Skip to main content

MSANII SAYNAG AELEZA KUWA KIFO CHA MAMA YAKE NDIO CHANZO CHA UKIMYA LAKINI KWA SASA YUPO MBIONI KURUDI KATIKA GEMU(AUDIO)


Saynag katika pozi.

Hitmaker wa Inatosha, Nafsi inauma SAYNAG ABRIHHAN a.k.a SAYNAG amesema sababu za ukimya wake katika gemu umetokana na matatizo ya kifamilia baada ya kufiwa na Mama yake mzazi.

Akipiga stori na Chumba Cha Sindano kupitia Kipindi cha Kali za Bomba cha Kituo cha redio Bomba FM Mbeya, SAYNAG ameeleza kuwa “kuna watu wanajua mimi nilifikwa na matatizo na msiba, kuna wengine hawajui hilo suala yaani yote hayo ni kutokana na matatizo ambayo marehemu mama yangu alikuwa nayo. Kwanza alikuwa anaumwa sana kwa hiyo nilikuwa sina muda wa kuingia studio kurekodi, kichwa change chote kilikuwa kina muwaza kwanza mama yangu, nilikuwa nataka apate afueni kwanza halafu niendelee na kazi zangu lakini haikuwa riziki kwa hiyo pia nikazindi kuchanganyikiwa kwamba nimemkosa pamoja na jitihada zangu, sikuwa na muda wa kufikiria kutoa nyimbo kwa wakate ule, sikuwa na muda wa kufikiria show, siku na muda wa kufikiria chochote zaidi ya kile kitu ambacho kilichokuwa kinaniumiza,  lakini hayazoeleki ila kutokana na hali halisi inabidi nikubaliane na hali halisi ilivyo kwa sasa inabidi niendelee tu na kazi zangu, lakini ni mtu aliyekuwa ananipa sapoti kubwa katika kazi zangu”.

Aidha SAYNAG amesema kuna changamoto nyingi ambapo kwa baadhi ya wasanii wenzake wenye menejimenti za uhakika wapo radhi wamzipe mtu Fulani atoke mtu Fulani kwa ushwawishi wa nyimbo kutopata airtime katika vituo vya redio na Tv kwa wasanii wengine wasio na menejimenti.
 “Lakini naamini kama wewe msanii unajua nini unachokifanya unaendelea tu kufanya kama mimi au watu wengine ambao hawasimamiwi au wanajisimamia mwenyewe, Kipaji mimi kama nakipaji  changu najiamini sehemu wowote hata kama mtu ataamua anizibe mimi lakini still wapo wanaokubali na wanataka uwepo kila siku siangalii nani yupo chini nani yupo juu mimi naangalia kazi yangu na mashabiki wanahitaji kitu gani, mara nyingi nilikuwa nasikia sana mashabiki wanalalamika kwenye mainternet kwamba sijatoa nyimbo mbona niko kimya, wanaona kama nimeacha gemu ni kipaji ambacho ninacho mwenyewe yaani, sifosiwi namaanisha sitafuti mtu anitungie, kwa maana kwamba amesusa kunitungia sasa hivi  wimbo, kwa hiyo nimeamua kunyamazwa kwa sababu sinanyimbo ya kutoa hapana, natunga mwenyewe natafuta melody mwenyewe, kwa hiyo ni kitu ambacho ninacho milele siwezi kukiacha kwa hiyo wao wasubirie tu sasa hivi nipo vizuri nitaachia track niliyomshirikisha BEKA sambamba na video niliyofanya na BLUE.
BOFYA HAPA CHINI KUMSIKILIZA ZAIDI SAYNAG.

Popular posts from this blog

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2013 wilaya ya tanga mjini pekee!!!

ARAFAH ENG-MED PRIMARY SCHOOL - P2007029 AVICENNA ENG -MD PRIMARY SCHOOL - P2007051 AZIMIO PRIMARY SCHOOL - P2007032 BOMBO PRIMARY SCHOOL - P2007001 BURHANI ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007055 CHANGA ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007033 CHANGA PRIMARY SCHOOL - P2007002 CHUDA PRIMARY SCHOOL - P2007034 CHUMA PRIMARY SCHOOL - P2007003 CHUMBAGENI PRIMARY SCHOOL - P2007004 DARAJANI PRIMARY SCHOOL - P2007005 DAYSTAR ENG - MD PRIMARY SCHOOL - P2007053 DONGE PRIMARY SCHOOL - P2007035 EBEN EZER ENG- MD PR SCHOOL - P2007048 ECKERNFORDE ENG-MD PRIMARY SCHOOL - P2007044 GOFU-JUU PRIMARY SCHOOL - P2007006 INDIAN OCEAN ENG-MED PR SCHOOL - P2007049 JABIR BIN ZAID ENG- MED PRIMARY SCHOOL - P2007052 JUHUDI PRIMARY SCHOOL - P2007036 KANA CENTRAL ENGMED PRIMARY SCHOOL - P2007054 KANA PRIMARY SCHOOL - P2007007 KISOSORA PRIMARY SCHOOL - P2007008 KOMBEZI PRIMARY SCHOOL - P2007009 KWAKAEZA PRIMARY SCHOOL - P2007026 KWANJEKA PRIMARY SCHOOL - P2007010 MABAW...

Coastal ipo tayari kuanza ligi kuu, yashinda 3-0 ikiwa kambini Moshi.

Wachezaji wa Coastal Union wakifanya mazoezi mepesi muda mfupi kabla ya kukabiliana na Machava FC kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi, anayeonekana pichani mwenye jezi namba 17 ni haruna Moshi 'Boban'. Mtokeo ya mechi hiyo ni ushindi wa 3-0 kwa Wagosi. Mazoezi yamekolea, uwanja wa Ushirika Moshi. Uhuru Suleiman amesifiwa na kocha kuwa ni kiungo mwenye kasi nyingi na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. Mshambuliaji anayetumia mguu wa kushoto kutoka Uganda, Yayo Lutimba Kato amefunga bao lake la kwanza tangu kujiunga na Coastal Union ambayo imeweka kambi mjini Moshi tangu jana. Kato ambaye ametoka URA inayoshiriki ligi kuu nchini Uganda, alipatia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Machava FC kwenye uwanja wa Ushirika mjini humo, bao hilo alilifunga kwa ufundi mkubwa katika kipindi cha pili baada ya kupokea pasi murua na kupiga shuti kali akiwa nje ya 18. Akitoa taarifa kutoka Moshi, mwenyekiti wa Wagosi Hemed Hilal ‘Aurora’ amesema “Katika dakika za lal...

Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Dk John Magufuli   Dar es Salaam.   Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge. Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012. Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni. “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. T...