GLOB SOUND PRODUCER J-B LIGHT YOHANNA TAMILWAI THENK YOU THE FRESH ENERTAINMENT AND THE FRESH2012 BLOG CONTACTS 0653785027 +255714091786 ZAIDI TEMBELEA www.the-fresh.blogspot.com ADRESS Thefresh@ymail.com AU Saidshabani60@gmai.com