Skip to main content

Hichi ndicho alichokisema yule producer aliyefukuzwa kazi na Wema Sepetu kwa Uzinzi

Hichi ndicho alichokisema yule producer aliyefukuzwa kazi na Wema Sepetu kwa UzinziBaada ya juzi kati kuripotiwa habari ya aliyekuwa producer ama mtengenezaji wa vipindi vya Wema Sepetu Chidi Mohamed kufukuzwa kazi kutokana na kulitumia gari la kampuni kama sehemu yake ya kuvunjia amri ya sita na wadada wa mjini, hatimaye katika pitapita zetu za mtandaoni tuliweza kukutana na kauli ya producer huyo akizungumzia habari hiyo ya yeye kufukuzwa kazi kwenye kampuni ya Endless Fame ya wema sepetu.
Chidi mwenyewe anasema kuwa habari hizo si za kwel na ni kwamba wote walioandika wamepanga kumchafua tuu kwa kuogopa kuwa anaweza kuyaniika mambo mazito yanayoendelea huko endless Fame
Kwa mujibu wa chidi anasema kuwa yeye ameondoka kwenye Kampuni hiyo siyo kwa sababu ya uzinzi ngani ya gari kama ilivyoripotiwa bali ni kutokana na sababu hizi kuu mbili.
1Ameona hamna jipya na wala hamna maendeleo yoyote ndani ya Kampuni hiyo ndio maana ameamua kuondoka

2. Wafanyakazi wa Endless Fame hawalipwi kabisa ndio maana yeye akaamua kujitoa kwani anafanya kazi bure na pia sio yeye peke yake aliyeondoka bali kuna wafanyakazi zaidi ya watatu walioondoka kwenye kampuni hiyo ila nashangaa ni kwanini wameamua kumchafua yeye?
Bado tunafanya mawasiliano na Endless Fame ili tujue kama daia haya ni ya kweli au la

Popular posts from this blog

Goog music from tng jojo yatakwisha hii apa

DownLoad Na Sikiliza Joint Mpya Ya Squizer Ft Belle 9 - Mtemi Pesa

Tugumiane tanga flevani 10_00AM-12_00PM 106.1Mhz @mwambaofm_ fm radio tanga