Takriban watu 11 wameuawa Magharibi mwa Mali wakati wa mapigano kati ya wapiganaji wa kiislamu na jeshi.
Mkaazi moja kwenye mji wa Nara, alisema kuwa watu hao waliwasili kwa magari na pikipiki mapema asubuhi ambapo walipandisha bendera yenye maandishi ya kiarabu.
Walioshuhudia walisema kuwa wanajeshi walijibu ambapo kulitokea ufyatulianaji wa risasi karibu na msikiti na kituo kimoja cha afya.
Shambulizi hilo linafanyika baada ya waasi wa kiarabu na wale wa Tuareg kutia sahihi makubaliano ya amani na serikali ya Mali.