Skip to main content

CINDY RULZ:- WASANII WA KIKE WANAOIMBA RNB WAMEANZA KUELEWEKA LAKINI NA HIPHOP HAITOCHUKUA MUDA KUELEWEKA BONGO



Rapper toka Bongo CORRINE MARY a.k.a CINDY RULZ ametoa pongezi na shukurani zake za dhati kwa wasanii wenzake wa kike ambao humpa ushirikiano kwa kuzisambaza nyimbo zake mpya mara kwa mara katika mitandao ya kijamii na media mbalimbali.




Akipiga Stori na kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba hapa Bomba FM Mbeya, hitmaker huyo wa Unstoppable, Party ya Cindy na Lets wait CINDY RULZ amesema licha ya muziki wa hiphop bongo kuwa na wadau wachache wanaousapoti lakini anatambua fika haitochukua muda muziki huo kuteka mashabiki wengi kutokana na kufuata misingi.




“Sasa hivi nachoshukuru Mungu ni kwamba wako more supportive wote female rappers ambao nawafahamu kawa wapo CHIKU K kuna DIVAwote tumekuwa response, maana nakumbuka hata nilipotoa hii Cover, isitoshe ali-post kwenye mitandao yake ya kijamii, CHIKU K alikuwa anaandika Status yaani ndo iko hivyo. Kwa sasa hivi tupo pamoja zaidi tunaandaa kitu kwa pamoja wote sisi sote wanne kwa hiyo siwezi kusema ni competition zaidi tunajitahidi kujisukuma sisi wenyewe ka wenyewe, lakini ukiangalia hao wengine sijui wanaoimba RNB  nini naweza nikasema kwamba it nice wameanza kueleweka zaidi kuliko sisi na sisi ndiko tunakoelekea” alisema CINDY RULZ




Kwa hatua nyingine Rapper CINDY RULZ ameweza kuelezea mikakati na ahadi alizopewa baada ya ngoma ya Lets Wait aliyomshirikisha DUNGAkuwekwa kwenye tovuti ya kimataifa www.hotnewhiphop.com na blogs mbili za Dearth Chambers na Grime Culture na kueleza furaha yake “(Anaanza kwa kucheka) kwanza sikutegemea kabisa kwa sababu unajua na-rap kwa Kiswahili  kwa hiyo ni tofauti kwa huko kuweza kuelewa hiyo lugha, lakini nacho shukuru Mungu  ndo hivyo walinitumia email wakasema wamependa quality ya nyimbo hata kama wao walikuwa wao walikuwa hawaelewi naongea nini, lakini delivery yangu iliwafurahisha niweze kusema kwa hiyo wakasema watakuwa wananisapoti  niendelee kutuma nyimbo zangu huko”.
BOFYA HAPA CHINI KUSIKILIZA MAHOJIANO ZAIDI. 

Popular posts from this blog

MAJINA YA WASHIRIKI NA WA WEZESHAJI WA FILM YA HOUSE GIRL!

CAST SELEMANI MOHAMED / BUNTO ANDREW / C-O YORAM MWETA / MGANGA MWANTUMU / MKE WA C-O JOHN / MCHUNGAJI BI FURURATU / JINI WAOMBOLEZAJI SAUMU HUSENI HASHIMU BABA RASTA MAN YOHANNA TAMILWAI SAIDI MWALUBADU SEMY STIR SELEMANI MOHAMEDI  AND ANDREW C-O LOCATION ATHUMANI HAMADI MAKE UP MWASHAMBA RAMADHANI BEDUI DEREVA DAUDI SPOONSER SAIDI SHABANI AND THE FRESH2012 GLOB SOUND PRODUCER J-B LIGHT YOHANNA TAMILWAI THENK YOU THE FRESH ENERTAINMENT AND THE FRESH2012 BLOG CONTACTS 0653785027 +255714091786 ZAIDI TEMBELEA www.the-fresh.blogspot.com ADRESS Thefresh@ymail.com AU Saidshabani60@gmai.com

Sababu ya Alicia Keys kumuita mwanae Misri (Egypt)

Siku chache kabla ya Mother’s Day Alicia Keys alihojiwa kwenye talk show iitwayo  ‘The Conversation’ inayotayarishwa na Demi Moore na mtangazaji akiwa Amanda de Cadenet. Waliongea mengi kuhusu maisha yake kama mama, umbo lake baada ya kuzaa, kunyonyesha na sababu iliyomfanya amuite mwanae Misri. “Well, Misri ilikuwa safari muhimu katika maisha yangu” Alisema Alicia. Ilikuja katika pointi ambayo nilikuwa nimefanya kazi mno bila kupumzika na sikuwa na idea yoyote kuhusu kuchukua likizo ya kweli na ilikuja katika muda huo ambao niliihitaji.  Hivyo nilipoenda, ilinipa nguvu sana, ikanifungua macho, safari ya kihistoria, yenye nguvu na experience ya pekee iliyonifanya niipende Misri.  Alicia, Demi na Amanda Hivyo  ulipokuja wakati wa kumpa jina mtoto wetu, nililipenda, wote tulilipenda na tuliamua miezi kadhaa hata kabla hajazaliwa” Egypt na baba yake Swizz Beatz Kuhusu kwanini alienda peke yake nchini Misri alisema “Muda huo nilihitaji sana kwenda

Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Dk John Magufuli   Dar es Salaam.   Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge. Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012. Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni. “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba