Skip to main content

Jokate Aoga Mvua ya MATUSI Toka kwa Mashabiki



Mwanamitindo  na Msanii wa Bongo Fleva, Jokate Mwegelo, maarufu kama ‘Kidoti’ amejikuta akiambulia matusi ya nguoni kwa kosa la kumpongeza msanii mwenzake wa Bongo Fleva, Ali Kiba baada ya kutwaa tuzo tano za Kili Music Awards zilizotolewa mwezi huu jijini Dar.

Mwanadada huyo ameioga mvua hiyo ya matusi katika akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Intagram kwa watu tofauti kwa kile kilichodaiwa kuwa anahaha baada kuachwa na Mbongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’ ambapo ameamua kufanya hivyo ili kuupoza mtima wake na kwa sasa kuna taarifa kwamba Ali Kiba ndiye anayemmiliki mtoto huyo.
 
Baada ya kutokea ishu hiyo, Mwandishi alimtafuta Jokate ili kusikia anazungumziaje hilo ambapo alisema: “Nashindwa kuielewa jamii inataka mtu aishi vipi, lakini yote kwa yote siwezi nikamkandia mtu kwenye muziki wake, kwa upande wangu mimi ni shabiki wa Ali Kiba kwa sababu ninapenda kazi zake na hakuna wa kunizuia kufanya chochote juu yake.”

Popular posts from this blog

NEW JOINT | dayna special nipe nafasi {Audio}

Goog music from tng jojo yatakwisha hii apa

DownLoad Na Sikiliza Joint Mpya Ya Squizer Ft Belle 9 - Mtemi Pesa