Skip to main content

Mataifa ya cecafa tayari kwa michuano


Mashindano ya GOtv Cecafa Senior Challange yatang’oa nanga siku ya Jumanne huku timu 12 zikishiriki kwenye mashindano hayo yanayo husisha timu kutoka kanda ya za Afrika Mashariki na  Kati.
Makocha wa timu zote wamewaita kambini wachezaji wao bora wakiwemo wale wanaocheza ugenini ili kuongeza nafasi zao za kushinda kombe hilo.

Mechi zitachezwa katika miji ya Nairobi, Kisumu, Nairobi na Machakos huku serikali za wilaya zikitoa udhamini na kushawishi kumbi ambapo mechi hiyo itaandaliwa- kwa kurejelea mashindano ya vilabu bingwa ya mwaka huu yalioandaliwa katika miji ya darfur na kusini mwa kordofan nchini sudan.Hela pia zitatolewa kama zawadi zimepangiwa ambapo kitita cha dola 100,000 zitagawanywa kati ya washindi watatu bora na hii ni baada ya kampuni ya Gotv kutoa udhamini wa dola 125,000 za kimarekani.
Mashindano ya cecafa yamesalia kuwa chanzo cha furaha katika soka haswa kwa mashabiki wa eneo la afrika magharibi na kati haswa ikizingatiwa kuwa timu kutoka eneo hili hazijapata nafasi ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa kutokana na viwango duni vya soka nchini.
Ukosefu wa wadhamini umesababisha kubadilishwa kwa jina la mashindano ya mechi za cecafa mara kwa mara kwa heshma za wadhamini.
Tanzania wamewaita washambulizi wa TP mazembe Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata ili kuonyesha uzito wa mashindano ya mwaka huu.
Mashindano ya klabu bingwa yameitwa baada ya rais wa Rwanda Paul Kagame huku Senior Challenge yakipewa jina la bwenyenye wa Ethiopia Sheikh Mohammed al Amoud kati ya 2005 na 2006.
Mashindano ya mwaka huu yatakayoisha tarehe 5 Disemba yanajumuisha timu 11 za kanda na Zambia ambao ni wageni.
Kundi A linajumuisha Kenya, Ethiopia, Sudan kusini na Zanzibar, kundi B ni Tanzania, Zambia, Burundi na Somalia, kundi C linahusisha mabingwa watetezi Uganda, Rwanda, Sudan na Eritrea.
Ni timu 4 pekee zimeweza kufuzu kwa kombe la Afrika katika mda wa miaka 10 huku 1 pekee ikishiriki hatua ya makundi.
Rwanda na Kenya zilifika Tunisia 2004, Sudan ilishiriki fainali Ghana 2008 na 2012 huko Equitorial Guinea huku Ethiopia ikishiriki Afrika Kusini 2013.
Cecafa ilianzishwa mwaka 1926 wakati huo ikijulikana kama Kombe la Gossage wa utawala wa ukoloni Kenya, Uganda,Tanganyika na Zanzibar, lakini mwaka wa 1967 ilibadilishwa jina na kuwa senior challenge cup na imekua ikiandaliwa mara kwa mara lakini imeshindwa kuhamasisha ushindani jambo ambalo limechochea mjadala kulifanya shindano hili kuwa la kuendeleza timu za vijana.

Popular posts from this blog

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2013 wilaya ya tanga mjini pekee!!!

ARAFAH ENG-MED PRIMARY SCHOOL - P2007029 AVICENNA ENG -MD PRIMARY SCHOOL - P2007051 AZIMIO PRIMARY SCHOOL - P2007032 BOMBO PRIMARY SCHOOL - P2007001 BURHANI ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007055 CHANGA ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007033 CHANGA PRIMARY SCHOOL - P2007002 CHUDA PRIMARY SCHOOL - P2007034 CHUMA PRIMARY SCHOOL - P2007003 CHUMBAGENI PRIMARY SCHOOL - P2007004 DARAJANI PRIMARY SCHOOL - P2007005 DAYSTAR ENG - MD PRIMARY SCHOOL - P2007053 DONGE PRIMARY SCHOOL - P2007035 EBEN EZER ENG- MD PR SCHOOL - P2007048 ECKERNFORDE ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007044 GOFU-JUU PRIMARY SCHOOL - P2007006 INDIAN OCEAN ENG-MED PR SCHOOL - P2007049 JABIR BIN ZAID ENG- MED PRIMARY SCHOOL - P2007052 JUHUDI PRIMARY SCHOOL - P2007036 KANA CENTRAL ENGMED PRIMARY SCHOOL - P2007054 KANA PRIMARY SCHOOL - P2007007 KISOSORA PRIMARY SCHOOL - P2007008 KOMBEZI PRIMARY SCHOOL - P2007009 KWAKAEZA PRIMARY SCHOOL - P2007026 KWANJEKA PRIMARY SCHOOL - P2007010 MABAW...

Coastal ipo tayari kuanza ligi kuu, yashinda 3-0 ikiwa kambini Moshi.

Wachezaji wa Coastal Union wakifanya mazoezi mepesi muda mfupi kabla ya kukabiliana na Machava FC kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi, anayeonekana pichani mwenye jezi namba 17 ni haruna Moshi 'Boban'. Mtokeo ya mechi hiyo ni ushindi wa 3-0 kwa Wagosi. Mazoezi yamekolea, uwanja wa Ushirika Moshi. Uhuru Suleiman amesifiwa na kocha kuwa ni kiungo mwenye kasi nyingi na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. Mshambuliaji anayetumia mguu wa kushoto kutoka Uganda, Yayo Lutimba Kato amefunga bao lake la kwanza tangu kujiunga na Coastal Union ambayo imeweka kambi mjini Moshi tangu jana. Kato ambaye ametoka URA inayoshiriki ligi kuu nchini Uganda, alipatia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Machava FC kwenye uwanja wa Ushirika mjini humo, bao hilo alilifunga kwa ufundi mkubwa katika kipindi cha pili baada ya kupokea pasi murua na kupiga shuti kali akiwa nje ya 18. Akitoa taarifa kutoka Moshi, mwenyekiti wa Wagosi Hemed Hilal ‘Aurora’ amesema “Katika dakika za lal...

Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Dk John Magufuli   Dar es Salaam.   Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge. Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012. Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni. “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. T...